johnthebaptist
JF-Expert Member
- May 27, 2014
- 94,035
- 164,307
Imeripotiwa na baadhi ya vyombo vya habari kwamba Askofu Gwajima yuko ktk mchakato wa kuingiza nchini treni ya umeme yenye thamani ya zaidi ya sh bilioni 11.
Binafsi nachukulia wazo la Gwajima kama kielelezo cha kutimiza kwa matendo kauli mbiu ya Rais Magufuli isemayo "Tanzania kwanza Siasa baadaye" au ile ya Maendeleo hayana chama.
Je, serikali itampa Gwajima hiyo fursa na je baba Askofu atatuletea treni ya "ukweli"? Yetu macho na masikio.
Ahsanteni.
=======
RAHCO WAMJIBU ASKOFU GWAJIMA BAADA YA KUTANGAZA KUNUNUA TRENI BINAFSI
Kampuni Hodi ya Rasilimali za Reli (RAHCO) imesema kuwa Askofu Mkuu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima anaweza kuendesha huduma ya usafiri wa treni nchini Tanzania huku wakiwataka wawekezaji wengine wenye nia kama yake kujitokeza.
Hayo yalisemwa na Msemaji wa RAHCO, Catherine Moshi ambapo alieleza kuwa, kampuni hiyo imebariki uamuzi wa Askofu Gwajima wa kuwekeza kwa kununua treni, lakini wakamshauri, kabla ya kufanya hivyo ahakikishe amepata kibali kutoka Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.
Baraka hizo za RAHCO zimekuja ikiwa ni siku moja tangu Askofu Gwajima alipotangaza kanisani kwake kwamba ana mpango wa kununua treni itakayokuwa inawapeleka waumini kanisani lakini pia itabeba na abiria wa kawaida.
Akiendelea kufafanua jinsi Askofu Gwajima anavyoweza kutumia reli kuendeshea treni yake, Catherine alisema, atatakiwa kutoa taarifa RAHCO ili apewe njia kwa sababu mtumiaji wa reli ni Shirika la Reli Tanzania (TRL) pekee na atatakiwa kuelezea mabehewa atakayotumia ili apangiwe gharama husika.
Aidha, alisema hakuna sheria inayomzuia mtu kuwekeza katika miundombinu ya reli kwani kwenye baadhi ya nchi wanafanya hivyo na husaidia kukuza uchumi na kuimarisha sekta ya usafiri.
Catherine alisema watu wengi hawajawekeza kwenye miundombinu ya reli kwa sababu gharama zake ni kubwa sana.
Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima amekaribishwa kuwa anaweza kuendesha huduma ya usafiri wa treni na kutaka wadau wengine wenye nia kama hiyo wajitokeze.
Katika ibada iliyofanyika juzi, Askofu Gwajima aliwaambia waumini wake kuwa amedhamiria kununua treni ya umeme itakayogharimu Sh11 bilioni, baada ya Rais John Magufuli kuzindua mradi wa ujenzi wa reli pana (standard gauge) itakayokuwa na kasi zaidi ya treni ya sasa na uwezo wa kuchukua shehena kubwa.