Askofu Gwajima yuko njiani anaelekea msiba wa Ndesamburo, Moshi

Upuuzi tu unaleta huku,kweli mzee wetu ametutoka na inatuuma kweli hasa wanamoshi ila sijui gwajima yupo njiani anatuhusu nini sisi yeye ni wa kawaida tu hapo kuna watu wa maana sana tu hapo msibani
 
Tafadhali CCM yeyote au mwenye harufu ya CCM asitie mguu hapo msibani
Sasa kwa coment hii, kama nyie wafuasi wa CCM, na CHADEMA, sasa si mtaombea viongozi wenu maarufu wafe, ili mpate kuwatambia wafuasi wa chama kingine. Maana na like, umeipata kuonyesha wanaunga mkono wazo lako, ila kwetu sisi huko umakondeni, tunaamini, marehemu hana kinyongo. Ndiyo maana msiba, hauna mwaliko.
 
Eeeee Mungu baba tunakuomba epusha asiende akaongelea tena "issue" ya zero brain pale atakapopewa maiki.
 
Muda si punde askofu huyu kiboko ya Bashite ametua uwanja wa KIA tayari kuelekea Moshi kuhudhuria msiba wa babu yetu kipenzi Ndesa pesa.

Mungu awajaalie wote walioko njiani kuhudhuria kumuaga mpendwa wetu.

Daima tutamkumbuka kwa mengi na hasa moyo wake mkunjufu wa kusaidia
Gwajima maisha yake tayari amekwisha "YASETI" (Ameyatengeneza) katika mtiririko wa "SIRIZ" ama ni kama DRAMA kwa sasa...

Maisha ya KIONGOZI huyu anae jitapa kwa UKWASI....ni kama HADITHI ya ISIDINGO (The need)

Toka nikiwa BAROBARO (Kijana nisie na Mpenzi) mpaka leo hii naitwa BABA,
Simulizi bado inaendelea tu..!!

Wakati wengine wanakwenda kuomboleza huyu GWAJIMA anakwenda kutafuta KIKI na NITOKE VIPI na Jumapili ijayo...!?

MTANIAMBIA KITAKACHO FUATA...
 
Sasa kwa coment hii, kama nyie wafuasi wa CCM, na CHADEMA, sasa si mtaombea viongozi wenu maarufu wafe, ili mpate kuwatambia wafuasi wa chama kingine. Maana na like, umeipata kuonyesha wanaunga mkono wazo lako, ila kwetu sisi huko umakondeni, tunaamini, marehemu hana kinyongo. Ndiyo maana msiba, hauna mwaliko.
Chuki mmeianzisha wenyewe CCM. Kuanzia bungeni mpaka kwenye maisha ya kawaida wacha kama ni chuki itamalaki ili CCM mjifunze kwamba chuki haijengi.
 
Chuki mmeianzisha wenyewe CCM. Kuanzia bungeni mpaka kwenye maisha ya kawaida wacha kama ni chuki itamalaki ili CCM mjifunze kwamba chuki haijengi.
Nikuambie tu ndugu yangu, mimi ujinga wa ufuasi wa vyama sina, ingawa siasa inagusa maisha yangu. Mimi ilimradi siku ya kura hawaulizi card ya mwanachama sioni tatizo, sipendi kujifunga upande fulani, mpaka sasa bado sijaona Chama ama mwanasiasa mwenye nia na Tanzania. Kwahiyo mwana furums, mwenzangu usinichukie, ukidhani ni mpinzani wako, ndiyo maana mara nyingi sichangii sana yanayohusu siasa. Hii nimechangia sababu ni msiba, hata wale wapemba walipokua hawazikani sababu ya Siasa, nilichangia, nikiwauliza siasa ina nguvu kuliko Mungu, maana wapemba wanaonekana wacha Mungu.
 
Amekwenda kuwafundisha kkkt ujasiri. Sikiliza hotuba ya mazishi kesho zisivyo na mvuto, linganisha na nyundo za dudee leo
 
Nikuambie tu ndugu yangu, mimi ujinga wa ufuasi wa vyama sina, ingawa siasa inagusa maisha yangu. Mimi ilimradi siku ya kura hawaulizi card ya mwanachama sioni tatizo, sipendi kujifunga upande fulani, mpaka sasa bado sijaona Chama ama mwanasiasa mwenye nia na Tanzania. Kwahiyo mwana furums, mwenzangu usinichukie, ukidhani ni mpinzani wako, ndiyo maana mara nyingi sichangii sana yanayohusu siasa. Hii nimechangia sababu ni msiba, hata wale wapemba walipokua hawazikani sababu ya Siasa, nilichangia, nikiwauliza siasa ina nguvu kuliko Mungu, maana wapemba wanaonekana wacha Mungu.
Kama siasa kwako si lolote nadhani unapoteza muda wako hata kuchangia humu. Endelea na biashara zako.
 
Back
Top Bottom