#COVID19 Askofu Gwajima: Wapo waliochanjwa chanjo feki ili kuwashawishi watu wachanjwe. Sijachanjwa na haitatokea

Shida moja tu ipo siku tutamuona nae amekaa foleni anapokea chanjo alafu anasema sasa tafiti ziko sawa chanjo ni salama wakati ajawai hata kuona panadol ikitengenezwa alafu ndo wako bungeni na sisi tunasubiri maendeleo
 
Ujue wenzio walishaonngezeka Sana Kwa maarifa walikuwa kwenye biological weapons sasa wameenda mbele zaidi biological weapons wameadvance into electromagnetic electronic killings
Mpendwa, kutekeleza "electromagnetic killings" ni rahisi sana. Fungua soketi, shika waya hai kwa mkono wako utapata "electromagnetic killing". Katika majimbo kadhaa ya Marekani walitekeleza hukumu ya mauti kwa miaka mingi kwa njia ya "Kiti cha umeme".

Ila tu - hakuna uhusiano wowote baina ya sumakuumeme na chanjo. (Ukiwa na mfano, lete chanzo ya kitaalamu!)
 
"Wapo wanaowaaminisha watu kuwa wamechanjwa na chanjo haijawaathiri kumbe wamechanjwa chanjo feki ili kuwashawishi watu wachanjwe" -- Askofu Gwajima

Namuona Gwajiboy kwenye Ubora wake sasa.

Haba ubora wowote. Akiombwa aseme ni nani aliyeingiza hizo chanjo mbovu na nani aliyechanja na kuchanjwa hizo feki ni akina na ataweza kusema??

Kama ubora ni kutoa taarifa yoyote tu - tuna kazi kubwa sana!! Na mnaoamini huo ndio ubora mna kazi kubwa zaidi!
 
Haba ubora wowote. Akiombwa aseme ni nani aliyeingiza hizo chanjo mbovu na nani aliyechanja na kuchanjwa hizo feki ni akina na ataweza kusema??

Kama ubora ni kutoa taarifa yoyote tu - tuna kazi kubwa sana!! Na mnaoamini huo ndio ubora mna kazi kubwa zaidi!

..ana bahati yuko CCM, angekuwa Chadema cha moto angekiona.
 
Askofu Gwajima anapata faida kubwa kwa kuendesha ibada za mazishi karibu kila siku, ibada hizo zina sadaka aliyopanga na kila muumini lazima aitoe ili abaki kuwa muumini wake.

Hivyo kwa karibu wiki nzima anaingiza hela mfukoni na kuendelea kutajirika, NDIO SIRI YA YEYE KUKATAA ChANJO.
Hana data zozote za kisayansi kuhusu maoni yake, ila anahofia kwamba endapo waumini wake wakichanjwa basi mpunga utakwisha,atabakiza sadaka za jumapili tu!

Kuna msemo usemao, ya kaisari muachie kaisari, kaisari ni serikali, iachiwe jukumu lake la kulinda afya za watu. Gwajima abaki na jukumu la kulinda afya za kiroho.

Ujanja ujanja was wahubiri jamii ya Gwajima umekwama,Mungu kawaumbua, Gwajima kashindwa kuombea mgonjwa hata mmoja was covid ili apone, hii ni wazi kwamba Mungu anajua kwamba Kaisari na taasisi zake za tafiti wanatosha kutatua tatizo kisayansi. Yesu alithamini mchango was kaisari na hakuupuuza,japo angeweza kufanya hivyo,anajua kwa upande mmoja, Kaisari anafanya kazi aliyokasimiwa na Mungu

Yesu alitembea juu ya maji, kwa imani, lakini kuna kipindi alipanda Mashua/Mtumbwi, mtumbwi ni zao la sayansi, hii haimaanishi hakuwa na imani,sio kila kitu tukipotoshe kwa kisingizio cha imani ya kidini
 
Kwan kabla ya Korona hakuwa na pesa na alipataje sadaka.....!! Twendeni tukachanje
 
Askofu Gwajima amewaambia wafuasi wake katika semina inayoendelea kanisani kwake kwamba wazipuuze taarifa zinazoenea mitandaoni kwamba yeye amechanjwa chanjo ya Corona.

Wapo wanaowaaminisha watu kuwa wamechanjwa na chanjo haijawaathiri kumbe wamechanjwa chanjo feki ili kuwashawishi watu wachanjwe" Askofu Josephat Gwajima

Gwajima amesema yeye hajachanjwa na haitatokea achanjwe.

Chanzo: Semina kanisani kwake




VIPANDE:

Safari hii watu watakufa kama mende
View attachment 1874166

Sisi hatuchanjwi, tutaishi na Corona


View attachment 1874169

Ni CHANJO FEKI, watakufa


View attachment 1875409

Aibu yako Gwajima watu hawajafa kama mende kama ulivyomuomba mungu wako ibilisi ili uzidi kuaminiwa. Tapeli mkubwa wewe kibushuti
 
Back
Top Bottom