Bazazi
JF-Expert Member
- Aug 18, 2008
- 2,806
- 3,476
Kama mjuavyo Bazazi ni mzururaji. Katika zungukazunguka yake amekutana na watu wengi ambao wanamuona Askofu Kakobe kuwa ni mtu mtata na wengine kumuona kuwa ni punguani flani. Lakini nilichokiona ni kuwa watanzania wengi ni wapumbafu na wala sio wajinga na wanaburuzika kirahisi sana. >Tafadhalini angalieni nguzo hizo anazolalamikia Kakobe zina umbali gani toka makazi ya raia ilhali WAYLEAVE inayopendekezwa na wataalamu ni mita 7.5 kila upande. >TANESCO ukitaka kuunganisha umeme unalipia waya na mita 463500/= na kama upo umbali wa mita 30 basi utahitaji nguzo ambayo moja wanauza 1,200,000/=. Pamoja na kuwavilipia vitu hivyo bado ni mali ya tanesco.Mtu mwingine ataunganishiwa umeme bila wewe kulipwa angalau kidogo kifidia gharama za nguzo. Bazazi ataendelea kuwa mshabiki wa Askofu KAKOBE na Mchungaji MTIKILA kwani wanatufungua macho acha watu wapumbafu waendelee kuwadharau kwani wamelishwa kasumba/afyuni (mihadharati) na CCM. Aluta continua mapambano bado yanaendelaea