Uchaguzi 2020 Askofu Gwajima ameonesha njia, wanaompinga hawana hoja

Hivi kuna mtu ana hofu na Gwajima kugombea ubunge?

Sijui kama kuna watu atawahadaa kama anavyowahadaa wafuasi wake kuwa yeye ni mtumishi wa Mungu.

Utapeli mkubwa wa zama hizi ni kupitia maneno ya Mungu. Gwajima ni miongoni mwa wanaoitumia biblia kutekeleza uovu wake. Kanisani kwake, kidogo kidogo, wafuasi wake wanapatwa na utambuzi. Hali hiyo imemfanya atafute mbinu mpya.

Sent using Jamii Forums mobile app
Acha upotoshaji wewe ,
 
Ukristo una “evolve” kutoka Jesus for love, kupitia Jesus for money na hatimaye Jesus for power.

Hivyo hamna mbaya yeye kutaka kuwa mbunge. Anafuata tu njia ya kawaida ya uibukaji wa dini zote.

Ila kwa ule ujinga aliojaribu kuwalisha watanzania kuwa chanzo cha Covid 19 ni mionzi ya 5G anatakiwa aombe radhi.

Kinyume cha hapo labda wapiga kura waendelee kuamini tu kuwa Saddam Hussein alikuwa rais wa Kuwait/Libya.
 
Wiki yote hii nikikosa update ya maana kwenye forum yoyote narudi kuendelea kusoma hili chapisho🤕.
 
Hawakufanya hivyo. Kwa hiyo suala sio kuchanganya siasa na dini bali hofu dhidi ya nguvu na umaarufu wa askofu Gwajima ambayo wanaificha nyuma ya kihoja dhaifu cha kutokuchanganya siasa na dini. Kama suala ni siasa na dini, mbona hatujawahi kuwasikia wakifanya hivyo huko nyuma?
Mkuu nadhani hoja Kubwa ni Kauli yake ya Kwamba Ubunge, Urais, Uwaziri ni kujishusha; Yeye kama Mtumishi wa Mungu aliongea ivi;
Ila Dini na Siasa sidhani kama ni tatizo na ina mashiko.
 
Kuna wana ccm 175 wenye Nguvu zao kwa nini mnampigia ngoma huyo Gwajima mwenye kutengeneza hela za bure kutoka kwa waumini Wake? Mnataka akusanye zaidi za bure tena? Siyo Kawe labda kwingine!
 
Naona mnapiga kampeni kwa spidi sana...angalia msije mkamponza mwenzenu..Hakuna anaempinga Gwajima...wala hakuna cha kushtua alichofanya...KINACHOSHANGAZA watu ni sababu Gwajima amekula matamshi yake.Nyie mnaojiita watumishi wa Mungu mnapaswa kuwa makini na mnayotamka...

Unakumbuka alichosema Gwajima kuwa hawezi kutafuta Uraisi au Uwaziri au Ubunge SABABU NI KUJISHUSHA HADHI SABABU yeye ni mtumishi wa Mungu..Au mnajitoa upofu....Watu wanachofanya ni kumtumia Gwajima kukumbusha tu kuwa SI VIZURI KUTAMKA MANENO KWA MIHEMKO UNAPOKUA MBELE YA WATU....

Zaidi ya hapo..hamna cha zaidi wa hamna kipya ana haki ya kugombea kama mtanzania mwingine yoyote
Kula matapishi yeye si wakwanza kwani kuna taasisi ilishakula matapishi yake vizuri tu na maanisha Chadema kwa mzee Lowasa
 
- Hofu ya Wapinzani kupoteza jimbo
- Wivu wa wachache
- Hofu za wana mitandao wa muda mrefu

Wiki hii na iliyopita habari kubwa inayojadiliwa kwenye mitandao ya kijamii Tanzania ni uamuzi wa askofu Josephat Gwajima wa kanisa la Ufufuo na Uzima kutangaza nia ya kugombea ubunge katika jimbo la Kawe. Wako waliompongeza na pia wako wanaombeza kuwa anachanganya siasa na dini.

Suala la Mchungaji au askofu kugombea ubunge au kuwa mwanasiasa siyo jambo geni duniani na Hata hapa nchini kwetu. Katika bunge lililopita tulikuwa na mchungaji Peter Msigwa na Mchungaji Getrude Rwakatare ambao wamekuwa wabunge katika awamu mbili zilizopita. Hakujawahi kuwepo na mijadala mikali kinyume na wachungaji hawa kuwa wanachanganya siasa na dini.

Kwa hiyo wanaomshambulia askofu Gwajima ikiwa hoja yao ni kutokutaka Mchungaji kujihusisha na siasa basi ilitakiwa tuwe tumewasikia wakitoa Hoja zao kinyume na Mchungaji Peter Msigwa na Getrude Rwakatare. Hawakufanya hivyo. Kwa hiyo suala sio kuchanganya siasa na dini bali hofu dhidi ya nguvu na umaarufu wa askofu Gwajima ambayo wanaificha nyuma ya kihoja dhaifu cha kutokuchanganya siasa na dini. Kama suala ni siasa na dini, mbona hatujawahi kuwasikia wakifanya hivyo huko nyuma?

Ni jambo lililo wazi kuwa askofu Gwajima ni mmoja Kati wa watu maarufu hapa nchini na mwenye misimamo yake isiyoyumbishwa kirahisi katika mambo anayoyaamini. Mchungaji Gwajima pia ni miongoni mwa watu wenye ushawishi mkubwa na hodari wa kujenga Hoja na kuitetea. Hiki ndicho wanachokiogopa wengi Kati ya wale wanaompinga. Wanaomtaka askofu Gwajima asichanganye siasa na dini sio kwamba wanataka asipotee kwa “kuacha wito wa uchungaji” bali wanaogopa kuwa atawafanya wapoteze jimbo.

Binafsi nilianza kumfuatilia askofu Gwajima kwa ukaribu mwaka 2006. Kipindi hicho wachungaji wengi wa kipetekoste walikuwa wakimpinga lakini aliendelea kusimamia kile alichokiamini na leo Baadhi ya walewale waliokuwa wakimpinga ndiyo wanatafuta kwa udi na uvumba kuwa marafiki zake.

Kuwa na viongozi wa dini kwenye siasa za nchi hii sio jambo geni. Lakini kuingia kwa wachungaji wa aina ya askofu Gwajima ni jambo geni kabisa na ndio sababu ya kelele zinazoendelea mitandaoni. Askofu Gwajima anatengeneza njia ya kuvunja mila isiyo na mashiko iliyohubiriwa muda mrefu ya kutochanganya siasa na dini...

Wako ambao hawamwelewi askofu Gwajima kwa sasa lakini wataelewa tu baadaye. Hili jambo limeonekana geni baada ya askofu Gwajima kutia nia na mimi nafurahi kwa kuwa atatengeneza njia kwa viongozi wa dini (yaani wachungaji na mashehe) wenye vipawa au wito wa kufanya siasa kufanya hivyo na kuendelea pia na wito wa kuwahudumia watu kiroho kama ambavyo wafanyabiashara wanafanya siasa na kuendelea na biashara zao.

Mabadiliko kwenye mambo yaliyozoeleka sio jambo rahisi na huwezekana tu pale mabadiliko hayo yanapoasisiwa na watu wenye misimamo isiyoyumba kirahisi kama alivyo askofu Gwajima. Askofu Gwajima amehimili mikikimiki mingi sana kwenye mambo aliyoyasimamia bila kuyumba. Sio watu wengi wana ujasiri huo.

Nakumbuka miaka ya zamani nikiwa kijana ilikuwa haikubaliki kwa makanisa ya walokole kuwa na vyombo vya muziki maana iliaminika kuwa vyombo vya muziki ni vya kidunia kwani vinatumika kwenye kumbi za muziki na starehe za kidunia. Walokole wengi waliamini kuwa ni kinyume cha maadili ya KiMungu kutumia vyombo vya muziki kwenye Nyumba za ibada. Kanisa la TAG nililokuwa naabudu enzi hizo lilikuwa miongoni mwa makanisa ya mwanzoni kununua vyombo vya muziki na tulionekana kama tumekengeuka kwa kuleta vitu vya kidunia kanisani.

Leo ni jambo la kawaida kwa makanisa kuwa na vyombo vya muziki. Wale walioanza kuvitumia walitengeneza njia. Kile kilichoonekana kama kukengeuka leo ni kitu cha kawaida kabisa. Naamini Ndivyo pia itakavyokuwa kwa suala la kuchanganya siasa na dini. Huko mbeleni wimbo huu usio na mashiko wa kutokuchanganya siasa na dini hautasikika tena.

Kuna makundi kama matatu yanayompinga askofu Gwajima juu ya uamuzi wake huu. Makundi hayo ni “walokole wenzake”, vyama vya upinzani na hasa chadema na baadhi ya wanaCCM. Makundi yote haya yana sababu zake.

“Walokole” wanaompinga askofu Gwajima kuhusu uamuzi wake wa kutia nia kugombea ubunge wanasumbuliwa na ujinga na wivu. Wokovu ulipoingia nchini ulipokelewa na watu wa maisha ya chini na ikaonekana ni dini ya watu dhaifu na walio duni kimaisha. Kwa kukosa mafundisho walokole hawa huona kuwa mambo ya hapa duniani hayana maana. Mawazo yao yako kwenye kuurithi ufalme wa mbinguni na kusahau kuwa mambo wanayoyaita ya kidunia yanaweza kuathiri masuala ya kiroho.

Walokole hawa huona kuwa kusoma shule sio muhimu na kwamba kuwa na fedha nyingi ni ushetani. Ujinga umefanya walokole wengi wadharauriwe na kuonekana vituko kwenye jamii. Watu hawa wenye ujinga Wanapoona Mchungaji anafanya siasa lazima waone amekengeuka. Tunaweza kuwasamehe maana wanasumbuliwa na ujinga na ni ngumu kuwasaidia watu wa aina hii kwa sababu hawajui na hawajui kuwa hawajui. Kuwapuuzia ndiyo stahiki yao.

Watu wengine wanaompinga askofu Gwajima ni wapinzani na hasa mashabiki wa chama cha Chadema. Hawa wanasukumwa na hofu inayoeleweka. Wanachadema wanaijua nguvu ya askofu Gwajima. Wanajua kuwa ikitokea amepitishwa na CCM kugombea ubunge basi watalipoteza jimbo la Kawe. Hawa wanajua kuwa hakuna mgombea wa Chadema anayeweza kumshinda askofu Gwajima kwa hiyo salama yao ni kumpaka matope ili aonekane hafai kufanya siasa. Askofu Gwajima angekuwa hana nguvu wala wasingehangaika kumshambulia.

Ikiwa ni kweli kuwa Wanachadema wanakwazwa na Mchungaji kuchanganya siasa na dini basi walitakiwa wawe walimzuia Mchungaji Msigwa kufanya siasa miaka kumi iliyopita. Mchungaji Peter Msigwa amekuwa Mbunge wa Chadema kwa miaka 10 mfululizo. Kwa nini iwe sahihi kwa Mchungaji Msigwa kufanya siasa lakini isiwe sahihi kwa Mchungaji Gwajima? Kwa nini iwe sahihi kwa Mchungaji Msigwa kuchanganya siasa na dhambi lakini isiwe sahihi kwa Mchungaji Gwajima?

Wanachadema hawa wanaomtukana Leo Mchungaji Gwajima mitandaoni kuwa asichanganye siasa na dini ndio hawahawa ambao viongozi wao wakuu walimwendea ili awasaidie kumleta Lowassa Chadema mwaka 2015 ili agombee uraisi. Kwa hiyo Gwajima kumleta Lowasa Chadema ilikuwa anafanya Kazi ya kuenenza injili na sasa kutaka kugombea ubunge ndio siasa?

Chadema wanaogopa sana kupoteza jimbo la Kawe ambalo wamelimiliki kwa miaka 10 mfululizo. Kile wanachokiogopa Chadema wanajua kitawapata ikiwa askofu Gwajima atapitishwa kugombea ubunge kwa tiketi ya CCM maana hawana uwezo wa kumshinda. Ndiyo sababu wanatumia nguvu yao yote mtandaoni kutukana na kumkashifu ili aache kugombea na wapate nafuu kwenye uchaguzi ujao kwenye jimbo la Kawe. Naamini kama askofu Gwajima angetia nia kugombea ubunge kupitia Chadema basi hawa Vijana wa Chadema wanaomtukana leo wangemshangilia kama Shujaa wao na kumwita kamanda. Kwa hiyo Hoja siyo kuchanganya siasa na dini.

Wako pia wana CCM wanaopinga askofu Gwajima kufanya siasa. Hawa pia wana hofu ya kupoteza nafasi zao maana walishajipanga mda mrefu kugombea jimbo la Kawe na sasa ujio wa askofu Gwajima unatishia adhima yao maana wanaona ni ngumu Kumshinda kwenye Kura za maoni. Hawa nao wanatumia maneno yale yale kuwa asichanganye siasa na dini lakini hawakuwahi kumwambia hivyo mbunge mwenzao wa CCM Mchungaji Getrude Rwakatare.

Kwa nini iwe sawa kwa mama Rwakatare kuwa Mbunge wa CCM lakini isiwe sawa kwa askofu Gwajima kana kwamba uchungaji wa Gwajima ni tofauti na ule wa Mama Rwakatare. Suala sio uchungaji bali hofu ya nguvu na umaarufu wa askofu Gwajima. Kama askofu Gwajima angekuwa Mtu asiye na nguvu au umaarufu usingesikia kelele yeyote mtandaoni juu ya uamuzi wake huo wa kugombea ubunge.

Wiki chache zilizopita askofu Mkuu wa makanisa ya Assemblies of God huko Malawi Lazaro Chakwera alishinda uchaguzi na kuwa raisi wa Malawi kupitia chama cha upinzani. Kwa wasiofahamu, askofu Lazaro alikuwa Mwenyekiti wa taifa wa chama cha upinzani cha MCP na Mbunge wa chama hicho akiwa bado ni askofu Mkuu wa makanisa ya Assemblies of God nchini Malawi.

Askofu Lazaro alistaafu kuwa askofu Mkuu mwaka 2014 lakini akaendelea kuwa Mchungaji na mhubiri wa injili. Baada ya Mchungaji Lazaro kugombea uraisi na kushinda tumewaona wapinzani wengi nchini wakimpongeza. Hatujawahi kuwasikia wapinzani hawa wakimkosoa askofu Lazaro kuwa anafanya makosa kuchanganya siasa na dini. Kwa hiyo kwa wanachadema hawa kwao ni sawa kumshabikia askofu Lazaro anayechanganya siasa na dini lakini kwa wakati huohuo wakimponda askofu Gwajima kuwa asichanganye siasa na dini!

Labda niongelee suala la kuchanganya siasa na dini ingawa katika mijadala inayoendelea mitandaoni linatumika tu kuficha hofu waliyonayo wanasiasa wanaomwogopa askofu Gwajima. Kufanya siasa sio dhambi kwa Mungu wala katika taifa letu. Ni watu wachache sana ambao maisha yao yote wameyaweka kwenye siasa ila wengi wanafanya siasa pamoja na shughuli nyingine. Kwa hiyo suala la kuchanganya siasa na jambo lingine halikwepeki.

Kuna wafanyabiashara wanafanya siasa lakini hatujawahi kusikia wakiambiwa wasichanganye siasa na biashara. Wafanyabuashara hawa hawajaacha biashara. Wanafanya siasa na kuendelea na biashara zao. Wakiwa kwenye biashara hawafanyi siasa isipokuwa biashara na wakiwa kwenye siasa hawafanyi biashara ila siasa. Kama hiyo imewezekana kwenye biashara kwa nini pia isiwezekane kwa kiongozi wa dini kufanya siasa bila kuathiri shughuli zake za kuhubiri mambo ya kiroho?

Kwa nini tunataka kuaminishwa kuwa siasa ni jambo chafu lisilopaswa kufanywa na viongozi wa dini? Kama siasa ni jambo chafu kwa nini serikali inaruhusu jambo chafu kufanyika nchini?? Siasa sio jambo chafu. Siasa inaathiri maeneo mengi sana ya maisha yetu na ni muhimu tuwe na watu Makini kwenye siasa ya nchi yetu.

Kuna wanaomponda askofu Gwajima kuwa anataka kuacha wito wa uchungaji na kujiingiza kwenye siasa kana kwamba amewaambia kuwa anastaafu uchungaji. Mbona wafanyabiashara Huwa hawaachi biashara zao pale wanapojiingiza kwenye siasa? Kwa nini tunataka kuaminishwa kuwa askofu Gwajima ataacha uchungaji pale atakapofanikiwa kuwa Mbunge? Mbona Mchungaji Msigwa hajaacha uchungaji? Mbona mama Rwakatare hakuacha uchungaji? Hoja ya kuwa askofu Gwajima ataacha uchungaji akiwa Mbunge haina mashiko yeyote.

Kwa muda mrefu tumeaminishwa kuwa siasa ni Mchezo mchafu unaochezwa na watu wachafu. Kwa sababu hiyo watu wenye hadhi fulani wameonekana kuwa hawatakiwi kabisa kujihusisha na siasa. Huu ni uongo wa hali ya juu sana.

Maamuzi karibia yote yanayoathiri maisha yetu hufanywa na wanasiasa katika siasa zao. Siasa huathiri mambo ya kiroho, kwa Hiyo tunawahitaji viongozi wa kiroho katika siasa. Siasa inaathiri mambo ya elimu kwa Hiyo tunawahitaji wasomi katika siasa. Siasa inaathiri mambo ya afya kwa Hiyo tunawahitaji watu wa afya katika siasa. Siasa inaathiri uchumi wetu kwa Hiyo tunawahitaji wachumi katika siasa. Siasa inaathiri michezo kwa Hiyo tunawahitaji wanamichezo katika siasa.

Maeneo yote ya maisha yetu yanaathiriwa na Siasa kwa hiyo ni vizuri kuwa na wanasiasa kutoka nyanja zote za maisha. Kuamini kuwa siasa ni mchezo mchafu ni kuamini kuwa maisha yetu tumeyaacha yaamuliwe na watu wachafu kwa kutumia mchezo mchafu!!!

Kuna watu wanasema kuwa kiongozi wa dini ya kikiristo hatakiwi kuwa mwanasiasa maana Yesu hakufanya siasa. Watu hawa wanataka kiongozi wa Kikristo afanye mambo aliyofanya Yesu tu. Lakini watu hawahawa wanaosema hivi utawakuta wameoa wakati Yesu hakuoa. Mbona hawamfuati Yesu kwa kuacha kuoa.

Watu hawa wanaojidai kuwa wanataka kufanya yale aliyofanya Yesu tu utawakuta wanafanya biashara kana kwamba na Yesu naye alikuwa mfanyabiashara. Yesu hakuwa na Mashule yafundishayo elimu dunia lakini viongozi wengi wa dini ya kikiristo wanamiliki Shule nyingi tu. Kama kweli wanafanya aliyofanya Yesu tu basi ilibidi wafanye Kazi ya injili tu. Yesu alisema wale wamwaminio yeye watafanya Kazi alizofanya na zaidi.

Kazi ya siasa ni Kazi ya kuihudumia jamii na hupendeza kama itafanywa na watu wa aina mbalimbali kama vile wanataaluma, wafanyabiashara, viongozi wa dini nk. Kuingia kwa askofu Gwajima katika siasa Kwangu naona kama ni fursa ya kuvunja miiko isiyo na mashiko. Kama kuna wachungaji hawawezi kuchanganya siasa na dini basi wawaache wanaoweza kuchanganya wafanye hivyo kama ambavyo kuna wachungaji wanaochanganya dini na biashara na wengine ambao hawawezi kuchanganya hawafanyi hivyo. Kile ambacho wewe hutaki au huwezi kufanya usitake na wale wanaoweza wasifanye.

Wakristo tunafahamu kuwa Paulo alikuwa mtume na mhubiri wa injili lakini pia alikuwa mfanyabiashara aliyekuwa akishona na kuuza mahema. Ingekuwa leo tungesema kuwa Paulo alikuwa na kampuni ya kushona mahema Lakini bado alifanya kazi ya kuhubiri injili na kuandika nyaraka nyingi kuliko Mtume mwingine yeyote. Biashara haikumzuia Paulo kutimiza wito wake wa kitume. Siasa na biashara haviwezi kumzuia Mtu kutimiza Kazi ya Mungu ikiwa ameitwa kuyafanya yote.

Katika bunge lililopita tulikuwa na mbunge Stephen Ngonyani (prof maji marefu) aliyekuwa mganga wa kienyeji. Hatukusikia makelele kuwa mganga wa kienyeji asichanganye siasa na uganga. Naamini prof maji marefu alikuwa akifanya siasa mda wa siasa na muda mwingine akawa anafanya shughuli za uganga. Kama tumekuwa na mbunge mganga wa kienyeji kwa nini iwe nongwa kuwa na mbunge Mchungaji?

Kuna watu wanaosema askofu Gwajima akiwa mbunge atatumia ubunge wake kuigeuza misikiti kuwa madarasa ya Sunday school maana katika mahubiri yake ya huko nyuma amewahi kusikika akisema anayo ndoto ya misikiti kuwa madarasa ya Sunday school. Hii ni Hoja nyingine dhaifu sana. Hakuna Mtu anayezuiwa kuwa na ndoto. Mwislamu yeyote mzuri ndoto yake ni ya kuyaona makanisa yanageuka kuwa misikiti. Kadhalika pia mkristo yeyote mzuri angependa kuona misikiti yote inakuwa makanisa. Hili sio tatizo ikiwa harakati za kufanya hivyo zitafanyika kwa kufuata sheria za nchi.

Tanzania ni nchi yenye uhuru wa kuabudu. Kila Mtu anayo hiari ya kuchagua dini anayotaka bila kulazimishwa na mtu. Kuna watu walikuwa wakristo lakini Leo ni waislamu. Hakuna aliyewalazimisha ila walisilimu baada ya kusikia mahubiri ya kislamu na kushawishika. Kadhalika pia kuwa watu walikuwa waislamu lakini Leo ni wakiristo. Hawa nao hawakulazimishwa na mtu ila walishawishiwa baada ya kusikia injili.

Wanaotumia Hoja kuwa askofu Gwajima akiwa mbunge atageuza misikiti kuwa makanisa wanajua fika kuwa jambo Hilo haliwezekani bali ni propaganda dhaifu wanayoitumia kupanda chuki na hofu ikilenga kufanya watu wamkatae askofu Gwajima.

Naamini kuwa Kama askofu Gwajima atafanikiwa kuwa mbunge hatahubiri dini kwenye siasa na pia hatahubiri siasa Kanisani kama a na hatukusikia Mchungaji Msigwa au Mchungaji Rwakatare wakifanya hivyo. Askofu Gwajima ni Mtu makini na Sijawahi kumsikia akihubiri dini kwenye shughuli isiyo ya kidini. Akiwa nje ya kanisa lake atakuwa anawahudumia watu wasio na dini, waislamu na wakristo kwa hiyo masuala ya dini hayatakuwa na tija.

Kadhalika askofu Gwajima kwa umakini wake naamini akiwa kanisani kwake hawezi kuhubiri siasa maana Baadhi ya waumini wake ni wanaChadema, ccm na wengine hawana chama. Kama kuna Hoja dhidi ya askofu Gwajima basi iletwe ili wananchi waipime na kuona kama hafai kuwa Mbunge badala ya kuokoteleza vihoja visivyo na mashiko.

Wito wangu kwa askofu Gwajima ni kuwa afanye kile ambacho moyo wake unamsukuma kufanya bila kujali kelele za watu wasio na uelewa au wale wanaotumia vihoja na propaganda dhaifu kumbeza kwa hofu waliyonayo juu yake. Na ikitokea wanaCCM na wananchi wa Kawe wakaona anafaa kuwawakilisha kama Mbunge wao basi awatumikie na kuwaletea maendeleo.

Mimi binafsi namwombea askofu Gwajima afanikiwe kuwa Mbunge wa Kawe. Naona kama Bunge lijalo litakuwa limechangamka sana kama litakuwa na watu wa aina ya askofu Gwajima. Pia kuna wanasiasa waliokuwa wanajiona hawafai kuwa watu wa Mungu kwa sababu wanafanya siasa kwani ilionekana siasa ni Mchezo mchafu. Wanasiasa wa aina hii watatiwa moyo kwa kuona kuwa mtumishi wa Mungu wa aina ya askofu Gwajima pia ni mwanasiasa. Kuna watu wanaompenda Mungu na wana wito wa kufanya siasa lakini wanaogopa kujiingiza kwenye siasa kwa hofu kuwa siasa ni jambo chafu. Ujio wa askofu Gwajima kwenye siasa utawaondolea watu wa aina hii hofu yao na njia itakuwa imetengenezwa kwao kuingia kwenye siasa.

Askofu Gwajima ameonyesha njia; wanaompinga hawana hoja. Gwajima hatakuwa kiongozi wa kwanza wa kiroho kufanya siasa. Lakini ujio wake kwenye siasa unafungua njia na kushusha mlima ili nyuma yake waje viongozi wa dini na wanasiasa wa aina yake ambao huko nyuma walitishwa na maneno kuwa siasa ni mchezo mchafu. Kwa vyoyote vile, siasa za Tanzania zinaelekea kupata mchezaji Mpya wa aina yake. Itengenezee njia baba askofu. Shusha milima. Jaza mabonde. Sawazisha palipotoka. Kuchanganya siasa na dini sio dhambi. Hata nabii Daniel alifanya.

Ni mimi,
Askofu Rogness Laswai
Assemblies of God church
Dar es Salaam

Email: rogness.laswai@gmail.com
Mbona unatutoa kwenye Ukweli kijana , ata Msigwa ni mchungaji lakini pia ni Mbunge, kinachojadiliwa hapa ni UNAFIKI wa Gwajima kudai yeye ni mkubwa kuliko UBUNGE hivyo hawezi KUJISHUSHA sasa kipo WAPI? umekula matapishi yake mchana KWEUPE siku nyingine aache kuropoka kama mtu aliekunywa Gongo , na hili tumalizane nae afute kauli ile hapa mtu anakaangwa na mafuta yake
 
Askofu Rognes kweli una njaa kali mno nimeipima kupitia gazeti uliloandika ukipinga hoja za raia kumkataa Pornstar , tapeli Gwajima , mzinzi wa wazi kwenye public na mbaguzi wa kidini asietaka waislam wakimbizi duniani kupata mahali salama!!

Video ya Gwajima ya ngono nimeiangalia mara kumi nikajihakikishia ni yeye hakuna editing yoyote viungo vyote vya mwili vina uwiano sawa na rangi ya mwili ni moja kuanzia miguu hadi kichwani , ni aibu mno kuwa na kiongozi mzinzi asie na aibu na mbaguzi wa kidini!

wajumbe tupeni heshma wapigakura wenu tuondoleeni takataka Gwajima!
 
Watu mna moyo. Kusoma riwaya ndefu Hivi kutoka kwa mleta mada. Nmesoma robo Ila mtiririko wake na ujengaji wa hoja umenishinda.

Mada haisjawishi kuisoma yote.
 
Wewe umetumwa kumchafulia maana chama kimekataza promo kwenye any media
 
Mkuu iko deep mno. Gwajima ni habari nyingine.
Nakumbuka kipindi cha uchaguzi 2015 wapinzani walisema kwamba nchi hii ingekuwa na akina Gwajima watano tungekuwa mbali..lakini leo kibao kimegeuka, imekuwa dini na siasa..ama kweli mkuki kwa nguruwe
2015 sio 2020 alipofanya zuri aliambiwa na kama kaamua kutafuna kauli zake mwenyewe pia anaambiwa , mtu kama huyu unawezaje kuendelea kumuita mtumishi wa Mungu? jitafakari
 
Hafai kua hata diwani rudi ukamwambie Tena na aache kukutuma kuja na mabandiko marefu hv
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom