Askofu Gwajima: Vita ya kwanza ya dunia iliizaa UN, vita ya pili ikazaa taifa la Israel, Je Corona itazaa nini? Watu wenye akili tunajiuliza

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
47,071
2,000
Askofu Gwajima amesema dunia ina mambo yake na utaratibu wake wa kufikia malengo na usipokuwa na akili basi utapata tabu sana.

Askofu Gwajima amesema vita ya kwanza ya dunia iliyoua watu zaidi ya milioni 20 ilipomalizika ukazaliwa Umoja wa Mataifa ( League of Nations)

Vita ya pili nayo iliuwa watu wengi na ilipomalizika likazaliwa taifa la Israel, Mrengo wa Magharibi na Mrengo wa Mashariki.
Kwa sababu Nyerere alikuwa na akili yeye na wenzake wakajianzishia Umoja wa nchi zisizofungamana na upande wowote.
Hata hivyo Umoja huu ulikuwa na faida 50% na hasara 50% kwa sababu nchi zake zilionekana hazina msimamo.

Askofu Gwajima anasema Watu wenye akili wamejichimbia kwenye maktaba zao wanatafakari hii Corona itazaa nini, na nini itakuwa impact yake kwenye uchumi na siasa

Gwajima amesema anamshauri Rais Samia atafute vijana " wenye akili " wajikite katika hili na kutupa mrejesho ili tuwexe kuvuka.

Chanzo: Ibadani Kanisa la Ufufuo na Uzima

Mungu ni mwema wakati wote!
 

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
47,071
2,000
Viongozi wa dini sometimes kuna vitu wanaviongelea bila ufahamu wa kutosha , mfano ni huyu gwaji boy, kuna mambo mengi ni mawazo yake na anayaongelea kama unabii na mengi haya uelewa nayo kabisa ila anawaaminisha watu...
Tupe mfano bwashee!
 

Jumbe Brown

JF-Expert Member
Jun 23, 2020
7,827
2,000
Ndugu Msigwa ameshasema....

UKIPOTOSHA KUHUSU CHANJO UTAKAMATWA.......

#TujitokezeniKuchanjwa
#ChanjoNiBoraKulikoTiba
 

Interested Observer

JF-Expert Member
Mar 27, 2006
2,135
2,000
Askofu Gwajima amesema dunia ina mambo yake na utaratibu wake wa kufikia malengo na usipokuwa na akili basi utapata tabu sana.

Askofu Gwajima amesema vita ya kwanza ya dunia iliyoua watu zaidi ya milioni 20 ilipomalizika ukazaliwa Umoja wa Mataifa ( League of Nations)..
Fact check:
1. League of Nations baada ya vita kuu ya kwanza
2. UN[O] = 1945, baada ya vita ya pili
3. Israel Nation: 1948
 

Kinyungu

JF-Expert Member
Apr 6, 2008
12,189
2,000
Askofu Gwajima amesema dunia ina mambo yake na utaratibu wake wa kufikia malengo na usipokuwa na akili basi utapata tabu sana.

Askofu Gwajima amesema vita ya kwanza ya dunia iliyoua watu zaidi ya milioni 20 ilipomalizika ukazaliwa Umoja wa Mataifa ( League of Nations)...
Gwajima ana swala/ibada ngapi kwa siku?
 

Dp800

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
1,148
2,000
Ndugu Msigwa ameshasema....

UKIPOTOSHA KUHUSU CHANJO UTAKAMATWA.

#TujitokezeniKuchanjwa
#ChanjoNiBoraKulikoTiba
Nani mwenye kipimo cha kujua upotoshaji na uhalisia?
Nikusaidie tu kati ya vitu vigumu kuvipata dunia ni kweli ndio maana mwana wa adamu alikuja kwayo.
Usim-beze Gwajima wala kumfagilia tumia ufahamu wako kutambua takwa lako
 

Babati

JF-Expert Member
Aug 7, 2014
49,206
2,000
Askofu Gwajima amesema dunia ina mambo yake na utaratibu wake wa kufikia malengo na usipokuwa na akili basi utapata tabu sana.

Askofu Gwajima amesema vita ya kwanza ya dunia iliyoua watu zaidi ya milioni 20 ilipomalizika ukazaliwa Umoja wa Mataifa ( League of Nations)..
We na Gwajima hakuna tofauti
 

zitto junior

JF-Expert Member
Oct 7, 2013
13,755
2,000
Jibu ni moja Tu itazaa Dini moja , stay tuned, na chanjo hii ni lazima , hlo wimbi la tatu ndo litahitimisha ulazima wa chanjo kwenye mahitaj mhimu
Black plague au Spanish Flu ziliua kuliko Corona na World war 1 ila zilizaa nini??

Msipende kuwa watu wa speculation na conspirancy.... Maisha ni process na dunia inapitia mabadiliko sio kila kitu kimepangwa.

Nakumbuka hata Tsunami ya 2004/05 kuna watu walidai ilisababishwa na bomu la nuclear iliyolipuliwa baharini na mabeberu!!!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom