MLAU
JF-Expert Member
- Aug 23, 2007
- 4,726
- 3,358
Tukio la Clouds ambako ndiyo habari ya mjini kwa wiki hii limezua mambo mengi sana,maana kila mmoja anaongea anachojisikia kuongea kiasi kutojua kipi ni kipi haswa.
Kwanza ni tofauti ya taarifa ya matumizi ya silaha kwa askari waliongoza na Mkuu wa Mkoa kwa wafanyakazi wa Clouds.
Askofu Gwajima aliwaambia waumini wake ktk Ibada ya Jpili kuwa baadhi walipigwa mtama,wengine walipigwa na Kitako cha bunduki na mwingine alinyoshewa mtutu wa bunduki.
Wakati Ruge akiongea mubashara na Clouds TV kipindi cha 360 na Redio Clouds ulisema hakuna mfanyakazi yoyote aliyepigwa wala kuumizwa kwa chochote kile na huyu ndiye mkuu wao.
Na hata katika Taarifa ya Tume ya muda ya Nape sijasikia lolote kuhusu kuwa silaha ilitumika au kuna mfanyakazi aliyeumizwa na silaha au askari wakati wa ile visit yao pale Clouds Media
Swali langu:
1.kwanini Askofu Gwajima ana publish mambo ambayo hayakutokea ?
2.Lengo lake ni nini kuhusu vyombo vyetu vya ulinzi na usalama ambavyo vinafanya kazi vizuri na kwa nidhamu ya hali juu sana kama kiapo cha utii?
3.Kwanini Askofu Gwajima ameacha jambo lake la msingi la kuanzisha kanisani ambako ni kuhubiri amani,upendo,kujua MUNGU, kumpenda jirani yako kama nafasi yako,kuwasaidia wasiojiweza,wagonjwa,wajane,yatima n.k.
Na kubwa zaidi kuhakikisha kila mmoja kurithi ufalme wa mbinguni?