Uchaguzi 2020 Askofu Gwajima kugombea ubunge Kibiblia atafakari upya kama mtumishi wa Mungu

Watu mnaweweseka tu kuona jamaa ana uhakika wa kumtoa mtu wenu Mdee akipewa ridhaa na chama chake.

Hao wachungaji wengine mbona hatukusikia hizi analysis uchwara?

Mdee out!
 
Habari wakuu!

Jana Askofu Gwajima ametangaza nia ya kugombea ubunge kwa tiketi ya chama tawala na ametoa sababu nyingi tu kwa nn yy ni Askofu na anataka kuingia kwenye siasa! Mm kama mtumishi wa Mungu pia na mchambuzi wa Biblia natoa sababu kwa nini askofu gwajima hatakiwa kuwa kwenye siasa.

1: Neno asikofu kibiblia ndo Kazi njema kuliko kazi nyingine zote, kuwa Askofu maanake ww unaongoza makanisa mengine, na umeitwa na Mungu kwa ajili ya Kazi hiyo, maana nyingine unamwakilisha Mungu hapa duniani, na unalipwa na Mungu.

2: Askofu Gwajima ni kiongozi wa kiroho anayeongoza watu wote wa vyama tofauti sasa anapoingia kwenye siasa ataweza kkuwa na ujasiri wa kukemea mabaya yatakayofanywa na chama chake?? Lakini pia Kanisani kwake ataweza kuhubiri bila kuwa na itikadi ya chama?

3: Kazi kubwa ya Askofu Gwajima ni kuwaleta watu kwa Yesu, he! Hiyo Kazi kaimaliza??? ( Rejea kwenye Biblia mavuno ni mengi watenda Kazi ni wachache) bado maasi yanaongezeka duniani huu ndo muda ambao angeutumia kuihubiri injili kwa kila kijiji na kabila watu waache dhambi, hii Kazi hajaimaliza bado anaenda kwenye majukumu mengine ya kaisaria.

4: Mifano aliyoitoa yote haina mashiko ukilinganisha na wito wake, kwanza lwakatare bila shaka alikuwa ni mbunge wa vyiti maalum maanake wa kuteuliwa, na madhara yake tuliyaona hana rekodi ya kuhubiri injili mikoani tofauti na Kanisani kwake!, lakini mchungaji Msigwa au mtikila baada ya kuingia tu kwenye siasa wote tunajua lina baki jina tu uchungaji lakini ule wito kamili unaondoka!

6: Huwezi kuwatumikia mabwana wawili ni lazima umchukie mmoja na umpende mmoja.

7:Kugombea ubunge na ww ukiwa mtumishi wa Mungu sio dhambi lakini madhara yake ni makubwa kwenye ulimwengu wa roho.

8: Kama ni swala la kumsaidia Rais hata hapo alipo uwezo huo anao sana sio mpaka uwe mbunge!

9: Kuwa mbunge ni kujiongezea majukumu ambayo sio ya lazima kwako ili hali kondoo bado wanahitaji malisho yako.

10: Gwajima alianza vizr ila kwenye siasa ungewaachia wenyewe ww uwe mshauri tu:

Note: Nia ya mwili ni mauti lakini nia ya Rohoni ni uzima wa milele, Mungu anaangalia mwisho mwema wala sio mwanzo, gwajima ww huwezi kutolea mfano wa papa wa Italia! Huko ni kuwafurahisha wanadamu ili hali ukweli unaujua tofauti ya makanisa ya kidini na makanisa ya kiroho! Labda kama unataka kuwa mwanadini sawa!

Ili kuelewa jambo hili unashauriwa kusoma mada hii
=> Uchaguzi 2020 - Askofu Gwajima atangaza nia ya kugombea ubunge jimbo la Kawe
Unasumbuka kumwambia gwajima bible uyo ni mganga wa kienyeji boss
 
Sisi wakaazi wa Kawe, hatuko tayari kuongozwa na mcheza filamu za ngono, muuza madawa, mtu anayemiliki silaha haramu, mtu tapeli anayibia waumini kwa madai kwamba ana uwezo wa kufufua ndugu zao waliokufa
Bro kwanza huyu mtu ni tapeli la kutupwa! maisha yake hadi kujiita nabii ni uatepeli na kufuru mbele ya Mungu.
 
Kwahiyo Msigwa na Lwakatale kwao haikuwa tatizo kuwa wanasiasa ila Gwajima ndo iwe?

Tofautisha Mchungaji na Askofu
Gwajima ni Askofu mkuu kwa ufupi ndiye mmiliki wa kanisa lake sijui linaitwa Ufufuo na uzima hivyo anawajibika kwa kanisa lake moja kwa moja, Tofauti na Mchungaji ambaye yeye anaweza kubaki na daraja la uchungaji laikini akawa anafanya shughuli zingine mf siasa.
Mama Rwakatare R.I.P naye ni kama Gwajima aliwakwa na tamaa akaingia kwenye siasa lakini kiroho hakupaswa kabisaaa Mola amsamehe
 
Ndo nyinyi mnaoingilia wake zenu kinyume na maumbile kisa eti mmeoa...

Mzee kuoa ni 1 na maadili ni kitu kingine.

Tatizo sio kugombea,tatizo ni nani anagombea kwa namna jamii inamchukulia.hamna siasa safi,watumishi wa Mungu wangebaki kuwa washauri tu.

Kama unamfananisha na msigwa,basi tukubali kuchukua hata mifano ya maisha mengine ya msigwa tuifananishe nae.
1- kutolea mifano isiyofaa kwa mtu, kwangu mm naamini huna hoja zaidi ya kujilinda kwa kauli hizo.

Binafsi najisifu na kuwasifu wazazi wangu RIP kwa kutonilea hivyo mwisho namshukuru Mungu kwa kuniongoza kupokea lugha zote na kuzitafakari.

Wapi
Ndo nyinyi mnaoingilia wake zenu kinyume na maumbile kisa eti mmeoa...

Mzee kuoa ni 1 na maadili ni kitu kingine.

Tatizo sio kugombea,tatizo ni nani anagombea kwa namna jamii inamchukulia.hamna siasa safi,watumishi wa Mungu wangebaki kuwa washauri tu.

Kama unamfananisha na msigwa,basi tukubali kuchukua hata mifano ya maisha mengine ya msigwa tuifananishe nae.
Wapi nilipofananisha ugombeaji na mchungaji Msigwa?

Maisha mengine ya sifa za mgombea yanahusikaje kwenye chaguzi.

Box la kura ndiyo hitimisho la mgombea iwe chamani au kituo cha kura!.

Gwajima ni Mwana CCM, ni Mtanzania amejipima na kujiona anafaa.
 
Gwajima huyu huyu aliwawleza wafuasi wake kwamba hawezi kugombea Ubunge au Uraisi na pia asingependa kuwa Waziri kwani huko ni kujishusha cheo. Yeye ataendelea kuwa Mtumishi wa Mungu daima dawamu. Alishambuliwa kwa makofi na vigeregere kwa sana. Leo hii anasikika akitaka kugombea Ubunge. Hapo ndipo utagundua huyu jamaa alivyo kama kinyonga, rangi yake haieleweki na hubadirika kufuatana na mazingira. Alianza kwa kufufua misukule na hivyo kuwavuta wale wanaoamini ushirikina. Kaona amepata wafuasi wengi sasa kakimbilia siasa. Lakini akumbuke kuwa huwezi kuwatumia mabwana wawili, Mungu na mali. Achague moja kati ya hivi viwili.
 
Gwajima ni mfanyabiashara kama walivyo wafanyabiashara wengine hivyo anayohaki Kugombea Ubunge.
Sawa kabisa. Haki ya kugombea Ubunge anayo. Lakini anataka kula matapishi yake mwenyewe. Mbele za Mungu na mbele ya kanisa lake na wafuasi wake alijiapiza kwamba hawezi kugombea Ubunge kwani kwa kufanya hivyo atakuwa amejishusha cheo. Alisema ataendelea kuwa Mtumishi wa Mungu daima dawamu.
 
Hao Watumishi ndio wanatakiwa Kwa sababu Taifa litakuwa na maadili
Yaani ccm ni watu wa kuhurumia tu, linatoka jamaa huko lilipo hata halina uchungu, wala ufahamu wa chama, linaingia lina kula maisha, wale magamba kindakindaki wanabaki kama walivyo na wanashangilia tu, daaa praise team bwana mna mioyo ya kipekeee!! Na mwaka huu ndio bala, wewe kwakuwa meko anakukubali hata kama umeingia kwwnye chama juzi, unateuliwa kugombea na sio kura za maoni tena ndio zinazo amua!!!
 
Sisi wakaazi wa Kawe, hatuko tayari kuongozwa na mcheza filamu za ngono, muuza madawa, mtu anayemiliki silaha haramu, mtu tapeli anayibia waumini kwa madai kwamba ana uwezo wa kufufua ndugu zao waliokufa
Ni filamu ipi ya ngono alicheza?
 
Tumuombe Mungu
59a85697b61b4984a8329f758c3f8098.jpg
 
Endapo hao wateja wake hawatatambua kipindi hiki kuwa huyu jamaa ni 'nabii' au tapeli basi ni wa kupelekwa mirembe wakapimwe akili.
 
Dr slaa.,alivyotamani kuowa aliacha upadri kabisa akaambatana na mke wake na siasa
Mim naamini hilo ndilo fungu jema.,Ngwajima aache uaskofu achague siasa.
Mfano wa Papaa kuwa Rais wa roma,ikumbukwe roma ndio makao makuu ya kiroho ya Kanisa Katoliki la Mitume
Zinapofanyika taratibu za kumpata papa si kwa ajili ya kuwa rais wa roma bali ni kwa ajili ya kuliongoza Kanisa Katoliki la Mitume ulimwenguni ila automatical anakuwa the president of roma.
 
Back
Top Bottom