#COVID19 Askofu Gwajima, kuwa Daktari (PhD Holder) hakumaanishi unaweza kutibu wanadamu

JUMA JUMA

JF-Expert Member
Jan 5, 2013
666
835
Askofu Gwajima, tuwaache wataalam wetu wa maswala ya Afya wanapoendelea kutoa Maelekezo mbali mbalimbali juu ya kujikinga na janga hili la Corona likiwepo swala la Chanjo.

Ndio maana hata Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan kila anapotamka swala la ugonjwa huu wa Corona anasisitiza tusikilize Maelekezo ya wataalam wetu wa afya maana sio swala la kila mtu kuongea na kutoa Maelekezo kumbuka Rais anauwezo wa kutoa Maelekezo yoyote lakini katika hili swala anawasikiliza wataalamu wa afya.

Sasa wewe Askofu kuyaongea masuala usiokuwa na utaalamu wake sio kitu kizuri pia kumbuka una watu wanaokuamini ukitoa tamko hata kama ni la ovyo hivyo basi tufungwe vinywa vyetu kwa masuala tusiokuwa na utaalam nayo.

20210726_150611.jpg
 
Kuelekea 2025, Gwajima boy, Joseph musukuma, baba wa star tv mwanza, Hamis kigwangala na mwigulu mchemba tunawatarajia sana mtuambie neno.
 
Niambie mtaalam mmoja wa Afya duniani, (achana na hawa wanaopasua vichwa watu badala ya miguu, wanaosema wamefanya utafiti halafu hawauweki wazi.

Wanaosema wamejiridhisha halafu wanawaambia watu wasaini form kabisa kabla ya kuchanjwa ili yatakayowatokea wasije kuilaumu serikali) ambaye anaijua hii chanjo,

Au hata anayeijua corona, nami nitakuonyesha wataalamu wasiopungua 100 waliojaa mashaka ila wanalazimishwa kutekeleza wajibu wao.

Hapa si siasa.
 
Askofu Gwajima hana AIBU.

Labda hakuumbwa na AIBU.

Na sidhani aliyekosa AIBU huwa ana HEKIMA NA BUSARA.

Na sidhani mwenye KUKOSA BUSARA anauchunga ULIMI WAKE.

Askofu Gwajima alituambia kuwa ATAMFUFUA yule dada mbunge......HOLAAA!

Askofu Gwajima alituambia kuwa yeye ni mtu wa MBINGUNI na atafanya maombi ili kuizuia CORONA isiingie nchini.....HOLAAA!!!

Yote hayo bado tu anaaminika?
Yote hayo bado tu ana ufuasi mtiifu?

Khaaa 😲😲😲

Kwani kuwa na ufuasi mwingi ndio kuwa sahihi?!!!

#TujiandaeKuchanjwa
#KingaNiBoraKulikoTiba
#NchiKwanza
#JMTMilele
#SiempreCCM
#KaziIendelee
 
Wewe ndo huelewi kuwa na PhD holder hakumanishi kwamba unajua kila kitu!! Gwajima yupo sahihi na mimi namuunga mkono asilimia 100%
 
Wewe ndo huelewi kuwa na PhD holder hakumanishi kwamba unajua kila kitu!! Gwajima yupo sahihi na mimi namuunga mkono asilimia 100%
 
Wewe ndo huelewi kuwa na PhD holder hakumanishi kwamba unajua kila kitu!! Gwajima yupo sahihi na mimi namuunga mkono asilimia 100%
 
Askofu Gwajima, tuwaache wataalam wetu wa maswala ya Afya wanapoendelea kutoa Maelekezo mbali mbalimbali juu ya kujikinga na janga hili la Corona likiwepo swala la Chanjo.

Ndio maana hata Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan kila anapotamka swala la ugonjwa huu wa Corona anasisitiza tusikilize Maelekezo ya wataalam wetu wa afya maana sio swala la kila mtu kuongea na kutoa Maelekezo kumbuka Rais anauwezo wa kutoa Maelekezo yoyote lakini katika hili swala anawasikiliza wataalamu wa afya.

Sasa wewe Askofu kuyaongea masuala usiokuwa na utaalamu wake sio kitu kizuri pia kumbuka una watu wanaokuamini ukitoa tamko hata kama ni la ovyo hivyo basi tufungwe vinywa vyetu kwa masuala tusiokuwa na utaalam nayo.

View attachment 1869710

Back
Top Bottom