Askofu Kakobe: Mubashara leo sherehe ya ibada ya kutimiza miaka 30 ya kanisa lake

BAOBAO

JF-Expert Member
Oct 12, 2012
1,874
547
UPDATES 1: Television ya Agape wanarusha mubashara sherehe hizi pia.

Askofu Zachary Kakobe ametangaza kwamba Sherehe za Miaka 30 ya Kanisa la Full Gospel Bible Fellowship, zitarushwa livestream kupitia ukurasa wake FACEBOOK maarufu kwa jina la BZKIM [https://www.facebook.com/342053105875881/posts/2192889134125593/ kutoka Kanisa hili Dar-Es-Salaam, leo Jumapili tarehe 5.5.2019, wakati wowote kuanzia saa 3 asubuhi, hadi saa 12 jioni.

Jiweke tayari kufatilia mubashara sherehe hiyo inatarajiwa kuhudhuriwa wageni mbalimbali wakiwemo viongozi wakuu wa taasisi za dini na serikali❗

Niombe tusaidiane kuweka hapa matukio yaliyojiri kwa utukufu wa Mungu kulingana na majukumu ya huduma zetu.

================================

UPDATES 2:
Tayari jeshi la watumishi wa Mungu limeingia katika ukumbi wa kanisa. Yuko Nabii Josephat Mwingira, Askofu Gamanywa, Askofu Gwajima na mhe. Paul Makonda na wengine bado wanaingia na watatoa salamu zao sasa hivi.

===============================

updates 3
Salamu zinaendelea kutolewa na wageni.
Zamu ya mhe. Senior Pastor Anny Fernandes wa kanisa la Agape ambaye ametoa zawadi ya vingamuzi 300 kwa askofu Zachary Kakobe. Tayari Mtume na nabii Mwingira,Askofu Gwajima na Askofu Gamanywa wametoa salamu.

UPDATES 4:
Askofu Zachary Kakobe kumkaribisha mkuu wa mkoa wa Dar Es Salaam,kutoa salamu maalum kwa walioohudhuria sherehe na kwa wakristo kwa ujumla.

MWISHO: Askofu Zachary Kakobe alimkaribisha mtume Peter Nyaga kufunga sherehe kwa maombi;na msafari wa kuondoka ukumbini kumsindikiza mhe.Paulo Makondahuku kanisa likiendelea na shagwe na vigegele na vifijo katika kuhitisha sherehe ya kihistoria.

KARIBU YOUTUBE LIVESTREAM SASA

UPDATES (DATE 26-05-2019)
Bishop Kakobe ameendelea kuweka katika kurasa yake FACEBOOK video na picha matukio ya sherehe za miaka 30 kutoka matawi yote zaidi elfu ya kanisa la Full Gospel Bible Fellowship. Tazama video na picha kwa link https://www.facebook.com/bishopkakobeministries/?ti=as
 
Attachments

  • FB_IMG_1557000456818.jpg
    FB_IMG_1557000456818.jpg
    21.4 KB · Views: 25
  • FB_IMG_1556959648862.jpg
    FB_IMG_1556959648862.jpg
    23.3 KB · Views: 29
  • 1557044946896.mp4
    2.3 MB
  • IMG_20190505_164216_954.jpg
    IMG_20190505_164216_954.jpg
    20.4 KB · Views: 36
  • IMG_20190505_164209_373.jpg
    IMG_20190505_164209_373.jpg
    38.4 KB · Views: 30
  • FB_IMG_1556994472990.jpg
    FB_IMG_1556994472990.jpg
    21.8 KB · Views: 29
Hakuna taasisi , huwezi kuwa na taasisi ya mtu mmoja! Kanisa hilo ni mali ya mfukoni ya Kakobe, wahuni kama wahuni wengine wanaotumia dini kwa wajinga wa Tanzania .....
Kanisa la Full Gospel Bible Fellowship ni taasisi iliyopitia majaribu yaliyofanya kujengeka imara kila itwapo leo.

Tuache chuki na wivu wa kijinga ! Kanisa lina bodi ya wadhamini na baraza KUU la watendaji wenye heshima zao si wahuni kama wewe.
 
Ni kweli MIAKA 30 yapasa kumshukuru kwa kila wema aliotenda kwa kanisa lake na watu wake tangu kuanzishwa kwa IBADA ya kwanza watu 13
Ubarikiwe Mtumishi. Miaka 30 si michache kujenga taasisi.
 
Duh Makonda atakua Mgeni rasmi

Kila mtu yuko huru kushiriki sherehe ya miaka 30 hapa kanisa. Kama mnaropoka ovyo ovyo kama Mhe.Makonda atahudhuria; itakuwaje akihudhuria mhe. Rais John Magufuli kwenye ibada hii ya kumshukuru Mungu ?
 
Attachments

  • FB_IMG_1556627486892.jpg
    FB_IMG_1556627486892.jpg
    18.8 KB · Views: 27
Kanisa la Full Gospel Bible Fellowship ni taasisi iliyopitia majaribu yaliyofanya kujengeka imara kila itwapo leo.

Tuache chuki na wivu wa kijinga ! Kanisa lina bodi ya wadhamini na baraza KUU la watendaji wenye heshima zao si wahuni kama wewe.
Akaunti za benki za hicho mnachokiita kanisa ni jina la mtu mmoja kakobe. Taasisi haiwezi kuwa na akaunti ya mtu mmoja kama signatory! akiondoka zinawekwa kanda, eti hiyo ni taaisis
 
Duh Makonda atakua Mgeni rasmi

Kila mtu yuko huru kushiriki sherehe ya miaka 30 hapa kanisa. Kama mnaropoka ovyo ovyo kama Mhe.Makonda atahudhuria; itakuwaje akihudhuria mhe. Rais John Magufuli kwenye ibada hii ya kumshukuru Mungu ?
Akaunti za benki za hicho mnachokiita kanisa ni jina la mtu mmoja kakobe. Taasisi haiwezi kuwa na akaunti ya mtu mmoja kama signatory! akiondoka zinawekwa kanda, eti hiyo ni taaisis

Tuache upotoshaji ! Tangu lini askofu mkuu Zachary Kakobe ana akaunti benki ? Waulize TRA na kikosi kazi kilichofatilia uzushi kama wako na kupata taarifa ya taasisi ya kanisa la Full Gospel Bible Fellowship. Nenda benki ya NBC watakueleza kuhusu akaunti za kanisa lina jina la nani !
PAMBANA NA HALI YAKO MAANA SISI TUNASHEREKEA MIAKA 30!!!
 
Hongera Sana FGBF Hakika Mungu ni mwema umepitia misukosuko mingi kumbe ilikuwa inakuhimarisha.Natamani kuwepo ila Niko mbali.Nimesali Sana hapo Mwenge.
 
Kila mtu yuko huru kushiriki sherehe ya miaka 30 hapa kanisa. Kama mnaropoka ovyo ovyo kama Mhe.Makonda atahudhuria; itakuwaje akihudhuria mhe. Rais John Magufuli kwenye ibada hii ya kumshukuru Mungu ?
Ukijenga hoja ya kidini usihusishe watu maarufu maana na wenyewe wana mwili wa nyama kama wewe bnadam .. Hata ibilis ana watu wenye hadhi kubwa..
 
UPDATES
Askofu Zachary Kakobe ametangaza kwamba Sherehe za Miaka 30 ya Kanisa la Full Gospel Bible Fellowship, zitarushwa livestream kupitia ukurasa wake FACEBOOK maarufu kwa jina la BZKIM [https://www.facebook.com/bishopkakobeministries/ ]
kutoka Kanisa hili Dar-Es-Salaam, leo Jumapili tarehe 5.5.2019, wakati wowote kuanzia saa 3 asubuhi, hadi saa 12 jioni.

Jiweke tayari kufatilia mubashara sherehe hiyo inatarajiwa kuhudhuriwa wageni mbalimbali wakiwemo viongozi wakuu wa taasisi za dini na serikali❗

Tutaweka hapa matukio yatakayojiri.

KARIBU YOUTUBE LIVESTREAM SASA

BAADHI YA VIDEO CLIPS ZA ASUBUHI BAADA YA SIKUKUU NA KARAMU KUANZA NA MVUA YA BARAKA
 
Attachments

  • 1557044854637.mp4
    4.1 MB
  • 1557046494571.mp4
    4.6 MB
Back
Top Bottom