#COVID19 Askofu Gwajima: Nasubiri wataalamu wa ndani wa chanjo ya COVID-19 waongee kisha nitawapiga kwa risasi moja tu watawanyike

Gwajima anasema viongozi na wataalamu wetu ni vigeugeu na hawafai kuongoza, Wanafanya mambo kwa kuangalia upepo na sio utaalamu

Anasisitiza wajiuzulu mapema kwenye suala la covid-19

Akihutubia maelfu ya waumini wake leo Gwajima amesema wataalamu wetu ndio hao walijenga pale Muhimbili jiko la kujifukiza nyungu na waliwaaminisha wananchi kuwa chanjo hazifai

Gwajima anasema Leo ghafla wataalamu hao wanahubiri chanjo, Je wanamdanganya nani?

Gwajima anahoji lile jiko sasa wanaalitumia kwa kazi gani pale Muhimbili kwani waliokataa chanjo ndio hao vinara wa kusisitiza chanjo

Gwajima anasisitiza hao wataalamu wa ndani walete Papers au Research zao wamefanya lini na wapi kuhusu chanjo za korona.

Gwajima anasema waje wataalamu hao wa ndani waeleze Madhara ya muda mrefu na mfupi wa chanjo ndio hapo atakuja na Maswali magumu ya kufanya watawanyike

Anasema viongozi makini wangejiuzulu kazi hawafai kuongoza Taifa kwa kuwa vigeugeu kwa kuangalia nani anaongoza juu yao
Nimemsikiliza mwanzo mwisho...

Leo kashusha makombora yasiyo ya kawaida...

Hili limekuja baada ya kumzushia kuwa yeye Mch. Gwajima alikwisha chanjwa chanjo ya COVID 19 tangu mwaka jana huko HONGKONG na CHINA...

Wameweka mpaka "fake certificate" kujaribu kuthibitisha kuchanjwa kwake. Hapo ndiyo wakamchokoza zaidi na ndiyo kulipuka na kusema yote hayo...

Kwa kifupi, Mch. Gwajima yuko kinyume kabisa ña chanjo ya UVIKO 19, yuko kinyume na Rais Samia, yuko kinyume na serikali. Yeye amechagua kupiga kampeni ya LA KUCHANJWA...

Nampenda sana mchungaji huyu. Si kigeugeu, ni muwazi na haumiumi maneno. Husimamia vilivyo kile anachokielewa na kukiamini bila kujali wengine mnasema nini...

Kwa hili kasema waziwazi kuwa, hata akibaki peke yake, basi hatageuka nyuma, kushoto ama kulia...

Kasema kwa upande wa wachungaji wenzake wa kidini, kuwa huu ni wakati wa kutengwa kwa wachungaji wa kweli na wachungaji wa uongo...!

Mchungaji wa kweli ni yule alindaye kondoo wake hata pale simba ajapo kutaka kuwararua, yeye hakimbii (hakani imani yake)...

Mchungaji mwema ni yule aliye tayari kuutoa uhai wake kwa ajili ya kondoo zake...

Yeye kasema, hata kwa kifo cha kimwili au kisiasa (kuvuliwa ubunge au kuamua mwenyewe kuacha), hata kuwa tayari kukubaliana na mikakati miovu ya shetani dhidi ya nchi hii...!

Duuh, huu ni msimamo wa mtu BOLD anayejiamini, mwenye nguvu zisizo za kawaida...
 
Anamsema Dada yake Dorothy......ila kusema ukweli wataalamu wetu wakubali tu waliteleza
Hawajateleza hata kidogo, walilazimishwa na wanasiasa wa ccm wanaotumia katiba dhaifu kunyanyasa wananchi..ni nani angethubuti katamka tofauti na dikteta?
 
Nimemsikiliza mwanzo mwisho...

Leo kashusha makombora yasiyo ya kawaida...

Hili limekuja baada ya kumzushia kuwa yeye Mch. Gwajima alikwisha chanjwa chanjo ya COVID 19 tangu mwaka jana huko HONGKONG na CHINA...

Wameweka mpaka "fake certificate" kujaribu kuthibitisha kuchanjwa kwake. Hapo ndiyo wakamchokoza zaidi na ndiyo kulipuka na kusema yote hayo...

Kwa kifupi, Mch. Gwajima yuko kinyume kabisa ña chanjo ya UVIKO 19, yuko kinyume na Rais Samia, yuko kinyume na serikali. Yeye amechagua kupiga kampeni ya LA KUCHANJWA...

Nampenda sana mchungaji huyu. Si kigeugeu, ni muwazi na haumiumi maneno. Husimamia vilivyo kile anachokielewa na kukiamini bila kujali wengine mnasema nini...

Kwa hili kasema waziwazi kuwa, hata akibaki peke yake, basi hatageuka nyuma, kushoto ama kulia...

Kasema kwa upande wa wachungaji wenzake wa kidini, kuwa huu ni wakati wa kutengwa kwa wachungaji wa kweli na wachungaji wa uongo...!

Mchungaji wa kweli ni yule alindaye kondoo wake hata pale simba ajapo kutaka kuwararua, yeye hakimbii (hakani imani yake)...

Mchungaji mwema ni yule aliye tayari kuutoa uhai wake kwa ajili ya kondoo zake...

Yeye kasema, hata kwa kifo cha kimwili au kisiasa (kuvuliwa ubunge au kuamua mwenyewe kuacha), hata kuwa tayari kukubaliana na mikakati miovu ya shetani dhidi ya nchi hii...!

Duuh, huu ni msimamo wa mtu BOLD anayejiamini, mwenye nguvu zisizo za kawaida...
Msimamo upi huyu mnafki mkubwa, yeye na kundi lake dhalimu wana hasira sababu mama kaachana na yale mambo ya kipuuzi ya mwendazake, hawapingi chanjo bali wanampinga mama..tunawajua.
 
Gwajima anasema viongozi na wataalamu wetu ni vigeugeu na hawafai kuongoza, Wanafanya mambo kwa kuangalia upepo na sio utaalamu

Anasisitiza wajiuzulu mapema kwenye suala la covid-19

Akihutubia maelfu ya waumini wake leo Gwajima amesema wataalamu wetu ndio hao walijenga pale Muhimbili jiko la kujifukiza nyungu na waliwaaminisha wananchi kuwa chanjo hazifai

Gwajima anasema Leo ghafla wataalamu hao wanahubiri chanjo, Je wanamdanganya nani?

Gwajima anahoji lile jiko sasa wanaalitumia kwa kazi gani pale Muhimbili kwani waliokataa chanjo ndio hao vinara wa kusisitiza chanjo

Gwajima anasisitiza hao wataalamu wa ndani walete Papers au Research zao wamefanya lini na wapi kuhusu chanjo za korona.

Gwajima anasema waje wataalamu hao wa ndani waeleze Madhara ya muda mrefu na mfupi wa chanjo ndio hapo atakuja na Maswali magumu ya kufanya watawanyike

Anasema viongozi makini wangejiuzulu kazi hawafai kuongoza Taifa kwa kuwa vigeugeu kwa kuangalia nani anaongoza juu yao
Gwajima hivi anakumbuka ni Mteule wa CCM kweli? Au ndio hana Cha kupoteza? Nafikiri wenye chama wameshaamua internally
 
Dunia hii ina maajabu sana! Hivi hao wanaoitwa wafuasi wake wanawezaje kukaa na kuanza kulisikiliza jitu taahira kama hilo,au ndio mataahira yamekutana?
Unamkumbuka Kibwetere wa huko Uganda? Aliwaponza wafuasi wake na yeye akasepa na hajulikani alipo.
 
na hilo kanisa sijui kama lina watu wanaojielewa

ushawahi kupita Kanisani kwake siku ya jumapili wakati wa ibada yao?

Nilishawahi pita siku moja ,idadi ya watu na haiba ya wengi , na wengine aina ya magari wanayokuja nayo .

Aisee huwezi ukasema waumini wa askofu Rashid hawajielewi kwa kweli wengi wanajielewa tu ila ndio hivyo tena mambo ya imani ni magumu kuya judge
 
Yule siyo mfufua misukule. Ni misunderstanding. Ni wale watu wanaozinduka mortuary ndio wanaokwenda pale kutoa ushuhuda. Yaani,wale watu waliopelekwa mortuary kimakosa.
 
Gwajima hivi anakumbuka ni Mteule wa CCM kweli? Au ndio hana Cha kupoteza? Nafikiri wenye chama wameshaamua internally
Labda hana cha kupoteza,huenda Mwendazake alimuweka kimkakati sasa alipofariki nahisi aliyoyotegemea hayapo
 
Mimi siyo shabiki wa drama za Gwajima na pia nafikiri nina uelewa basic wa jinsi chanjo za corona (na chanjo kwa ujumla) zinavyofanya kazi kiasi kwamba sometimes namwonaga Gwajima kuwa kama comedy anapomwaga "elimu" zake kuhusu corona. Lakini kwa hili la chanjo za corona zilizoletwa bongo ana hoja, na hoja zake zisipuuzwe.

Hoja ya msingi kabisa ni hoja inayonigusa mimi binafsi kabisa kwenye familia yangu. Nilimpoteza mdogo wangu mwaka juzi akiwa na miaka 22. Lakini tatizo lake lililopelekea kifo chake lilianza akiwa na miezi mitatu tu mara baada ya kudungwa chanjo. Tokea hapo aliparalyze hadi umauti unamfika, na katika kufuatilia tuligundua kumbe ile chanjo aliyodungwa ilikuwa ipo katika majaribio na watoto wengi walikufa au kuparalyze mara baada ya chanjo miaka hiyo. Kimya kimya ile chanjo waliithdraw lakini iliacha madhara yasiyofutika kwa baadhi ya familia ikiwemo ya kwangu.

Sasa hii chanjo ya corona, iliyopatikana under emergency authorisation, hatujui madhara yake yatakuwaje au la!
 
Back
Top Bottom