Askofu Gwajima kapandishwa kizimbani leo

cosa nostra

JF-Expert Member
Sep 17, 2010
1,773
1,804
Askofu Mkuu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima na wenzake watatu watapanda tena kizimbani leo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kujitetea katika kesi ya kushindwa kuhifadhi silaha inayowakabili.



Kesi hiyo ambayo upande wa utetezi inawakilishwa na wakili Peter Kibatala na Faraja Mangula ilikuwa isikilizwe jana lakini Hakimu Mfawidhi, Cyprian Mkeha anayesikiliza kesi hiyo hakuwepo, na hivyo ikaahirishwa hadi leo ambapo upande wa ushahidi watakapoendelea kutoa utetezi wao.

Katika kesi hiyo, Askofu Gwajima anakabiliwa na shtaka la kushindwa kuhifadhi silaha na risasi anayomiliki kihalali kwa sababu za kiusalama.

Washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni Geroge Msava ambaye ni msaidizi wa Askofu Gwajima, Yekonai Bihagaze na George Milulu ambao wanakabiliwa na shtaka la kukutwa wanamiliki silaha (bastola aina ya berreta na risasi 20) kinyume na sheria.

Machi 25 wanadaiwa kuwa walikuwa katika Hospitali ya TMJ, Mikocheni A jijini Dar es Salaam wakimiliki silaha hiyo bila kibali kutoka kwa mamlaka inayohusika na silaha na milipuko.


Chanzo: Swahili Times
 
Ukweli utasimama.Maji hayasahau baridi hata yakichemshwa kufikia degree 1000....
 
Kesi ya muda tu huyo enzi za Kamanda Kova.

Hakuna uhusiano wowote na kinachoendelea kwa sasa.

Nakumbuka aliitwa tu kuhojiwa na Polisi Central baada ya kumtolea maneno yasiyo ya kiuungwana Askofu Pengo na alipotoka ndiyo ndiyo hali yake ilibadilika na kupelekwa TMJ kwa matibabu kama alivyopenda yeye mwenyewe.
 
Kesi zisizo na kichwa wala miguu kama hizi ni za kupoteza muda tu.

Bora hata wangepandisha mwizi wa kuku mmoja aliyeko gerezani huko kama mahabusu ambaye anapigwa danadana mpaka leo kuwa kesi yake uchunguzi bado unaendelea.
 
Vyeti na viwanda mwisho chalinze! Mjini tunaangalia usalama wa Bashite tu! Msema kweli ni mpenzi wa "mungu"!
 
Back
Top Bottom