Askofu Kakobe: Nipo tayari kukatwa Kichwa kuliko kumuabudu Nyerere, Kosa kubwa ni kuondoa Mipaka ya Tanganyika!

Mhabarishaji

JF-Expert Member
Oct 5, 2010
1,006
598
Katika Ibada Kuu ya Pasaka ya Kanisa la Full Gospel Bible Fellowship (FGBF), Mwenge, Dar-Es-Salaam; wakati wa Neno la Pasaka 20.4.2014, lenye kichwa, "JE, KUIDAI TANGANYIKA NI HALALI KATIKA MPANGO WA MUNGU?" Askofu Mkuu Zachary Kakobe wa Kanisa hilo, pamoja na mambo mengine, alizungumza kuhusu Tanganyika na Nyerere. Video hizi mbili hapa, zitakupa japo kwa ufupi juu ya mambo aliyoyazungumza katika mahubiri yake:


VIDEO NA 1: KAKOBE: "Kila mtu anayepigania kurudi kwa Tanganyika, ana Mungu ndani yake." MUDA WA VIDEO: DAKIKA 5 SEKUNDE 10:



VIDEO NA 2: KAKOBE: "Wako watu ambao wameanza kumfanya Nyerere aonekane kuwa ni Mungu asiyekosea. Hatua hii, inalenga kumfanya Nyerere kuwa kama Rais wa Korea Kaskazini, KIM IL SUNG, ambaye alitangazwa rasmi kuwa Mungu wa Korea Kaskazini, na Rais wao wa milele. Ingawa amekufa miaka kadha iliyopita, mpaka leo bado ni mungu wao na Rais wao wa milele: North Korea's cult of personality - Wikipedia, the free encyclopedia

Kanisa lazima tukatae kufikishwa kwenye ibada hii ya miungu. Na mimi ni wa kwanza kukataa. Nazungumza kwa herufi kubwa, na ninatamka mara kumi, "NYERERE SIYO MUNGU." - MUDA WA VIDEO: DAKIKA 9 SEKUNDE 0:

 
Last edited by a moderator:
Hakika askofu Kakobe anamjua Mungu anayemtumikia si kama vi-askofu vingine uchwara na yule mama tapeli Rwakatare anayejiita mchungaji.
 
Ubarikiwe Mtumishi wa Mungu. NYERERE SI MUNGU!! Ana makosa mengi na tutayasahihisha. Asante Kakobe paaza sauti usiache.
 
Last edited by a moderator:
Kwa mahubiri haya, CCM wanaweza kumnyang'anya uaskofu wake badala yake wakampa mh. Lukuvi.
 
Ahsante mtumishi wa Mungu kwa kutuongezea hamasa ya kuidai nchi yetu ya Tanganyika... Hawa jamaa walitumia uchawi naisi hata sasa tulikuwa hatujioji maswali muhimu kama haya.. sasa tumeifahamu kweli na imetuweka huru....
 
Last edited by a moderator:
Kiongozi wa dini hupaswi kuwa mnafiki...... nashukuru sana kwa mtumishi wa Mungu Kakobe.
 
Ndoa inayoishi kwa nguvu ya tunguli (limbwata) ni huwa haidumu na siku mbwata likiisha nguvu na upendo hupotea ghafla na atimae ndoa huvunjika.

Hii ndoa ya Tanganyika na Zanzibar nahisi waasisi walifanya kitu na sasa inaonekana mbwata limeisha nguvu kwa hiyo ni swala la muda tu matokeo tutayapata soon.
 
What do these two groups have in common na kwanini wanaona njia sahihi ya kufikia malengo yao ni kusema baba wetu wataifa alikuwa na makosa mbele ya vilaza wenzao




Nyerere akuwa kilaza ata chembe alikuwa ni mtu pekee alieilewa Afrika huku tunapoanza kumuona muongo, wanaomuangalia kwa nje na matatizo waliyo nayo wanamuona ilikuwa baraka kwa Tanzania na aliyoyafanya ilibidi kwa mtu mwenye ufahamu wa hata chembe jinsi ilivyo kazi ngumu kujenga taifa lenye makabila chungu mzima na imani tofauti waliofungwa na waliouliwa ilibidi. Mwalimu alisema wazi udini utatumika kutugawa kama taifa la muungano, tukitoka hapo tunarudi kwenye ukabila na udini wa ndani ya mataifa yaliyo gawanyika. Si lazima uwe genius kulijua hilo ni ufahamu tu how easy it is to corrupt the ignorance mind.

Viongozi wa CCM kamwe wasisahau hili agizo la baba yetu wa taifa.

Chama Cha Mapinduzi chenye wanachama wenye akili, na ukweli, na ujasiri, hakiwezi katu kukubali sera ya serikali tatu, kikijua wazi wazi kwamba matokeo na shabaha ya sera hiyo ni kuiua, na kuizika Tanzania. Chama Cha Mapinduzi kikiwa na msimamo huo na wala kisiuonee haya, Tanzania itadumu.
Tunapo elekea ni kubaya na sijui tumewaachia vipi watu hatari wafike hapa, jamani siasa za nyumba za ibada sio nzuri, huko kumejaa watu wajinga tu na wakuchotwa akili kirahisi, kwanini wanachekewa hawa watu.
 
Last edited by a moderator:
Kwa hili, Mungu mwenyewe amekutia ujasiri kulinena kwa nguvu zote, AMINA.
 
M nadhan kakobe anafaa kuwa mwanasiasa zaidi kuliko Mchungaji...

Tatzo langu kwake ni kwa nini anautashi wa kisiasa? Ilihali yy ni anajiita mchungaji?
 
Safi sana mtumishi wa Mungu kwa kuzungumza yaliyo kweli kwa kujiamini.
 
What do these two groups have in common na kwanini wanaona njia sahihi ya kufikia malengo yao ni kusema baba wetu wataifa alikuwa na makosa mbele ya vilaza wenzaoNyerere akuwa -------- alikuwa ni mtu pekee alieilewa Afrika, udini utatumika kutugawa kama taifa la muungano, tukitoka hapo tunarudi kwenye ukabila na udini. Si lazima huwe genius kulijua hilo ni ufahamu tu how easy it to corrupt the ignorance mind.Viongozi wa CCM kamwe wasisahau hili agizo la baba yetu wa taifa.Tunapo elekea ni kubaya na sijui tumewaachia vipi watu hatari wafike hapa, jamani siasa za nyumba za ibada sio nzuri, huko kumejaa watu wajinga tu na wakuchotwa akili kirahisi.
Hata hueleweki unachozungumza labda jitahidi kutulia unyooshe hoja yako tukuelewe vema. Labda kama kuna aliyemwelewa huyu ndugu anamaanisha nini atusaidiae.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom