Askofu Gwajima na Jerry Silaa waitwa kwenye Kamati ya Bunge kujieleza kwa kusema uongo na kushusha hadhi ya Bunge

Kwenye siasa hasa hizi "SIHASA" zetu za kibongo bongo .... Unatakiwa kuwa vuguvugu, muongo muongo,manafiki, mchonanishi mlafi na mbinafsi.

Askofu Gwajima aitike wito, aende mbele ya hiyo kamati akatetee hoja zake ... Kimsingi ni nzito, na zimeshiba:.. baadaye ahitimishe kwa kujiuzuru ubunge! .... vinginevyo akiendelea kuwa mbunge atakuwa msanii zaidi.

Namshauri ajikite kwenye kutoa huduma kwenye kanisa lake na kupitia huko hata wasio waumini wa kanisa lake wataupata ujumbe.
 
Hizi kanati za bunge haziwezi kurusha hewani mubashara wananchi wakajionee Jerry na Gwajima wakiwekwa kitimoto?
 
Kosa alilolifanya Gwajima ni kuamua kutumikia Mabwana wawili , Mbaya zaidi anaenda Kwa bwana huyu na masharti na taratibu za Bwana mwingine kitu ambacho hakipo. Akubali amekengeuka ama sivyo ataaibishwa mchana kweupe
Mungu hadhihakiwi
Yeye alishasema hawezi kuwa Mbunge wala Rais Hivyo ni kujishusha hadhi.


What if kama aliamua ku-revise maono yake? Kwani ni kosa?

Yani mnaona ni ishuuuu Eti Kwanini alisema hataki ubunge halafu akautaka badae?!

Mbona siyo ishu?!

NB: “ it is okey for a person to change his/her opinion(s) after learning more about it “

Msikariri mambo, Ulimwengu huu haujasimama wala kukaa unakimbia na kubadilika kila sekunde kutokana na maendeleo ya teknolojia.

Asomae na afahamu!
 
Kosa alilolifanya Gwajima ni kuamua kutumikia Mabwana wawili , Mbaya zaidi anaenda Kwa bwana huyu na masharti na taratibu za Bwana mwingine kitu ambacho hakipo. Akubali amekengeuka ama sivyo ataaibishwa mchana kweupe
Mungu hadhihakiwi
Yeye alishasema hawezi kuwa Mbunge wala Rais Hivyo ni kujishusha hadhi.


Amemdhihaki Mungu kwa namna gani?

Hao mabwana wawili ni gani na gani?

Kwani kina Daniel hawakuwa wanasiasa huku wakiwa Manabii?

Yusuf Je ? N.k.

Nakushauri uongeze kiwango chako cha ufahamu wa mambo maana bado kiko chini!

Yani una ule ulokole wa kizamani ambao hata kujipulizia uturi safi ilikuwa ni anasa na dhambi!

Samahani kwa kunena hayo!
 
What if kama aliamua ku-revise maono yake? Kwani ni kosa?

Yani mnaona ni ishuuuu Eti Kwanini alisema hataki ubunge halafu akautaka badae?!

Mbona siyo ishu?!

NB: “ it is okey for a person to change his/her opinion(s) after learning more about it “

Msikariri mambo, Ulimwengu huu haujasimama wala kukaa unakimbia na kubadilika kila sekunde kutokana na maendeleo ya teknolojia.

Asomae na afahamu!
Usinidanganye. Kinywa kinaumba hicho ulichokikataa siku ukikiendea kitakukataa wewe
Subiria matokeo
 
Usinidanganye. Kinywa kinaumba hicho ulichokikataa siku ukikiendea kitakukataa wewe
Subiria matokeo



Kinywa kuumba inategemea na wala siyo rahisi kama wengi mnavyozani!

Sasa kama kweli kinywa kinaumba nikuulize swali?;

Kwa hiyo mtu yeyote (ok chukulia Mwamini ) akisema

1.”nataka kuwa tajiri” itawezekana kulala kisha akaamka asubuhi akiwa tajiri kweli kirahisi bila kufanya kazi ?

2. Au mwanamke Mzee wa miaka 80 akisema “Nataka kushika mimba nizae” itawezekana kweli kushika mimba sababu ametamka kwa kinywa chake?


Walokole kuna baadhi ya mambo huwa mnanishangaza sana!
 
Kusema ukweli ni kushusha haadhi ya Bunge?

Kuwa na mtazamo tofauti na spika ni kuvunja haadhi ya Bunge?

JPM aliwahi itwa na Bunge kuonywa juu ya kauli zake kuwa chanjo hazifai? maana na yeye alikuwa sehemu ya Bunge.
IMG_20210822_094750.jpg
 
Kwahiyo wewe umejigeuza mtetezi wa wapinga chanjo, na wasumbua wenye hiari ya chanjo sio, wao kukataa chanjo nu hiari yao ila sii kuwazuia wenye hiari au kuwapotosha wengine.
Hakuna anayepotoshwa hapo, kama Gwajiboy anapotosha basi na serikali inapotosha kwa upande wake lakini kiuhalisia kila upande unatoa maelekezo unayoamini ni sahihi.
Serikali few months back ilikuwa ikikataa katakata habari ya vaccinations lakini lahaula hiyo U-turn waliyopiga si ya mchezo kisa tu mtizamo wa rais aliye madarakani unaibali chanjo yaani suala la chanjo ni la kisiasa zaidi na si la kisayansi kwa Tz.
Hiki anachoitiwa Gwajiboy ingekuwa enzi za Jiwe angeitwa kupongezwa kwa kuelemisha vizuri umma wa Wabongo.
 
Jerry kusema wabunge watoe tozo kwenye mishahara yao imekuwa nongwa, khaaa! Na kila baada ya miaka 5 wanafunga mikataba ya ajira zao za ubunge wanapewa marupuru yao yote haijalishi mbunge ataendelea kwa vipindi vingapi? Tena hiyo hiyo serikali inayafanya mambo tofauti kabisa kwa wafanyakazi wake wengine fikiria walimu, makarani, askari kama yule aliye kuwa analalamika hadharani akisema mke wake ni mwalimu ana ahueni kuliko yeye. Ulinganishe watumishi wote hawa na wabunge ambao spika wao anamwita Jerry kwenye kamati kwa kosa la nafsi yake kumsuta na kuwaambia wenzake walipe tozo kutoka kwenye mishahara yao.

Kweli wabunge wetu wasingeona fahari mh Mwigulu akitutangazia kwamba tumekusanya bilioni kadhaa kutoka kwenye tozo ya miashara ya miezi 3 ya wabunge na fedha hizi tayari zimepelekwa kuchimba visima vya maji kadhaa kwenye vituo vya afya/ shule zilizo na changamoto ya huduma hiyo ya maji.
Si kwa wabunge wa Kibongo, ndiyo kwanza wanataka waongezewe mishahara na marupurupu tena wawe wanalipwa kwa US $.
 
Hii kamati ndio ndugu Pasco Mayalla aliwahi kuitwa nadhani, akabadilika sana toka aende huko
Ukiitwa kwenye hiyo kamati, kama ni mwana-CCM, wanachukua akili yako, wanakuacha uende mikono mitupu. Nafikiri unaona jinsi Mayala alivyo leo, na kabla ya kuitwa kwenye hiyo kamati.
 
Back
Top Bottom