Katiba Mpya: Askofu Kakobe ampelekea Rais Kikwete ujumbe wa wazi kutoka kwa Mungu

Mhabarishaji

JF-Expert Member
Oct 5, 2010
1,006
598
1.jpg

2.jpg

3.jpg
 
Aah, Kakobe kwa vitisho bwana, kama vile JK atamsikia. Humjui JK nini, yeyey atasema ni upepo tu huu wa Bunge la Katiba! Kuna mambo makubwa zaidi ya hili la Wajumbe wa Pentokosti kwenye Bunge la Katiba yamepita na wala JK hakutikisika.
 
Natamani ujumbe huu utimie leo maana hawa CCM wamejitukuza sana kwamba wao wako juu ya kila kitu hawajui taifa letu limekuwepo kabla ya CCM najua siku moja itatoweka bali Tanzania yetu itabaki. Mungu akubariki mtumishi wa Mungu najua hapa mbweha watatoke na dhihaka zao wewe umamaliza kazi uliyotumwa kwamba waamini ama wasiamini.
 
Hivi hule mpango wa kupanua hile barabara ya Mwenge mpaka Ubungo si bado hupo? Au zile nguzo za umeme ambazo zinatakiwa kupita katikati ya lile kanisa.
Naona serikali inaweza kuja na njia ya kuzifufua hizi projects.
 
mhmh mpake 2016 waandishi wa vitabu watakua wamejaza library tayari kwa vizazi vijavyo kusoma historia ndefu ya nchi changa!
 
Haa huu usanii mwingine bwana

Kila mtu anaona na anajua mtifuano uliopo ndani ya CCM, na fujo kubwa kweli itakuwepo wakati CCM itakapo mchinjia Baharini Lowassa

anyway
 
Mh. JK na jopo lako, hii ni habari njema kwenu. Ni vyema mkajikusana mkafanya toba yakweli na kutorejea hiyo dhambi mliyoitenda na hata kuwakwaza wauminin na watumishi wa Mungu. Wengi tunaimani viongozi wetu wanachaguliwa na Mungu, hivyo mkitubu atawasamehe na kuwapa hekima ya kuliongoza Taifa kwa maslahi ya watanzania wote. Mamlaka mliyonayo na Mungu pia anamkono wake, hivyo ni wakati muafaka mkaomba kuongozwa sala ya toba kabla mambo hayajaharibika.
 
Kakobe na siasa!!!

Mimi siyo fan wa Kikwete na kwa muda mrefu tu namrespect sana Kakobe kwa mambo mengine mengi isipokuwa tu yanapokuja maeneo mawili: 1. Kakobe unapenda sana kuwa comfrontationist kwa dini nyingine hata kwa madhehebu mengine ya Kikristo 2. Kakobe unapenda kumhusisha sana Mungu na hisia zako binafsi, na la kufurahisha inaonekana Mungu hajawahi kukubaliana na hisia zako.

Anyway, kwa vile wewe ni msomaji na mjuzi sana wa biblia kuliko mimi mshirika wa kawaida, lakini hata hivyo siamini kwamba vita yenu nyie walokole yapaswa kupiganwa bungeni kwenye majumbe ya katiba. Je Mt. Paulo hakusema vita yenu si ya damu na nyama bali ya roho huku mkipambana na mamlaka zisizoonekana katika ufalme wa giza?

Pambaneni huko huko na Mungu aweza kukushindia bila hata kuwa na uwakilishi bungeni.
 
Duh! Hii kali! Kakobe ni mtumishi wa Mungu ninayemheshimu sana pamoja na mafundisho yake potofu juu ya Ukatoliki lakini hilo halibadili ukweli kuwa ni mtumishi wa Mungu na asipuuzwe!:A S-coffee:

mafundisho yapi potofu aliyofundisha?
 
Back
Top Bottom