Askofu Gwajima: Kutoka Kanisani hadi CHADEMA na sasa CCM akielekea bungeni ili kazi iendelee!

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
41,747
2,000
Ni jambo la baraka kuona mtumishi wa Mungu askofu Gwajima ameteuliwa kugombea ubunge kutuwakilisha Wananchi wa Kawe.

Dr Gwajima ana weledi mkubwa katika uongozi wa watu kiroho na kimwili na ubobezi wake ameupatia nchini Korea. Ni mtu mwenye malengo makubwa na naweza kumfananisha na Rais wa sasa wa Malawi.

Askofu Gwajima karibu ulete ukombozi Kawe.

Maendeleo hayana vyama!
 

Akilinjema

JF-Expert Member
Aug 9, 2016
5,932
2,000
Halima hata yeye mwenyewe moyoni mwake kama yuko mkweli wa nafsi yake anajua kabisa kuwa ameshachoka kutumikia wananchi wa jimbo la Kawe!

Huo ndiyo ukweli kabisa !

Halima Mdee kuna maswala muhimu kabisa ya msingi yamemshinda Jimboni ikiwemo migogoro ya ardhi Halima hii imemshinda kabisa, Gwajima atafuatilia na kuleta ufumbuzi ili haki itendeke!
 

Lord denning

JF-Expert Member
Jun 3, 2015
6,673
2,000
Ni aibu na fedhea ya kiwango ya juu sana kwa mtu Mwenye siasa za kikabila na kidini Kama Gwajima kuaminiwa na Chama Kama CCM kugombea ubunge katika jimbo nyeti Kama Kawe!!!

Gwajima sio mchungaji, Gwajima sio Askofu, Gwajima ni mfanyabiashara wa dini na tapeli mkubwa wa maisha ya watu!

Sasa naanza kuuelewa wimbo wa Ney wa Mitego Mungu Uko wapi!!!
 

Marytina

JF-Expert Member
Jan 20, 2011
7,225
2,000
johnthebaptist,
ni mtu asiye na huruma hata kidogo akitumia umaskini wa wakristo kujineemesha maisha magumu, ndoa hazipo badala ya kuwaelekeza wakristo wabaki kumtumainia MUNGU aliye hai yeye anawaaminisha wapande mbegu na kutoa sadaka za ukombozi.

Tunao viongozi wengi wa dini ambao hawana ukwasi, yeye amekuwa akilitumia kanisa kama mradi na sasa kwa kuwa waamini wameanza kupungua kwake ameona akimbilie UBUNGE kugharamia maisha yake ya kifahari.

Jamani watu wa dini tuiweke dini mbele tuachane na haya mambo ya wanasiasa.
 

MKANDAHARI

JF-Expert Member
Apr 7, 2011
3,806
2,000
Gwajiporn hajawahi kuwa kiongozi wa kiroho, ila alikuwa ni kiongozi wa dini. Na kama ujuavyo kuna mpaka dini za mashetani.
 

Akilinjema

JF-Expert Member
Aug 9, 2016
5,932
2,000
Halima Mdee hakuwahi kuonekana jimboni kwa Wananchi kipindi chote cha miaka 5 mara baada ya uchaguzi,imagine

Hata kuja kufanya mikutano kuzungumza za wananchi kujua changamoto na shida zao haji hadi wakati wa campaign ya uchaguzi Mkuu kama hivi akishachaguliwa anapotea!

Sasa huyo wa nini?

Aende akateule viti maalum huko kupitia umoja wa kina mama huko Chadema lakini huku basi tena.
 

kantasundwa

JF-Expert Member
May 25, 2020
1,557
2,000
Huku bunju Mdee hajulikani kabisa..... Wengi wanadhani ni Vanessa wa bongo fleva!
Acha uongo bhana John ..Mdee anajulikana mpk huko kasanga sumbawanga sembuse hapo bunju ambapo anafanya mkutano kila leo?? Waulize hapo boda boda bunju mwisho Kama sio uongo n nn
 

Akilinjema

JF-Expert Member
Aug 9, 2016
5,932
2,000
It is very unfortunate that wananchi wa Kawe wanajielewa sana!

Sasa Halima amejisahau sana ama amechoka!

Haiwezekani mbunge uwe unatelekeza wananchi wako kwa muda miaka 5 mfululizo huonekani kutembelea wananchi wako kujua matatizo, changamoto, kero zao na kuwapa mrejesho wa mambo kama upo badala yake unapotea mazima hadi kipindi cha campaign na uchaguzi?!

Safari hii hapana!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom