Askofu Gwajima afutiwa kesi ya kumtusi Kardinali Pengo

Return Of Undertaker

JF-Expert Member
Jun 12, 2012
4,572
26,885
Na Kulwa Mzee, Dar es Salaam

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imemwachia huru Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima katika kesi ya kutoa lugha ya matusi dhidi ya Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo.

Gwajima ameachiwa huru leo baada ya mahakama kuifuta kesi hiyo kwa sababu upande wa Jamhuri umeshindwa kuonesha kujali kwani kwa miezi 14 wameleta shahidi mmoja kutoa ushahidi.

Hakimu Mkazi Mfawidhi wa mahakama hiyo, Cyprian Mkeha, ametoa uamuzi huo leo wakati kesi hiyo ilipokuja kwa kusikilizwa huku upande wa Jamhuri ukiongozwa na Wakili wa Serikali Mwandamizi, Joseph Maugo, ukiomba upewe ahirisho lingine kwa kuwa hawakuwa na shahidi.

Mkeha aliamua kuifuta kesi hiyo kwa kutumia kifungu cha 225 cha Sheria ya Mwenendo wa Mashauri ya Jinai (CPA) na kumwachia huru Gwajima.

Alisema upande wa Jamhuri umeshindwa kuonesha kujali shauri hilo ambapo ndani ya miezi 14 umeita shahidi mmoja tu.

Gwajima alipandishwa kizimbani mahakamani Aprili 17,2015 akidaiwa kati ya Machi 16 na 25, 2015, katika viwanja vya Tanganyika Packers, vilivyopo Kawe jijini Dar es Salaam, alitoa lugha ya matusi kwa Kardinali Pengo.

Alitamka: "Mimi Askofu Gwajima nasema Askofu Pengo ni mpuuzi mmoja yule, mjinga mmoja, amekula nini yule, sijui amekula nini yule mtoto hana akili yule..”

Chanzo: Mtanzania
 
Pengo padri wa ukweli asie na vinyongo kama gwajima.

Samehe saba mara sabini
 
Eti alisema nae pengo hana vyeti kama bashite
Sasa huyo "Mwanya" anavyo kweli? je hatakiwi nae alete tuvione ili kuonesha njia na mfano bora kwa mkulu wa Dar yetu? Nadhani mkuu nae atahamasika kuonesha vyake nchi itulie. Maana naona TZ kama meli aliyopanda Yona! Yona kama hatumtosei baharini, meli yetu Tz haitokaa itulie!
 
Tatizo serikali ilitaka kutumia kesi hiyo kisiasa wakati aliyestahili kushitaki Kama katukanwa hakwenda mahakamani na wala hakuona tusi lolote alilo tukanwa.

Kesi ya kashfa sheria inasema aliyekashifiwa ndio anayetakiwa kufungua kesi na sio mtu mwingine uwe na kihere here eti umeumizwa Kwa MTU mwingine kutukanwa au kudhalirishwa.

Ndio mana hakuna mashahodi walio jitokeza kutoa ushahidi Kwa kuwa anayesemekana kutukanwa hajafungua kesi hiyo.
 
Naombeni ile audio niisikilize tena, ni wimbo mkali baada ya ule Acheni Waisome #
“Mjinga mmoja, mpuuzi mmoja, sijui amekula maharage ya wapi…… “
 
Pengo anaakili na asingeweza kwenda mahakamani kutoaushahidi ilikubishana na huyo jamaa, gwajima alitaka pengo apaniki ili apatekiki ionekane amewezaku kujibizana na pengo.

Busara aliotumia Pengo nisawa nabusara ya mtuyeyote yule mwenye akili ambae akiwa anaoga alafu akajamtu akachukua nguo na kukimbianazo mtumwenye akili hawezi kumkimbiza alieibanguo maana nayeye atakuasawa na anaekimbia na nguo.
 
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imemwachia huru Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima katika kesi ya kutoa lugha ya matusi dhidi ya Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo.

Gwajima ameachiwa huru leo baada ya mahakama kuifuta kesi hiyo kwa sababu upande wa Jamhuri umeshindwa kuonesha kujali kwani kwa miezi 14 wameleta shahidi mmoja kutoa ushahidi.

Hakimu Mkazi Mfawidhi wa mahakama hiyo, Cyprian Mkeha, ametoa uamuzi huo leo wakati kesi hiyo ilipokuja kwa kusikilizwa huku upande wa Jamhuri ukiongozwa na Wakili wa Serikali Mwandamizi, Joseph Maugo, ukiomba upewe ahirisho lingine kwa kuwa hawakuwa na shahidi.

Mkeha aliamua kuifuta kesi hiyo kwa kutumia kifungu cha 225 cha Sheria ya Mwenendo wa Mashauri ya Jinai (CPA) na kumwachia huru Gwajima.

Alisema upande wa Jamhuri umeshindwa kuonesha kujali shauri hilo ambapo ndani ya miezi 14 umeita shahidi mmoja tu.

Gwajima alipandishwa kizimbani mahakamani Aprili 17,2015 akidaiwa kati ya Machi 16 na 25, 2015, katika viwanja vya Tanganyika Packers, vilivyopo Kawe jijini Dar es Salaam, alitoa lugha ya matusi kwa Kardinali Pengo.

Alitamka: "Mimi Askofu Gwajima nasema Askofu Pengo ni mpuuzi mmoja yule, mjinga mmoja, amekula nini yule, sijui amekula nini yule mtoto hana akili yule..”

Source: Mtanzania
 
Ha haa! Sasa kila mmoja anamgwaya Gwajey! Am sure hata huyo shahidi mmoja alikuwa anaongea kwa kutetemeka!
 
Kuna mtu siku yake imeshaharibika baada ya kusikia habari hii.....
Pengo huwa halumɓani na watukanaji wanaomtukana wawe wakatoliƙi au akina gwajima.Hii case message sent to gwajima kuwa kuna watu hawatukaniki hovƴo hata wakae kimya utakoma.Ni somo tosha kwake.
 
Ha haa! Sasa kila mmoja anamgwaya Gwajey! Am sure hata huyo shahidi mmoja alikuwa anaongea kwa kutetemeka!
Gwajima umesahau kuwa alilazwa ƙwa ƙutetemeƙa kwa presha ya hiyo case alienɗa kanisani akiwa kwenye wheel chair kama kiwete nenɗa kamuulize kama atakuja tukana pengo tena maisha yake yote hana hamu na mzee pengo.jina pengo ukilitaja mɓele ya gwajima lazima aanguke ƙwa presha
 
Back
Top Bottom