Return Of Undertaker
JF-Expert Member
- Jun 12, 2012
- 4,572
- 26,868
Askofu Josephat Gwajima ametangaza nia ya kugombea ubunge Jimbo la Kawe kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) na leo amefika kwenye ofisi za chama hicho kupewa utaratibu.
Kuhusu kuunga mkono UKAWA mwaka 2015, amesema hajawahi kuwa Mwanachama wa CHADEMA, ila hutetea haki wakati wote.
===
Aliingia Ofisi ya CCM Wilaya ya Kinondoni
Amesema alikwenda pale baada ya kumsikia Rais na Katibu mkuu wa CCM aliyetangaza kuwa wale wenye nia ya kumsaidi Rais achukue fomu, na yeye ameona aweze kwenda ofisini kujua utaratibu wa kugombea
Amesema inaweza kuwa mtu mchungaji haimzuii kuwa mbunge kwa kuwa wako viongozi wa dini ambao pia ni viongozi kisiasa, amesema hajawahi kuwa mwananchama wa chadema
Amesema amekuwa mwanachama wa CCM tangu mwaka 1994, aliipata katika mkoa wa Mwanza, Wilaya ya Misungwi, kata ya Buhingo kijiji cha Kabale na alipewa kadi na mzee Kasmiriki Futumo, alikuwa ni mwenyekiti wa ccm ambaye katibu wake alikuwa Leoneidas Masungwa
Kadi yake amesha-upgrade kuingia mfumo mpya, amesisitiza hajawahi kuwa mwanachama wa CHADEMA, ila anapenda kutetea haki na tatatetea haki siku zote. Amesema anatetea haki sehemu yoyote, iwe CCM au kokote pale atatetea haki
Hajasema kitu ambacho anaweza kwenda kuwafanyia watu wa Kawe. Aidha ilionekana kuwa angeweza kugombea Misungwi, lakini amesema Misungwi ni sehemu aliyozaliwa lakini maisha yake yamekuwa Kawe kwa hiyo atagombea Kawe