Askofu Kakobe Asipuuzwe: Ni kama David Koresh na Camp Davidians!

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,428
113,431
Wanabodi,
Saa hizi ni Saa 8:39 za usiku!, yaani usiku wa manane, nimepita nje ya kanisa la Full Gospel Bible Fellowship, la Askofu Zakaria Kakobe, nikashuhudia mamia ya waumini wake wamekaa kwenye viti na meza nje ya kanisa hilo huku limepambwa na disco lights zinazobadilika badilika rangi, kwa mgeni aweza dhania ni night club fulani.

Nimeshauri asipuuzwe kwa sababu mimi ni mmoja ambaye ninatoa ushuhuda jamaa ana nguvu, yaani he has powers! Niliwahi fanya nae mahojiano miaka ya nyuma, nikamuuliza hiyo daraja ya Uaskofu alipewa na nani?. Alijibu na Mungu mwenyewe!. Nikauliza kuhusu tuhuma mbalimbali zinatupwa kwake na watu wa mataifa, zikiwepo yeye kuwa tajiri wakati waumini wake wako kwenye umasikini uliotopea, kuhusu Mkewe kuwa ndio Mweka hazina, kuhusu kama hayupo inawekwa kanda kuhubiri.

Na swali la mwisho nilimuuliza kuhusu ukweli kuwa waumini wake wanavuliwa dhahabu na anaziteketeza kwa moto, nikamuomba angalau anionyeshe lilipo hilo tanuru nishuhudie smelted gold deposits kwa macho yangu mwenyewe.

Askofu alinyamaza, akaniangalia machoni kwa kunikazia macho kama anahasira fulani, nami nikajisikia baridi ya ghafla nikataka kuanza kutetemeka na kusikia kizunguzungu ile staili ambayo hatimaye watu huanguka chini. Nikajishika imara kwenye kiti, nikwamwambia Askofu, nimeyaondoa maswali yangu yote, hana haja ya kuyajibu tena!. End of interview.

Huu ni uthibitisho tosha kuwa Askofu Zakaria Kakobe ananguvu fulani, hivyo sio wa kupuuzwa.

Kitendo cha kuwaona waumini wake kwa mamia, wanalala macho usiku kucha kwa kumsikiliza Askofu wao akiwaamuru kuhakikisha wanaipinga serikali in the name of God, ninaamini hao walala nje, wanalala macho hapo nje kwa imani 100 kwa 100 kuwa huko nako ni kumtumikia Mungu Baba na sio kumtumikia binadamu mwenye jina la Askofu.

Kwa lugha nyingine, Nguvu za Askofu Kakobe zimewahypnotize waumini wake kwa kiwango cha juu, kiasi kwamba, chochote atakachowaambia wafanye, watafanya, ndivyo ilivyokuwa kwa David Koresh na wafuasi wake wa Camp Davidians na Askofu Kibwetere na wafuasi wake ambao mwisho wao wote waliishia kuteketezwa kwa moto na kujilipua kwa mabomu kwa ahadi ya safari ya mbinguni kwenye uzima wa milele, imewadia!.

Kama kuna yoyote ambaye ni muumini ama aliwahi kuwa muumini akatusaidia sisi akina Tomaso, kwa kutupa ushuhuda wa msingi wa nguvu za Baba Askofu Zakaria Kakobe kama ni za Mwanga au za giza ili nasi tumuaminiye na tumfuate, vinginevyo huyu ni mtu mwenye nguvu za ajabu na siyo wa kupuuzwa hata kidogo!.

David Koresh wa Camp Davidian alipuuzwa hivi hivi, Joseph Kibweteere nae alipuuzwa hivi hivi, kilichofuata sote tunakijua.

NB. Mode, hii siyo ya dini na imani, ni ya politics of religion.

Paskali
 
why do people subscribe to things like this. The man preys on people with no hope and difficult troubles in their lives. Shameful really.
 
Huu ndio udaku?? Mi nilifikiri una jipya ? We kama hukunywa chai asubuhi, glucose levels zipo chini ukataka kuanguka unataka kumpa Kakobe mdhamana wa afya yako duni??
 
Ukiwa na imani kama mfano wa punje ya haradani unaweza kuuhamisha hata mlima. believe me.usimfananishe kakobe na kibwetere.

Ni punje ya haradali-Simfananishi Kakobe na Kibwetere nimezungumzia the powers within him, kuwalaza waumini wake nje in the name of God, hivi hao waumini wanaamini kutekeleza wito wa mkuu wao kulala nje kwao ni sehemu ya ibada ama just blind faith?.

Ni hapo kwenye blind faith ilipocapitalize Coresh na Kibwetere.
 
why do people subscribe to things like this. The man preys on people with no hope and difficult troubles in their lives. Shameful really.
Ndio maana nimawashuhudia has powers, ni kweli 'The man preys on people with no hope and difficult troubles in their lives' ndio maana nikauliza huko kuwalaza macho hapo nje ni sehemu ya Ibada?.
 
Kama kila akifanyacho anatumwa na Mungu wake, basi 1995 Mungu wake alishindwa kumuweka madarakani Mrema maana alizunguka na kutuambia "Huyu ndiye yeye yule anayetakiwa"
Naungana nawe Mkuu Pasco, Kakobe asipuuzwe kabla hatujayaona makubwa na tukabaki kujutia yakitokea kama kawaida yetu ya kupuuzia ilivyo.
 
Pasco, hayo ni majungu bwana. Ila sikushangai, Yesu mwenyewe aliambiwa anatoa Pepo kwa nguvu ze Belzebuli, itakuwa Kakobe? Umepita makanisa mangapi ukakuta hawapo makanisani time hizo? Kama haumuamini Kakobe, mwache akae, nyamaza kimya enedelea na kazi zako.
 
Pasco, hayo ni majungu bwana. Ila sikushangai, Yesu mwenyewe aliambiwa anatoa Pepo kwa nguvu ze Belzebuli, itakuwa Kakobe? Umepita makanisa mangapi ukakuta hawapo makanisani time hizo? Kama haumuamini Kakobe, mwache akae, nyamaza kimya enedelea na kazi zako.
Rudi mwanzo na msome Pasco vizuri kabla ya kumjibu. Usiweke mbele hisia zako katika hoja.
 
huyu mzee ''kwa mtizamo wangu'' NINASHAURI ASIPUUZWE!the man is decent,let's be honest people
 
ooops....! i have been kimya to some ishuz but this ''MADE A SNAKE COME OUT''
mleta hoja amejaribu kwa upeo wake kueleza jinsi mtu huyu KAKOBE alivyo na nguvu....! amejaribu pia kuwafananisha na watu anaowajua yeye au watu ambao public itawajua kwa urahisi.
all in all KAKOBE has virtues/powers from above,is a charismatic leader and a follower of JESUS THE CHRIST......!
Yale yafanywayo kwake laiti yangefanywa kwa WATU WA MADHEHEBU FULANI nadhani tunge-expirience something else.KUVUNJIWA KANISA,KUAMBIWA ANAKUSANYA DHAHABU ZA WATU NA MENGINEYO TELE WA TELE.....!
Ukiona simba kalowana usidhani ni paka.....all have been done to this man naye amejaribu kuelezea malalamiko yake kwa maneno tu (diplomatic,peacefully,dialogue) je mtu kama huyu akisema SASA BASI inakuwaje......YOUUUUUUU DECISION MAKERS WATCH OUT.........!
We see some of your decisions yanavyowaumiza watu e.g MAJEMBE SAGA e.t.c
 
Ni punje ya haradali-Simfananishi Kakobe na Kibwetere nimezungumzia the powers within him, kuwalaza waumini wake nje in the name of God, hivi hao waumini wanaamini kutekeleza wito wa mkuu wao kulala nje kwao ni sehemu ya ibada ama just blind faith?.

Ni hapo kwenye blind faith ilipocapitalize Coresh na Kibwetere.

Wewe bwana wacha kupotosha watu humu. Kwani mbona watu wa dini nyingine hukutanika kwa nia mbalimbali na hamuwasemi ??
 
Kama kila akifanyacho anatumwa na Mungu wake, basi 1995 Mungu wake alishindwa kumuweka madarakani Mrema maana alizunguka na kutuambia "Huyu ndiye yeye yule anayetakiwa"
Naungana nawe Mkuu Pasco, Kakobe asipuuzwe kabla hatujayaona makubwa na tukabaki kujutia yakitokea kama kawaida yetu ya kupuuzia ilivyo.

Naungana na Pasco kuwa tuwe wanagalifu na Mtu kama Kakaobe. waumini wake wanaweza kulala mbele ya buldoza ili wafe kuzuia ujenzi wa laini za umeme.
 
Ukiwa na imani kama mfano wa punje ya haradani unaweza kuuhamisha hata mlima. believe me.usimfananishe kakobe na kibwetere.
KAKOBE is a disaster waiting to happen.
Leo akiwaambia waumini wake laleni barabarani watalala.Kunyweni sumu kuprotest watakunywa.
You only have to press Kakobe na athari zake utazipata kwa waumini wake.
Hiyo sehemu anayoipigania hana legal right ya aina yoyote kwa vile iko ndani ya hifadhi ya barabara.
 
Naungana na Pasco kuwa tuwe wanagalifu na Mtu kama Kakaobe. waumini wake wanaweza kulala mbele ya buldoza ili wafe kuzuia ujenzi wa laini za umeme.

Watu humu mnataka kuimba kiitikio cha wimbo hata msiojua. Hivi kuandamana na kusimamia jambo unaloliamini kuna ubaya gani?? Hivi wale wanaoprotest jambo fulani ni lazima wawe wamekuwa brain-washed??
 
Paco uko right kabisa, huyu mtu anahitaji very close watch. na serikali iache kuchanganya vitu, ifuate taratibu za sheria
 
Nimeshauri asipuuzwe kwa sabu mimi ni mmoja ambaye ninatoa ushuhuda jamaa ana nguvu, yaani he has powers! Nliwahi fanya nae mahojiano miaka ya yuma, nikamuuliza hiyo daraja ya Uaskofu alipowe na nani?. Alijibu na Mungu mwenyewe!. Nikauliza kuhusu tuhuma mbalimbali zinatupwa kwake na watu wa mataifa, zikiwepo yeye kuwa tajiri wakati waumini wake wako kwenye umasikini uliotopea, kuhusu Mkewe kuwa ndio Mweka hazina, kuhusu kama hayupo inawekwa kanda kuhubiri.

Na swali la mwisho nilimuuliza kuhusu ukweli kuwa waumini wake wanavuliwa dhahabu na anaziteketeza kwa moto, nikamuomba angalau anionyeshe lilipo hilo tanuru nishuhudie smelted gold deposits kwa macha yangu mwenyewe.

Askofu alinyamaza, akaniangalia machoni kwa kunikazia macho kama anahasira fulani, nami nikajisikia baridi ya ghafla nikataka kuanza kutetemeka na kusikia kizunguzungu ile staili ambayo hatimaye watu huanguka chini. Nikajishika imara kwenye kiti, nikwamwambia Akofu, nimeyaondoa maswali yangu, hana haja ya kuyajibu. end of interview.

Huu ni uthibitisho tosha kuwa Askofu Kakobe ananguvu fulani, yaani psychic powers hivyo sio wa kupuuzwa.

Kitendo cha kuwaona waumini wake kwa mamia, wanalala macho usiku kucha kwa kumsikiliza Askofu wao akiwaamuru kuhakikisha wanaipinga serikali in the name of God, ninaamini hao walala nje, wanalala macho hapo nje kwa imani 100 kwa 100 kuwa huko nako ni kumtumikia Mungu Baba na sio kumtumikia binadamu mwenye jina la Askofu.

Ulichofulia ni kumwangalia usoni. Ulipaswa kuangalia moyo wake. Ungemfaidi zaidi kama ungemuuliza Mungu kibali chake kwanza ili kumvaa mtu huyo na kumuuliza kwa ujasiri. Hakukujibu lakini maswali yako yalikuwa ya kimsingi kabisa ambayo ni kweli yanasemwa nje. Ungekuja nje na majibu ya kuifaa jamii kwa sana. Lakini huenda wewe ulishaijenga nguvu yake mapema, hata alipokuangalia labda hizo "nguvu" alizo nazo zilikukoroga zaidi mpaka ukaamua kufuta maswali. Kwa nini ulifuta? Ulikuwa unamtania?

Sasa angekuja Obama ukamhoji na makachero wake wana silaha zilizochanganyikiwa si ndio ungezimia kabisa?

Nguvu ofcourse lazima anazo, akini ni nguvu gani? Hata Elia alipokutana na wachawi wa Nebukadneza walitisha kwa mbwembwe zao, lakini kwa kuwa alikuwa anajua anamtumikia nani alidiriki kuwadhihaki wachawi wale, mpaka watu wakakiri Mungu wak Elia ni zaidi. Tumeambiwa tuzijaribu kila roho, maana sio zote ni za Mngu zijaposema kazituma Mungu, kwa wengine dini ni biashara safi sana, ndio maana utawala muhimu inashika familia - mtunza pesa mama, msemaji mkuu baba, mkuu wa Kanisa baba, n'k.

Leka
 
Saa hizi ni Saa 8:39 za usiku!, yaani usiku wa manane, nimepita nje ya kanisa la Full Gospel Bible Fellowship, la Askofu Zakaria Kakobe, nikushuhudia mamia ya waumini wake wamekaa kwenye viti na meza nje ya kanisa hilo huku limepambwa na disco lights zinazobadilika badilika rangi, kwa mgeni aweza dhania ni night club fulani.

QUOTE]

Ndugu yangu inawezekana kakobe akawa na nguvu ...lakini kwa kuwa yeye naye ni mwanadamu anaweza kutumia nguvu au ushawishi wake vibaya....hainiingii akilini kuona kakobe anapingana na serikali..bila sababu za msingi..

umeme unapita ndani ya hifadhi ya barabara ambayo inamilikiwa na TANROAD ..ambao wameshawapa kibali TANESCO...ndani ya hifadhi ya barabara ndipo panapohusu upanuzi wa barabara,mitaro,simu,gesi,umeme,maji etc...zote hizo ni huduma za jamii...ambazo ndugu kakobe hazipiti kwenye eneo la miliki yake....isitoshe hata mabango yake ameweka kwenye eneo la TANROADS tena bila kibali chochote...kimsingi kakobe hana haki yeyote pale zaidi nafikiri anazo hasira ....labda kwa kushindwa kuzuia kisheria wakati eneo lake lote la parking la kanisa alilojengaga barabarani lilipobomolewaga wakati wa kupisha upanuzi wa barabara ya Sam nujoma.........

serikali ya kikwete ina staha sana na huruma nadhani ...nafikiri angekuwa ni mkapa angembomolea kama alivomvunjia parking mwaka 2005.....na kakobe anautumia vibaya upole wa kikwete....

jambo lingine ambalo ni hatari kwa usalama ..linalotokea mara ya pili sasa ni la baadhi ya viongozi wa dini kama hawa kutumia misingi ya imani kuwachochea waumini wao kufanya jambo...tuliona wakati viongozi wa dini walipotumia imani kali ya kikristo kuingiza DECI na kuwafanya waamini kuwa DECI ni mkombozi aliyeletwa na YESU.....sasa kakobe anawafanya watu waache kulala makwao na wake zao au waume zao ...wanakesha wanaumwa na mbu kulinda eneo ambalo si la kwao kisheria ....nafikiri iikiendelea hivi badi anao uwezo wa kuwashawishi wajichome moto kama kibwetere[samahani kwa kufikia hapo]...lakini ndiko tunakoelekea kama tutaruhusu watu watumumie imani za waumini wau ..kuwatumikisha watakavyo!!!......

ni bora watu wa usalama wakawa makini na kuibuka kwa fundamenalism ...iwe kwenye christian everngelism au muslim ...zote ni sawa ...pamoja na kuwa ndugu zetu yao inatokuwa movements tofauti na ya wakristo ambayo mtu mmoja anaweza kuwakusanya watu kama mazoba na wakasahau kila kitu na kumfuata yeye....badala ya Mungu!!!
 
Huu ndio udaku?? Mi nilifikiri una jipya ? We kama hukunywa chai asubuhi, glucose levels zipo chini ukataka kuanguka unataka kumpa Kakobe mdhamana wa afya yako duni??

Kaka niamini mimi, lazima Tanesco wafanye mazungumzo na hawa waumini na wasithubutu kujaribu kupitisha nyaya hizo bila ridhaa yao, kama hujaona vita kali jaribu kucheza na imani ya watu.

Hata mi nilipita nikaona wanalala nje nafikiri wana zaidi ya wiki sasa, mtu anayelala nje yupo tayari kwa lolote mkuu

Tanesco ikijaribu kufanya kazi yao kwa nguvu ya serikali basi yatakuwa ya mwembechai mengine.

Ni kweli kakobe ana nguvu - we kama unabisha nenda kaongee na yeye leo utamkuta pale then uje utupatie update.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom