Askofu Gwajima anafaa kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani, Dkt. Kimei Waziri wa Fedha, Tarimba Abbas Waziri Viwanda na Biashara!

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
38,506
2,000
Ni mapendekezo tu kutokana na viwango vyao vya elimu na uzoefu wao katika kutumikia watanzania.

1. Askofu Dr Gwajima........ Waziri wa mambo ya ndani

2. Dr Kimei........Waziri wa Fedha

3. Mh Abbas Tarimba.......Waziri viwanda na biashara

4. Mh Babu Tale........Waziri wa Habari, Sanaa na michezo

5. Mh Mrisho Gambo....... Waziri wa Tamisemi

6. Mh Godwin Kunambi........Waziri wa Katiba na Sheria

Unaweza kuendeleza orodha

Maendeleo hayana vyama!
 

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
40,172
2,000
Katika hawa wote uliowataja na hadi kuwapigia Chapuo hapa japo Mimi Kura yangu JPM na CCM wameipata ila akiwateua wote au hata tu kumteua mmoja wapo hapa nitamdharau kuliko Mwenyekiti wangu CCM na Rais wangu Dk. Magufuli kwakuwa hakuna anayemfaa hapa.
 

Wacha1

JF-Expert Member
Dec 21, 2009
15,720
2,000
Dah wacheni kumchagulia safu yake ya uongozi. JPM ameaminiwa kwa kura za kishindo hivyo yeye mwenyewe anapanga safu yake ya Hapa Kazi Tu.
 

desertfox

JF-Expert Member
Oct 4, 2014
328
250
Kifupi itoshe kusema unaropoka wala hujui uzito wa wizara ya mambo ya ndani pale na mtu km Mwigulu akili mingi na roho mbaya sana
 

Kichwa Kichafu

JF-Expert Member
Apr 13, 2017
36,967
2,000
Unatumia haya maneno "Maendeleo hayana chama" wakati serikali yako sidhani kama inaamini hayo!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom