The Palm Tree
JF-Expert Member
- Apr 13, 2013
- 7,951
- 12,535
Kila mtu aliona na kusikiliza namna bunge lilivyomjadili Mch. Gwajima (MB) na mwenzake na kumhukumu kutohudhuria vikao vya mikutano miwili vya bunge...
Kwa waliofuatilia mjadala ule siku ya J'nne tarehe 31/8/2021 bunge likiwajadili hawa wabunge wawili, bila shaka atakubali kuwa lilikuwa ni tukio la kupangwa, lenye hila kwa lengo la kuwadhalilisha na kuwavunjia heshima na utu wao tu ili kuwatisha na kuwaogopesha wasiendeleze ajenda zao hizo huko nje kwa umma...
Tuliona na kusikiliza hoja za upande mmoja yaani za KAMATI YA BUNGE YA KUHOJI WENZAO chini ya M/kiti wake mbunge wa Tabora mjini ndg. Mwakasaka na kisha bunge zima kuzitumia kama "base" ya kuwahukumu wenzao...
Kwa kudhalilishwa kule na kunenewa UONGO, ni ngumu sana mbunge (hata kama ungekuwa wewe usomaye sasa) asiye na hatia, anayejiamini kunyamaza kimya asiseme lolote kwa umma baada ya hapo kwa lengo la kuweka rekodi ya mambo haya sawa...
Bahati mbaya kwa Job Ndugai (Spika wa Bunge) na wabunge wenzake, kuwa, kwa Askofu Gwajima wameshafeli tayari, YOU CAN BELIEVE THAT..!
Leo tarehe 5/9/2021 Bishop Rwv. Dr. Josephat Gwajima wa makanisa ya GCTC - UFUFUO NA UZIMA Tanzania na duniani ametujuza upande wake ambayo tulikuwa hatuyajui...
Ni ajabu kuwa, kuna upotoshaji mwingi unaendelea kupitia mitandao ya kijamii alichokisema Mch. Gwajima leo.
Kuna wengine wanasema alipaswa kunyamaza kimya kwa sababu mambo ya kamati ya bunge ni SIRI ambayo haipaswi kutolewa nje....
Hawa ni wajinga kwa sababu, taarifa ya KAMATI YA KUHOJI ilisomwa hadharani mbele ya kamera za TV zote duniani bungeni na wabunge wote wakaijadili taarifa hiyo kwa uwazi na bunge kuamua lilivyoamua...
Rev. Josephat Gwajima hajafanya kosa lolote kukanusha baadhi ya hoja za uongo za kamati huku baadhi ya wabunge wakizitumia kumdhalilisha na kumtukana kumuonesha kama ni mtu mbaya sana...
Nategemea na Jerry Silaa atatoka na kusema kwa wazi ya upande wake ili umma ujue...