#COVID19 Askofu Gwajima: Nasubiri wataalamu wa ndani wa chanjo ya COVID-19 waongee kisha nitawapiga kwa risasi moja tu watawanyike

Gwajima anasema viongozi na wataalamu wetu ni vigeugeu na hawafai kuongoza, Wanafanya mambo kwa kuangalia upepo na sio utaalamu

Anasisitiza wajiuzulu mapema kwenye suala la covid-19

Akihutubia maelfu ya waumini wake leo Gwajima amesema wataalamu wetu ndio hao walijenga pale Muhimbili jiko la kujifukiza nyungu na waliwaaminisha wananchi kuwa chanjo hazifai

Gwajima anasema Leo ghafla wataalamu hao wanahubiri chanjo, Je wanamdanganya nani?

Gwajima anahoji lile jiko sasa wanaalitumia kwa kazi gani pale Muhimbili kwani waliokataa chanjo ndio hao vinara wa kusisitiza chanjo

Gwajima anasisitiza hao wataalamu wa ndani walete Papers au Research zao wamefanya lini na wapi kuhusu chanjo za korona.

Gwajima anasema waje wataalamu hao wa ndani waeleze Madhara ya muda mrefu na mfupi wa chanjo ndio hapo atakuja na Maswali magumu ya kufanya watawanyike

Anasema viongozi makini wangejiuzulu kazi hawafai kuongoza Taifa kwa kuwa vigeugeu kwa kuangalia nani anaongoza juu yao

Enzi za Magufuli hakukuwa na Covid-19; kulikuwa na “changamoto” iliyokuwa ikimalizwa kwa maombi, nyungu, na juisi mchanganyiko wa tangawizi, malimao, pili pili kichaa, n.k.

Covid-19 imefahamika awamu ya 6 na kuagiziwa chanjo. Halafu watu ni wale wale minus JPM!

Gwajima anajifanya kama vile hajui kuwa yuko kwenye chama cha wasanii kinachoendeshwa kwa propaganda. Anajifanya hajui kuwa wenzake walikuwa wanafanya usanii ili kwenda sawa na Magufuli. Kupotea kwa ile connection aliyokuwa nayo Ikulu kumemchanganya hasa!
 
Hakuna cream hapo weweee! Unajidanganya tuu.

Cream bongo!!!?? THUBUTU

Bongo kumejaa makasuku tupu! Mzungu akisema vaa barakoa na wao wanakimbia kwenda kujitwika mibarakoa usoni bila hata kuuliza!

Ujinga mtupu, hebu niondokee mimi na mabarakoa yako usije kunitapisha bure masotojo nilokula usiku huu!
Hahahaaa

here comes the clown 🤡
 
Gwajima anaitafuta nafasi ya urais wa jmt hivyo anapiga jaramba baada ya kuona ombwe lililopo! Ni kweli ana watu wengi Sana nyuma yake ambao ni wale wasiojitambua ( illiterate) na ukabila kwani yeye ni kiongozi wa wale wa Kanda pendwa kule fb! Mkijashtuka yupo magogoni au chamwino!
Hutaki sasa, Wasukuma tuko wangapi kwenye hii Jamhuri?

Yani buda ukiweka Mgombea Msukuma na mwingine wa kabila lolote i assure you Msukuma is gonna win
 
Nadhani Askofu Gwajima anajisahaulisha jambo muhimu sana. Nchi yeti haina "taasisi" IMARA zinazojitegemea kutoa maamuzi bila ushawishi au matakwa ya wanasiasa/Viongozi wakuu. Ndio maana sishangai kuona kuna watu wanadai Katiba Mpya.

Anataka Wataalamu wa Afya wajiuzulu kwa kuwa wameshindwa kuwa na msimamo. Lakini anajisahaulisha kuwa hii dhana ya kuwajibika kwa hapa kwetu HAIPO. Akitaka tufike hapo, inabidi tuanze na kiongozi wakuu wa kisiasa, Ni wazi kuwa baadhi yao maamuzi/matamko yao yamegharimu maisha ya watu kwenye suala hili hili la UVIKO-19.

Ila Ukweli ni kwamba UVIKO-19 sio kitu cha mzaha, kamą umepata kutoa huduma kwa wagonjwa hawa utanielewa vizuri. Kama unadhani Nyugu inakusaidia itumie, kama maombi ni kinga kwako, Funga na kuomba. Lakini kama kuna watu wanaamini kupata chanjo kutawasaidia, waachwe wafanye maamuzi yao. Kila mtu yuko huru kufanya anachoona kina msaaidia.
 
Anapointi ila kwa watanzania hawa kila wakati ni waongowaongo.Anagalia hata kazi za ikulu zimeeudi Dar kalibia mwezi na matokeo yake hera nyingi zinatumika kulioana posho
IKULU KWENDA DODOMA NI .................WEND.....STRAGETICALLY
 
Hutaki sasa, Wasukuma tuko wangapi kwenye hii Jamhuri?

Yani buda ukiweka Mgombea Msukuma na mwingine wa kabila lolote i assure you Msukuma is gonna win
Mwalimu alishaonya juu ya suala hili rais atatoka miongoni mwa makabila madogo kabisa jk alilipindisha hili na madhara yameonekana kukiuka maneno ya mwalimu
 
Mimi siyo shabiki wa drama za Gwajima na pia nafikiri nina uelewa basic wa jinsi chanjo za corona (na chanjo kwa ujumla) zinavyofanya kazi kiasi kwamba sometimes namwonaga Gwajima kuwa kama comedy anapomwaga "elimu" zake kuhusu corona. Lakini kwa hili la chanjo za corona zilizoletwa bongo ana hoja, na hoja zake zisipuuzwe.

Hoja ya msingi kabisa ni hoja inayonigusa mimi binafsi kabisa kwenye familia yangu. Nilimpoteza mdogo wangu mwaka juzi akiwa na miaka 22. Lakini tatizo lake lililopelekea kifo chake lilianza akiwa na miezi mitatu tu mara baada ya kudungwa chanjo. Tokea hapo aliparalyze hadi umauti unamfika, na katika kufuatilia tuligundua kumbe ile chanjo aliyodungwa ilikuwa ipo katika majaribio na watoto wengi walikufa au kuparalyze mara baada ya chanjo miaka hiyo. Kimya kimya ile chanjo waliithdraw lakini iliacha madhara yasiyofutika kwa baadhi ya familia ikiwemo ya kwangu.

Sasa hii chanjo ya corona, iliyopatikana under emergency authorisation, hatujui madhara yake yatakuwaje au la!
Sasa Unataka majaribio wafanyie wapi?
 
Hakuna cream hapo weweee! Unajidanganya tuu.

Cream bongo!!!?? THUBUTU

Bongo kumejaa makasuku tupu! Mzungu akisema vaa barakoa na wao wanakimbia kwenda kujitwika mibarakoa usoni bila hata kuuliza!

Ujinga mtupu, hebu niondokee mimi na mabarakoa yako usije kunitapisha bure masotojo nilokula usiku huu!
Habari yako Kasuku
 
Kitendo cha gwajima kusema viongozi ni vigeugeu na kuwataka wajiuzulu ni mwendelezo wa dhihaka na kebehi kwa kiti cha urais na mwenyekiti wake wa chama. Huyu mtu adhibitiwe mapema kabla hajaaribu zaidi
Wewe unaona amefanya dhihaka gani sasa.au unamaanisha na samia alikuwa kigeugeu?.
 
Sasa "mheshimiwa" Gwajima, unataka kutuambia wewe sio kigeugeu kuliko hao viongozi unaowatuhumu?

Umesahau kwamba ilipotangazwa kwamba corona imeingia duniani, wewe uliuambia ulimwengu wote kwamba kwa nguvu za kiroho ulizonazo umefunga corona isiingie Tanzania? Lakini ulivyo KIGEUGEU (KIWANGO CHA RELI YA STANDARD GAUGE), wewe huyo huyo ndio ulitengeneza video kufundisha watu namna ya kunawa mikono ili wajikinge na corona ambayo wewe ulishasema umeifunga haitakuja Tanzania kamwe ??

Je, unasahau kwamba ulisema KAMWE hutaki cheo chochote cha kisiasa maana cheo chako cha uaskofu ni kikubwa hata kuliko waziri au rais? Sasa kwa nini ulibugia tena matapishi yako ukakubali kugombea ubunge? Wewe sio kigeugeu kuliko hao viongozi unaowashutumu?

Mbona humtii Yesu ambaye wewe unasema ni Mungu wako na kiongozi wako? Yeye si alisema kwenye Mt 7:3 kwamba TOA KWANZA BORITI LILILO JICHONI MWAKO NDIPO UWEZE KUONA VIBANZI VILIVYO MACHONI MWA VIONGOZI WA NCHI?
Ha ha anazani hata video zake za xes tumesahau mbwa yule doggy kabisa.
 
Gwajima anasema viongozi na wataalamu wetu ni vigeugeu na hawafai kuongoza, Wanafanya mambo kwa kuangalia upepo na sio utaalamu

Anasisitiza wajiuzulu mapema kwenye suala la covid-19

Akihutubia maelfu ya waumini wake leo Gwajima amesema wataalamu wetu ndio hao walijenga pale Muhimbili jiko la kujifukiza nyungu na waliwaaminisha wananchi kuwa chanjo hazifai

Gwajima anasema Leo ghafla wataalamu hao wanahubiri chanjo, Je wanamdanganya nani?

Gwajima anahoji lile jiko sasa wanaalitumia kwa kazi gani pale Muhimbili kwani waliokataa chanjo ndio hao vinara wa kusisitiza chanjo

Gwajima anasisitiza hao wataalamu wa ndani walete Papers au Research zao wamefanya lini na wapi kuhusu chanjo za korona.

Gwajima anasema waje wataalamu hao wa ndani waeleze Madhara ya muda mrefu na mfupi wa chanjo ndio hapo atakuja na Maswali magumu ya kufanya watawanyike

Anasema viongozi makini wangejiuzulu kazi hawafai kuongoza Taifa kwa kuwa vigeugeu kwa kuangalia nani anaongoza juu yao
Gwajima atulie tu.Katika hali ile na utawala ule wa magufuli ni nani alikuwa tayari kutoa kile anachokiamini?Watu wote pamoja na Gwajima tulikuwa tunaangalia upepo unaelekea wapi,ni watu wachache wa mtandaoni na vyama vya upinzani waliojaribu ila wote tulifyataaa.
Kwa muoga huenda kicheko na kwa shujaa huenda kilio na wote tunajua vilio vilitokea upande gani.
Tunapumua kidogo lakini ilikuwa huwezi kuandika hapa mpaka upost bila kufuta mara tatu!!!
 
Back
Top Bottom