Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 50,468
- 113,583
Wanabodi,
Saa hizi ni Saa 8:39 za usiku!, yaani usiku wa manane, nimepita nje ya kanisa la Full Gospel Bible Fellowship, la Askofu Zakaria Kakobe, nikashuhudia mamia ya waumini wake wamekaa kwenye viti na meza nje ya kanisa hilo huku limepambwa na disco lights zinazobadilika badilika rangi, kwa mgeni aweza dhania ni night club fulani.
Nimeshauri asipuuzwe kwa sababu mimi ni mmoja ambaye ninatoa ushuhuda jamaa ana nguvu, yaani he has powers! Niliwahi fanya nae mahojiano miaka ya nyuma, nikamuuliza hiyo daraja ya Uaskofu alipewa na nani?. Alijibu na Mungu mwenyewe!. Nikauliza kuhusu tuhuma mbalimbali zinatupwa kwake na watu wa mataifa, zikiwepo yeye kuwa tajiri wakati waumini wake wako kwenye umasikini uliotopea, kuhusu Mkewe kuwa ndio Mweka hazina, kuhusu kama hayupo inawekwa kanda kuhubiri.
Na swali la mwisho nilimuuliza kuhusu ukweli kuwa waumini wake wanavuliwa dhahabu na anaziteketeza kwa moto, nikamuomba angalau anionyeshe lilipo hilo tanuru nishuhudie smelted gold deposits kwa macho yangu mwenyewe.
Askofu alinyamaza, akaniangalia machoni kwa kunikazia macho kama anahasira fulani, nami nikajisikia baridi ya ghafla nikataka kuanza kutetemeka na kusikia kizunguzungu ile staili ambayo hatimaye watu huanguka chini. Nikajishika imara kwenye kiti, nikwamwambia Askofu, nimeyaondoa maswali yangu yote, hana haja ya kuyajibu tena!. End of interview.
Huu ni uthibitisho tosha kuwa Askofu Zakaria Kakobe ananguvu fulani, hivyo sio wa kupuuzwa.
Kitendo cha kuwaona waumini wake kwa mamia, wanalala macho usiku kucha kwa kumsikiliza Askofu wao akiwaamuru kuhakikisha wanaipinga serikali in the name of God, ninaamini hao walala nje, wanalala macho hapo nje kwa imani 100 kwa 100 kuwa huko nako ni kumtumikia Mungu Baba na sio kumtumikia binadamu mwenye jina la Askofu.
Kwa lugha nyingine, Nguvu za Askofu Kakobe zimewahypnotize waumini wake kwa kiwango cha juu, kiasi kwamba, chochote atakachowaambia wafanye, watafanya, ndivyo ilivyokuwa kwa David Koresh na wafuasi wake wa Camp Davidians na Askofu Kibwetere na wafuasi wake ambao mwisho wao wote waliishia kuteketezwa kwa moto na kujilipua kwa mabomu kwa ahadi ya safari ya mbinguni kwenye uzima wa milele, imewadia!.
Kama kuna yoyote ambaye ni muumini ama aliwahi kuwa muumini akatusaidia sisi akina Tomaso, kwa kutupa ushuhuda wa msingi wa nguvu za Baba Askofu Zakaria Kakobe kama ni za Mwanga au za giza ili nasi tumuaminiye na tumfuate, vinginevyo huyu ni mtu mwenye nguvu za ajabu na siyo wa kupuuzwa hata kidogo!.
David Koresh wa Camp Davidian alipuuzwa hivi hivi, Joseph Kibweteere nae alipuuzwa hivi hivi, kilichofuata sote tunakijua.
NB. Mode, hii siyo ya dini na imani, ni ya politics of religion.
Paskali