#COVID19 Askofu Gwajima: Ni jambo baya sana kuwapa Chanjo ya Corona Wanajeshi, Polisi na watu wa Usalama

Mtumishi wa Bwana

Nataka ujuwe sipingani na wewe wala sipo kinyume na wewe, nataka nieleze mawazo yangu kuhusu somo lako la leo kuhusu kuchanjwa.

Leo umehubiri kuhusu chanjo kwamba waumini wako wasikubali kuchanjwa, napenda nikufungue macho kidogo uweze kuona,


Nilipozaliwa nikiwa mtoto mchanga kutoka tumboni mwa mama yangu nilichanjwa chanjo tano siku ile ile nazaliwa,na kwa taarifa yako hao wazungu unaowapinga kwa nguvu zote wangependa kuniangamiza wangenimalizia kwenye zile chanjo tano nilizopokea wakati nazaliwa.

Napenda nikusaidie upate kuelewa,dunia hii tunayoishi inaongozwa na watu wachache sana wala hawafiki kumi


Napenda nikufahamishe kabla corona haijaingia kuna watu walikuwa na taarifa,nimekueleza hilo ili ujue nini kinaendelea duniani
chanjo ya corona inatoka kwa wazungu na wao wameonyesha mfano kuanza kuchanjwa wao.

Nataka ujue kama wazungu wana nia mbaya na sisi wangeweza kutumia njia yoyote ile kutumaliza,

Kwa taarifa tupo mikononi mwao na sisi kama waafrica hatuna chance ya kusimama mbele yao kwa kuwa hatuna jambo lolote tulilofanya katika kuchangia maendeleao ya dunia tangu tunajitawala mpaka muda huu

Mtumishi naomba ujuwe kuna dunia,mwili na roho,haya ni mambo matatu yanayotofautiana sana na sijakusikia ukigusia,huu mwili ukipata chanjo hauwezi kuathiri roho kwa sababu kila kitu kinajitegema,kumbuka ukifa roho inatoka ndani ya mwili na huo mwili unabaki kurudishwa mavumbini

Shirika la Afya Duniani linasimami chanjo dunia nzima unaingilia kati na kuanza kuwanyima washarika wako wasichanjwe naona kuna hatari inakujia hapo mbele

Corona inabadilika kila siku vipi kikija kirusi ambacho waliochanjwa wanapona na ambao wamechanjwa wanakufa??
Utaficha wapi uso wako Mtumishi wa Bwana

Nikiwa kama mkristo aliyeokoka nakushauri ubiri ujumbe wa aina nyingine kwa sababu haya mambo ni magumu kidogo,kumbuka ni watumishi wangapi wa Mungu wamekufa kwa corona?

 
Leo nimemsikia Gwajima akisema hataruhusu vyombo vya ulinzi, madaktari, manesi na viongozi wa dini wachanjwe! Nimepatwa na mshangao mkubwa na mshituko nikajiuliza mtu huyu katoa wapi ujasiri wa kuamuru au kutoa ushsuri kwa vyombo vyetu vya ulinzi nini wafanye na nini wasifanye! Hajui kama jeshini kuna chain of command? Au siku hizi kapewa cheo cha msemaji wa jeshi letu na madaktari wetu?

Gwajima kasahau kwamba nchi hii ina Amiri jeshi mkuu ambaye pia ni Rais wa nchi ambaye aliunda jopo la wataalam wakaja na mapendekezo ya kitaalam..Yaani Gwajima anataka vyombo vyetu vya ulinzi wapinge amri halali ya Amiri jeshi mkuu!? Kwa lugha nyepesi Gwajima anafundisha uasi jeshini?
Hajui kama anachokifanya ni uhaini tena mchana kweupe? Huyu Gwajima hajui adhabu ya uhaini? Kama ana mawazo yake na mapendekezo yake hajui namna ya kuwasilisha mpaka kuanza kuwahimiza wanajeshi wetu wagome !
Huyu Gwajima amejisahau kiasi hiki au ni laana ya kumtukana Pengo? Nitashangaa huyu Gwajima asiposhughulikiwa kwa kuhimiza uasi kwa vyombo vyetu vya ulinzi na madaktari wetu!
Kuchanjwa ni hiari sio lazima
 
sidhani kama unajielewa wewe.ana haki yatoa mano yake juu ya mambo ya usalama wa wananchi wenzake

Soma hapa chini

chanzo uwezo wake ni 65%
haijajaribiwa kwa mtu mweusi kama africa
ina madhara kwa watu fulani fulani
RNA made vaccine

tuna haki ya kuwa na wasiwasi

1. Janssen imefanyiwa majaribio South Africa na ilionyesha mafanikio makubwa kupambana na South African variant link hii hapa👇



2. Pia unaposema kwamba hazikujaribiwa kwa mtu mweusi, wakati tunaambiwa majaribio yafanyike si tuligoma tukasema sisi sio nyani wa kufanyiwa majaribio ? Nchi zenye majority ya watu weusi ambazo zilifanyiwa trials nakumbuka ilikuwa South Africa na Kenya na tuliwadhihaki kuwa wamekubali kutolewa chambo.

3. Janssen vaccine haitumii mRNA technology na ndio maana ni rahisi kuletwa Africa , mRNA inahitaji uhifadhi wa joto la chini sana kitu ambacho ni ngumu kupatikana kwenye hizi nchi zetu
SmartSelect_20210725-175748_Chrome.jpg

SmartSelect_20210725-175808_Chrome.jpg

4. Hizo namba za efficacy kwa vaccines hazina maana inapotumika kulinganisha ubora wa chanjo kwa sababu efficacy figures zinapatikana katika trials, mfano Pfizer inaweza kufanyiwa trials kipindi maambukizi ni madogo nchi tofauti halafu ikaja AstraZeneca ikafanyiwa trials muda maambukizi yako juu na nchi tofauti...mpaka sasa hakuna research iliyofanyika kuangalia ipi ni chanjo bora zaidi. Kinachoangaliwa ni uwezo wa chanjo kumlinda mtu kama atapata maambukizi basi asiumwe ugonjwa mkali utakaopelekea yeye kulazwa ama kufariki , aliyepewa chanjo ana uwezekano mkubwa kuumwa kidogo sana ama kutokuumwa kabisa kama atapata maabukizi ya corona na hivyo kuufanya ugonjwa kutokuwa tishio.

5. Madhara ya chanjo ya Janssen ambayo yaliongelewa sana ni damu kuganda ambapo probability ni 0.000007% ( watu 7 kati ya milioni 1). Uwezekano wa damu kuganda iwapo utapata maambukizi ya CoVID-19 bila chanjo yoyote ni kama umelazwa hospitali ni 0.05%(mtu 1 kati ya 20) na kama upo nyumbani na ugonjwa wa usio mkali ni 0.01% (mtu 1 kati ya 100).

Tatizo taarifa zinaweza kubadilishwa kuweka hofu tu juu ya chanjo bila kuangalia hizo hizo risks zilizopo kama ukiachwa ukaambukizwa hiyo COVID-19.

Watu wamekunywa bupiji,nimricaf, covidol bila kujua humo ndani kuna nini, majaribio yamefanyikia wapi na side effects ni nini, wengine mpaka wamesababisha figo kufeli kwa kuchanganya mitishamba lakini hakuna aliyekuwa na wasi wasi nazo...jiulize hizo nyungu zina efficacy kiasi gani?
 
Huwa wanajeshi wanatumika wachache tu Kwa ajili ya majaribio na sio wote.

Sasa mamlaka waangalie namna wanafanya ,

Isiwe wote ila Wachache tu Kwa ajili ya kuangalia uelekeo wakee.
Serikali imeshasema ni salama hivyo hayo majaribio hayahitajiki tena maana yameshafanyika.
 
Serikali imeshasema ni salama hivyo hayo majaribio hayahitajiki tena maana yameshafanyika.
Chanjo hizi zote unazoziona ni za majaribio

Halisi bado

Ndio maana hata wakielezea uwezo wake wanakupa Kwa asilimia.

Hizi zimekuja tu Kwa ajili ya kupunguza madhara ya ugonjwa.

Anyways kila mtu atumia akili yake ambayo Mungu kamjalia.
 
Ni wazo baya sana kuwachanja chanjo ya Corona askari wa majeshi yetu kwa sababu hatujui usalama wa hizo chanjo.

Baba Gwajima amesema anapinga kwa 100% vyombo vya dola kuchanjwa kwa sababu tunaweza kupoteza taifa. Askofu Gwajima amesema haya Kanisani kwake leo.

Askofu Gwajima amewataka wafuasi wake na wapiga kura wa jimbo la Kawe wakatae kabisa kuchanja kwa sababu watapata hasara kubwa sana maishani.

" Naikataa kabisa chanjo ya Corona " amesisitiza baba askofu.

Chanzo: Mtandao wa You tube!
kama hawatachanjwa wasije kutukamata sisi wananchi watatuambukiza
 
IGP amuite na kumuonya aache unafiki....yeye mbunge hapaswi kuwa hivyo kwa hilo mengine yote mbona hatumuoni atuache ni hiari yetu yeye kama nani ? Wanamlea wàmfunge mdomo
 
Ni wazo baya sana kuwachanja chanjo ya Corona askari wa majeshi yetu kwa sababu hatujui usalama wa hizo chanjo.

Baba Gwajima amesema anapinga kwa 100% vyombo vya dola kuchanjwa kwa sababu tunaweza kupoteza taifa. Askofu Gwajima amesema haya Kanisani kwake leo.

Askofu Gwajima amewataka wafuasi wake na wapiga kura wa jimbo la Kawe wakatae kabisa kuchanja kwa sababu watapata hasara kubwa sana maishani.

" Naikataa kabisa chanjo ya Corona " amesisitiza baba askofu.

Chanzo: Mtandao wa You tube!
Viongozi wenu wanatakiwa waoneshe mfano, aanze kuchanjwa Rais kwanza na hadi huko kwa UVCCM wote.
 
Chanjo hizi zote unazoziona ni za majaribio

Halisi bado

Ndio maana hata wakielezea uwezo wake wanakupa Kwa asilimia.

Hizi zimekuja tu Kwa ajili ya kupunguza madhara ya ugonjwa.

Anyways kila mtu atumia akili yake ambayo Mungu kamjalia.

..nadhani huko tunakoelekea chanjo nyingi zitatengenezwa kwa kutumia njia zilizotumika kutengeneza chanjo za covid-19.
 
Back
Top Bottom