Askofu Gwajima apigwa kombora Bungeni na Mbunge wa Mtambwe, Khalifa Issa

Ileje

JF-Expert Member
Dec 20, 2011
8,759
12,175
Aitaka serikali kuongea na manabii wanaodai kufufua wafu ili wafufue wapendwa wetu?
===
Mbunge wa Mtambwe (ACT-Wazalendo), Khalifa Mohamed Issa amehoji "Serikali haioni wakati umefika kukaa na manabii wanaodai kufufua waliokufa, ili kuweza kuwafufua wapendwa wetu." N/Waziri Mambo ya Ndani, Khamis Hamza Chilo, amejibu akisema "tutawaelimisha ili tuondoe migogoro."
 
Spika akemee hili!! Nauona mgogoro wa dini ukilinyemelea Bunge la JMT. Upepo wa Mashariki ya Kati unatusogelea tuwe waangalifu sana ndg zangu.

Wakristo wanaamini kuwa kupitia Jina la Yesu wafu wanaweza kufufuliwa na hii ni ahadi ya Mungu wao. Sasa kumshambulia Gwajima ktk imani ni kuwashambulia Wakristo ktk imani kwani amesema kwenye kitabu ni Yesu anafufua na sio yeye binafsi.

NARUDIA TENA SPIKA AKEMEE HILI HARAKA KABLA HALIJATUGAWA KAMA TAIFA. KUMBUKA HOTUBA YA RAIS MAGUFULI KWENYE BARAZA LA IDDI! TUHESHIMIANE KWENYE HIZI DINI!
 
Spika akemee hili!! Nauona mgogoro wa dini ukilinyemelea Bunge la JMT. Upepo wa Mashariki ya Kati unatusogelea tuwe waangalifu sana ndg zangu...

Shambulizi liko wapi hapo, hivi wewe ukisema unashehena ya mahindi na unaweza kutusaidia kuondoa njaa kwenye njaa, mtu akishauri serikali ikae na wewe tununue mahindi yako tupeleke kwenye njaa shida iko wapi?

Itagawaje taifa?
 
Shambulizi liko wapi hapo, hivi wewe ukisema unauza mahindi mtu akishauri serikali ikae na wewe tununue mahindi yako tupeleke kwenye njaa shida iko wapi?
Itagawaje taifa?
Huyu amekoment kulingana na kichwa cha habari,hajasoma content
 
Spika akemee hili!! Nauona mgogoro wa dini ukilinyemelea Bunge la JMT. Upepo wa Mashariki ya Kati unatusogelea tuwe waangalifu sana ndg zangu...
Hiyo Yesu hufufua wafu iko kwenye maandiko na utaondoka dunia imebaki hapo hapo. Ila Uhalisia hutakaa ona Binadam alofariki(ubongo ku stop kufanya kazi) Akafufuka.

Hajataja Jina Gwajima ila kauli kwanini wasikae na hao Manabii ili kurahisisha mambo ya kutufanyia muvi.

Hata Kagame kupiga baadhi ya makanisa na misikiti yuko sawa mana kuna imani zikiendekezwa unazalisha taifa lawajinga
Mana kazi kutupigia makelele mitaani kwa
 
Spika akemee hili!! Nauona mgogoro wa dini ukilinyemelea Bunge la JMT. Upepo wa Mashariki ya Kati unatusogelea tuwe waangalifu sana ndg zangu.

Wakristo wanaamini kuwa kupitia Jina la Yesu wafu wanaweza kufufuliwa na hii ni ahadi ya Mungu wao. Sasa kumshambulia Gwajima ktk imani ni kuwashambulia Wakristo ktk imani kwani amesema kwenye kitabu ni Yesu anafufua na sio yeye binafsi.

NARUDIA TENA SPIKA AKEMEE HILI HARAKA KABLA HALIJATUGAWA KAMA TAIFA. KUMBUKA HOTUBA YA RAIS MAGUFULI KWENYE BARAZA LA IDDI! TUHESHIMIANE KWENYE HIZI DINI!
Sasa si ndiyo aonyeshe miujiza aliyonayo? Udini uko wapi hapo!
 
Huyo mbunge kama kweli kasema hivyo basi ni mpumbavu wa kiwango cha kimataifa.

Anafanyia utani masuala ya kifo wakati hajui ni lini moyo wake utasimama milele.
 
11 Reactions
Reply
Back
Top Bottom