Uchaguzi 2020 Askofu Gwajima: Naweza kufanya kazi yoyote ambayo haijakatazwa kibiblia, Mungu alijitambulisha kwa majina tofauti!

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,887
141,819
Askofu Gwajima amesema Mungu anayemtumikia alijitambulisha kwa majina tofauti tofauti kulingana na nyakati na jukumu husika.

Alijiita Jehova, Niko ambaye Niko, Mungu Mwenyezi, Bwana wa Majeshi nk.

Hivyo mtumishi wa Mungu unaweza kufanya kazi yoyote ilimradi tu kazi hiyo siyo katazo la kibiblia.

Askofu Gwajima ametangaza nia ya Kugombea Ubunge katika jimbo la Kawe Wilayani Kinondoni.

Maendeleo hayana Vyama!
 
Aache utapeli, naona sasa anapeleka siasa kanisani na waumini wake watakuwa wanamshangilia kama kawaida yao.

Mbona wale wakina Petro, Paulo, Mathayo, Luka na wengine wao hawakujigeuza Wanasiasa?

Utawala wa Mungu wa kweli sio wa dunia hii, utawala wake ni wa mbinguni, hii dunia inamtawala wake mwingine tofauti, ndio maana Yesu alipowachukua wale wanafunzi wake aliwaambia wayaache yote ya ulimwengu wamfuate yeye.
 
Aaache unafiki, anajifanya kusafisha kauli aloisema mwanzoni kua yy ni zaidi ya mbunge.....ila anyway Kwani mbona alikata mauno juu ya kondoo wakati Biblia imekataza Uzinzi?? Gwaji miunoo akae kando, Siasa awaachie magabachori
 
Mnafiki mkubwa

Biblia inasema huwezi kutumikia Mabwana wawili

Either utamdharau huyu umfate yule.

Huyu ni mpumbavu na mjinga anaeamini Watanzania wote mazuzu na yeye anauelewa zaidi yetu wote.

Mungu ampe laana na stahiki kwa kadri ya utapeli, uwongo, unafiki na uchonganishi.

Anainajisi Meza ya Mungu aliehai na kufitinisha watanzania kwa kisingizio cha kumtumikia Mungu ilihali gwajima amejazwa ushetani ndani yake.
 
Aache utapeli, naona sasa anapeleka siasa kanisani na waumini wake watakuwa wanamshangilia kama kawaida yao.

Mbona wale wakina Petro, Paulo, Mathayo, Luka na wengine wao hawakujigeuza ...
Ni sawa ana wajibu wake kiroho huko kanisani kwake lakini yeye ni mtanzania ana haki sawa na watanzania wengine.

Tunaweza kuhoji dhamira na integrity yake lakini hatuwezi kuhoji haki yake ya msingi ya kiraia. Marehemu Rwakatare na Mchungaji Msigwa wote walikuwa wabunge hatukuwahi kuhoji haki zao.

Watanzania tusome zaidi siasa hata kama hatutaki kuwa wanasiasa ili tunapojadili tujadili mambo kwa kufuata misingi badala ushabiki.
 
Back
Top Bottom