#COVID19 Askofu Gwajima: Ni jambo baya sana kuwapa Chanjo ya Corona Wanajeshi, Polisi na watu wa Usalama

Mkuu, pana wengine hukurupuka tu kupinga hoja bila tafakari. Toka mwanzo umesema HUPINGI hanjo ila si hizi za MRNA! Jamaa kakomaa tu na chanjo chanjo huyu hana tofauti na wanaotupigia kelele za CORONA kana kwamba kirusi hiki kimeanza 2019. Kirusi cha korona kipo duniani hapa miaka nendarudi ila sasa tunapigana na hiki cha CoVid19.
Kaka....ona hii


TAARIFA KWA UMMA. TAHADHARI YA UGONJWA WA NIMONIA INAYOTOKANA NA CORONA VIRUS

Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, imepokea taarifa kutoka Shirika la Afya Duniani (WHO) mnamo tarehe 22 Mei 2013, kuhusu kuwepo kwa ugonjwa wa Nimonia unaosababishwa na kirusi cha Novel Coronavirus.

Taarifa hiyo inaeleza kuwa,tangu ugonjwa huo utokee mwishoni wa mwaka 2012 hadi tarehe 23 Mei 2013 idadi ya wagonjwa wapatao 44 na vifo 22 viliripotiwa

Shirika la Afya Duniani limethibitisha ugonjwa huu kuwepo katika nchi za Mashariki ya Kati yaani Jordan, Qatar, Saudi Arabi na Falme za Kiarabu (UAE). Katika bara la Ulaya, ugonjwa huu umethibitishwa kutokea nchi za Ujerumani, Ufaransa, na Uingereza. Katika bara la Afrika, ugonjwa huu umetokea Tunisia.

Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii inapenda kutoa tahadhari ya Ugonjwa huu kwa wananchi wote, katika mikoa yote ya Tanzania na hasa wale wanaosafiri kuelekea maeneo tajwa yenye uthibitisho wa ugonjwa huu.

Ugonjwa huu unaenezwa na kirusi kiitwacho novel coronavirus (nCoV).

Dalili kuu za ugonjwa huu ni kushindwa kupumua kwa ghafla, homa kali, kukohoa, na kubanwa na mbavu na hatimaye kupata Nimonia.

Dalili nyingine ambazo zinaweza kutokea ni pamoja na kupata maumivu makali ya tumbo pamoja nakuharisha. Vile vile ugonjwa huu unaweza kupelekea figo kushindwa kufanya kazi na hata kusababisha kifo.

Kipindi cha kuonekana kwa dalili za ugonjwa huu ni kati ya siku 2 hadi 10 baada ya kupata maambukizi. Ugonjwa huu hauna tiba wala chanjo.

Ugonjwa huu unaweza kuambukizwa kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine.

Njia za maambukizo bado hazijajulikana ingawa uwezekano mkubwa wa maambukizo ni kwa kwa njia ya hewa (kukohoa/kupiga chafya) au kwa kugusa majimaji/makamasi kutoka kwa mgonjwa aliyethibitishwa kuwa na ugonjwa huo.

Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, imechukua hatua zifuatazo katika kukabiliana na tishio la ugonjwa huu:

Kutoa taarifa ya tahadhari ya ugonjwa huu kupitia kwa Waganga Wakuu wote wa Mikoa na Wilaya kwa Tanzania bara.

Aidha, taarifa hii pia imejumuisha namna mgonjwa anavyoweza kutambuliwa (Ainisho la Ugonjwa),

Fact sheet ya ugonjwa, Mwongozo kwa watumishi wa afya wa namna ya kuchukua sampuli ikiwa ni pamoja na vipeperushi vinavyoelezea jinsi ya kujikinga na maambukizi ya ugonjwa huu.

Kuimarisha ufuatiliaji wa ugonjwa huu kupitia kwa Wataalamu wa Afya katika Mikoa, Wilaya na maeneo ya mipakani. Aidha watalaamu hawa pia wanatoa elimu kwa wananchi kuhusu dalili za ugonjwa huu na jinsi ya kujikinga na maambukizi ili endapo ugonjwa huo utatokea uweze kutolewa taarifa mapema.

Wizara inasisitiza kuwa hakuna vikwazo vyovyote vilivyowekwa kwa ajili kwa wasafiri watakaokwenda au kurudi katika maeneo tajwa yaliyothibitishwa kuwa na ugonjwa huu. Vipeperushi vya ugonjwa huu vimetumwa katika maeneo ya mipakani ili iwapo msafiri anayeondoka au kurudi nchini akiwa na dalili tajwa atoe taarifa kwa watumishi wa afya wa mpakani ili hatua stahili ziweze kuchukuliwa.

Kutoa mafunzo kwa watumishi wa afya na mipakani wa namna ya kutambua na kujikinga dhidi ya maambukizo ya ugonjwa huu pamoja na uchukuaji wa sampuli iwapo mgonjwa atapatikana

Kupeleka vifaa kinga kwa ajili ya watumishi wa afya Wananchi wanashauriwa kutokuwa na hofu kwani mpaka sasa hakuna mgonjwa yeyote aliyeripotiwa nchini. Wizara inapenda kutoa tahadhari kwa wananchi juu ya umuhimu wa

KUNAWA MIKONO VIZURI KWA SABUNI NA MAJI MARA KWA MARA na pia KUZUIA MDOMO NA PUA KWA KITAMBAA AU KARATASI LAINI WAKATI WA KUKOHOA AU KUPIGA CHAFYA.

Pia wananchi wanashauriwa kutoa taarifa kwenye kituo cha kutolea huduma za afya kilicho karibu mara watakapoona mgonjwa yeyote atakayehisiwa kuwa na dalili za ugonjwa huu.

Imetolewa na;

Nsachris Mwamwaja
Kitengo cha Mawasiliano ya
Serikali
30/05/2013

Screenshot_20210727-010031.jpg
 
Mtu analeta Teolojia kwenye Sayansi, ajabu Sana hii

Baadhi ya watu wanafikiri kusoma clinical studies ni ushetani. Hawajui kuwa Mungu ndio anatoa vipaji na hekima za watu kuwa mahiri kwenye fani za clinical studies and research.

Mbaya zaidi Watanzania nao wanaamini hoja mfu za kuwachukia wasomi wa clinical sciences wanaposisitiza umuhimu wa chanjo. #Maajabu!

IMG-20210726-WA0075.jpg
 
Acha KUOKOTEZA OKOTEZA fake news kutoka vyanzo vya habari visivyo na CREDIBILITY na REPUTATION ni sawa kuchukua habari toka vyanzo vya magazeti ya UDAKU na kuleta habari hizo hapa. Narudia tena 97% ya wanaolazwa mahospitalini ni wale ambao ni unvaccinated ina only 3% ya wale ambao ni vaccinated ndiyo wanaolazwa vivyo hivyo 99% ya wanaokufa ni wale ambao ni unvaccinated na only 1% is from those who are vaccinated

USIKURUPUKE kuja hapa kuandika uongo.






Mimi nayewaambia watu kuhusu ukweli wa chanjo wasichanjwe wasichokijua Vs wewe unayewahamasisha watu wachanjwe wasichokijua yaani watu milioni 60 wageuzwe majaribio ya wazungu ni nani hatari kwa usalama wa taifa?
Mimi nayewaambia watu kuhusu ukweli wa chanjo wasichanjwe wasichokijua Vs wewe unayewahamasisha watu wachanjwe wasichokijua yaani watu milioni 60 wageuzwe majaribio ya wazungu ni nani hatari kwa usalama wa taifa?
Mimi nayewaambia watu kuhusu ukweli wa chanjo wasichanjwe wasichokijua Vs wewe unayewahamasisha watu wachanjwe wasichokijua yaani watu milioni 60 wageuzwe majaribio ya wazungu ni nani hatari kwa usalama wa taifa?
 
Gwajima hawezi kubadilika na kuwa mtu mwenye akili timamu tena, ameshakuwa muongo na mpotoshaji kiasi kwamba anauamini uongo wake mwenyewe kama ukweli.
 
Namuunga mkono Gwajima kwa mara ya kwanza, huo utopolo wachanje wenyewe, Alafu viongozi baadhi wanatuchezea danganya toto tu, mtu anaonyeshwa anachomwa live mna uhakika gani hachomwi maji ya dripu??

Sichanjwi, Imeisha hio!!
 
Eleza ubaya wa mRNA, acha kusagia tu bila facts
Mods naomba msiunganishe hii thread naomba ibaki hapa hapa...tuanze sasa...

Nipo nadrive ila nimepaki kwanza pembeni niandike captions kidogo tu

Kwanza kabisa kuna mtu atauliza mbona tulichanjwa toka utotoni sasa kwanini tupinge hii Nikuelemishe kidogo tu
Umechanjwa chanjo utotoni sawa hata mm pia ...hivi unajua kwamba chanjo za covid za pfzer,modena na j&j zimetengenezwa tofauti na chanjo nyingine zitengenezwavyo hizo tatu zimetengenezwa na mrna technology ambayo inaingizwa kwenye cell,vinasaba dna pamoja na genetics ambavyo ni hatari ndo maana watu wanapinga......

Gwajima yupo sahihi kwa asilimia 100%

Gwajima kaongea fact tupu nakubaliana nae kabisa

Chanjo za MRNA kama pfzer,moderna na JJ hazifai ni hatari tupu

Chanjo zote ni emergency authorization na hazijathibitishwa

Zote zinahesabiwa kama majaribio tu na madhara ni juu yako wewe mtumiaji

Chanjo hizi za mrna ni uongo mwingi mnooo na hata uwezo wake wa kuzuia version mpya ya virus ni mdogo unazuia mno ile ya wimbi la mwanzo tu

Wanaokufa wamechoma mrna vaccine ni maelfu huko marekani lakini media za mabeberu hawatangazi japo kwa uchache mnooo

Gwajima kaongea fact kabisa hata hao wanaojimwambafy wamechoma na wamegeuka pro chanjo kama yule wa ndege za tanapa kukodi yule tunamjua anavyoweza kutumika kwa vipande vya fedha.....

Gwajima nakuunga mkono sikatai chanjo ila hizi za mrna hapana aisee bora hata zile za wachina na wacuba ila sio huo utupolo wa mrna vaccines wa kuchoma mkachome ila mjue mrna zinagusa mpaka cell, dna,aka vinasaba na genetics hapo ndo noma

Halaf hawatengenezi kwa njia kama zilivyo za surua,polio etc....wao wanatengeneza kwa liteknolojia la mrna ambalo halijawahi kutengeza chanjo yoyote ile hiyo kitu ni hatari mno nenda hata google mkasome....

Mwishoni big up gwajima........umejitahidi sana broo....umeukataa huu ushetani

Ngoja niendelee na safari....tukutane baadae
 
Tatizo ni gwajima?
Au tatizo ni mtu kutaka kujua chanjo ya Corona imebeba nini?
Je ni vibaya mtu kutaka kujua chanjo imebeba nini?
Mbona chanjo zingine na dawa, vitu vilivyomo viko wazi?
Mambo ya kutishia madaktari kapuyanga, ila hoja ya msingi ni kuwa uchunguzi ufanyike na iwekwe wazi, kuna tatizo hapo?
Hamna majibu, juu ya hoja yake ya msingi,mmeishia kumshambulia tu.
 
GWAJIMA ANAWASIWASI NA CHANJO YA CORONA TUU! LABDA NI KWA UJINGA WAKE AU KAAMUA KUIPINGA SERIKALI KWA UJEURI TUU.

Kwa Mkono wa, Robert Heriel.

Nimeiona Clip inayomuonyesha Ndugu Gwajima akitoa maoni yake Kanisani kwake kuhusu Masuala ya Chanjo ya Corona.

Katika Hotuba yake hiyo, Gwajima alitoa maudhui yaliyolenga kuwashawishi waumini na wasikilizaji wake kuwa wasikubali Chanjo ya Corona mpaka pale Madaktari wa kitanzania watakapo fanya uchunguzi wa contents akimaanisha Gradients au Chemical composition zilizopo kwenye Chanjo hiyo.

Kauli za Gwajima mbali na kushawishi waumini wake na waliokuwa wakimsikiliza, pia zililenga kutishia na kuwaogopesha baadhi ya watendaji katika sekta ya Afya, Kwa kuwataja Madaktari watakaohusika kuipitisha chanjo hiyo.
Gwajima alitoa kauli ambazo Mimi niliziona za kipuuzi na kitoto, kwani Kwa. Uelewa wake alidhani mungu anayemuamini yeye basi ni mungu wa watu wengine.

Gwajima kupitia kauli yake ya kutisha Madaktari namlimgamisha na Wale masheikhe waliomtishia Afande Sele wakidhani mungu wao ananguvu ya kufanya atakavyo Kwa watu wote Kama afanyavyo kwao. Jambo ambalo ni uongo.

Nikiachana na mambo ya Imani ili nisiguse makundi ya waaminio. Naomba nirejee kwenye hoja.

Gwajima anaongea Kama mtu asiyemtaalamu, anayebebwa na upepo wa propaganda za kitoto na watu wasioenda shule.
Na Kama kaenda shule basi elimu yake itakuwa na Shaka kubwa Sana, sio ajabu Mbunge Msukuma akiwakejeli wasomi ikiwa ndio akili zao zipo Kama hivi.

Gwajima lazima aelewe kuwa ishu ya Corona ipo kitabibu zaidi kuliko porojo zake au Siasa ambazo ni kuongea tuu.

Kuwaambia Madaktari ati wachunguze contents zilizopo ndani ya Chanjo ya Corona ni kujaribu Kueleza kuwa Madaktari WA nchi hii hawajui wajibu na kazi Yao.

Gwajima anataka kuwaambia Waumini na wasikilizaji wake kuwa, Madaktari wa Tanzania huwaga hawafanyagi uchunguzi katika madawa yanayotoka nje.

Gwajima anafikiri kuwa Madaktari WA Tanzania wanaongozwa na Teolojia inayomuongoza yeye ambayo ni Tawi la Falsafa ambayo Wachungaji huitumia kuwafundisha watu habari za Mungu, Jambo ambalo sio kweli. Madaktari huongozwa na Sayansi zaidi kuliko masuala dhahania.

Gwajima anajifanya anaakili mbele ya waumini na wasikilizaji wake na hawapi nafasi ya kufikiri kuliko upeo ili aonekane kaongea hoja yenye manufaa wakati Kwa akili ndogo ni kuwa ameongea pasipo kufikiri vizuri.

Kama Gwajima angetoa nafasi ya kuulizwa maswali huenda angejidharau pale pale na kujiona ameongea vitu visivyopaswa kuzungumzwa na mtu Kama yeye.
Mfano wa maswali;

1. Tangu nchi imepata Uhuru, ni lini Madaktari walitaja contents zilizopo kwenye madawa yatokayo nje au hata Chanjo ambazo tulichanjwa?

2. Kwa nini Gwajima Hana wasiwasi na Dawa zingine Kama vile ARVs, chanjo wapigwazo watoto wachanga, au wamama wajawazito, Kwa nini iwe Chanjo ya Korona na sio hizo?

3. Gwajima amegusia suala la biashara imejiingiza kwenye suala la Chanjo ya Corona, yupo sahihi. Ni Ugonjwa upo ambao sio biashara?
Na ni Huduma gani isiyobiashara Kwa sasa? Mbona hata kwenye dini biashara imejiingiza, yeye anaona Kwa wenzake haoni upande wake.

Gwajima alikuwa anaelezea Jambo ambalo Hana Uelewa nalo Kwa sababu yeye sio Daktari, hivyo kujifanya anaamrisha mambo asiyo na Uelewa nayo ni Kama kujivua nguo mbele za watu.

Gwajima sijui hajui au anafanya ukaidi, mambo mengi tunayoyatumia iwe Kwa kula au kutumia kawaida yanatoka nchi za nje, Kwa hao hao Wazungu. Hivyo Kama ni kutumaliza wangetumaliza hata kabla Gwajima mwenyewe hajazaliwa.

Gwajima anaweza akawa na hoja lakini uwasilishaji wake umekuwa wakijinga Kwa sababu maoni yake anajaribu kuyalazimisha na kutisha watu, huku akielezea mambo asiyo na utaalamu nayo.

Mahali ninapoungana na Gwajima;
Ninaungana na Gwajima ile siku alipompinga Mbowe kuhusu kauli yake kuwa Chanjo iwe Lazima,
Gwajima anajaribu kuifichua tabia ya Mbowe ya udikteta ya kulazimisha Chanjo ya Corona Kwa wote badala ya kutumia Demokrasia.

Hata hivyo Gwajima naye anajisahau, anataka kulazimisha watu wakatae Chanjo ya Corona badala ya kuruhusu demokrasia Kama Tamko la serikali lilivyoelekeza kuwa; Chanjo ya Corona ni Hiyari.
Anayetaka akapigwe, asiyetaka aache.

Gwajima usiwaze Kama mtu asiye na Uelewa wa mambo.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
MOROGORO
Hivi mtu kama huyu kuna haja ya kumjadili?
 
Habari!

Hili jambo nililisikia 2020 toka kwa waumini 2 wa Gwajima.

Mimi niko karibu na waumini kadhaa wa Askofu Gwajima ambapo kati yao 2 ninafanya nao kazi ofisi moja, idara moja. Na hao wote ni wachungaji wa kikundi (Ministry pastors) wa kanisa la Ufufuo na Uzima.

Aliamini huenda angerithi mikoba ya Magufuli 2025 lakini Magufuli ametangulia mbele za haki.

Je, atasubiri mpaka 2030 pindi atakapomaliza Rais Samia Suluhu?
Hapana.

Hataweza kusubiri 2030 bali atajaribu karata yake ya bahati 2025.

Msitegemee 100% kuwa Gwajima atamuunga mkono Rais Samia Suluhu kwa sasa.

Gwajima mtu mwenye akili nyingi anaweza kuipiga ngome ya mama na ikapigika. Ngoja tusubiri.

Hii ni tetesi hivyo naomba msiufute huu uzi, hauna dhamira ya uchochezi.
Umekosea hapo ulipoandika kwamba ana akili nyingi. Labda akili za kitapeli.
 
Tatizo ni gwajima?
Au tatizo ni mtu kutaka kujua chanjo ya Corona imebeba nini?
Je ni vibaya mtu kutaka kujua chanjo imebeba nini?
Mbona chanjo zingine na dawa, vitu vilivyomo viko wazi?
Mambo ya kutishia madaktari kapuyanga, ila hoja ya msingi ni kuwa uchunguzi ufanyike na iwekwe wazi, kuna tatizo hapo?
Hamna majibu, juu ya hoja yake ya msingi,mmeishia kumshambulia tu.

Mkuu, umesoma ukaelewa nilichoandika?

Mbona nimeshaeleza kuwa, Huyo Gwajima Kwa nini asiwe na wasiwasi kwenye madawa mengine au Chanjo zingine isipokuwa Chanjo ya Corona yeye ndio kaiona?

Nani alimuambia Dawa zinazoletwa TANZANIA hazifanyiwi uchunguzi mbali na hiyo Chanjo ya Corona??

Au kihere here cha mdomo wake?

Yeye ni vitu vingapi anavitumia yakiwemo madawa yanathibitishwa na Wataalamu wa kitanzania pasipo kelele wala Matangazo?
 
Tangu Gwajima alivyojiapiza kuwa atamfufua Amina chifupa na akashindwa kumfufua basi nikajua huyu ni tapeli tu.
 
Habari!

Hili jambo nililisikia 2020 toka kwa waumini 2 wa Gwajima.

Mimi niko karibu na waumini kadhaa wa Askofu Gwajima ambapo kati yao 2 ninafanya nao kazi ofisi moja, idara moja. Na hao wote ni wachungaji wa kikundi (Ministry pastors) wa kanisa la Ufufuo na Uzima.

Aliamini huenda angerithi mikoba ya Magufuli 2025 lakini Magufuli ametangulia mbele za haki.

Je, atasubiri mpaka 2030 pindi atakapomaliza Rais Samia Suluhu?
Hapana.

Hataweza kusubiri 2030 bali atajaribu karata yake ya bahati 2025.

Msitegemee 100% kuwa Gwajima atamuunga mkono Rais Samia Suluhu kwa sasa.

Gwajima mtu mwenye akili nyingi anaweza kuipiga ngome ya mama na ikapigika. Ngoja tusubiri.

Hii ni tetesi hivyo naomba msiufute huu uzi, hauna dhamira ya uchochezi.

Huu Uzi ufutwe Maxence Melo Boqin Innovator Panel Moderator Paw
 
Ubunge tu hakushinda na aliiba kura, huyu ndiye tumuote eti Askofu? Hapana ! Askofu ni lazima awe MTU wa haki, MTU anayeichukia dhuluma, mtu anayeishi ndani ya ukweli, huyu hawezi kuwa askofu.
 
Ulichoandika hapa ni UONGO MTUPU! 99% ya wanaokufa ni wale ambao hawajapata chanjo ná 97% ya wanaolazwa ni wale ambao pia hawajapata chanjo.

Wanaokufa wamechoma mrna vaccine ni maelfu huko marekani lakini media za mabeberu hawatangazi japo kwa uchache mnooo
Bc ww uchanjee ili tuone km unajiamini au unabwabwaja trh 28 zoezi linaanza
 
Back
Top Bottom