Uchaguzi 2020 Askofu Gamanywa: Nimefanya utafiti wa soko la almasi na Tanzanite huko Ulaya, tumeibiwa sana Rais Magufuli ni Mwokozi

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,840
141,765
Askofu Gamanywa amesema Tanzania imeletewa Rais Magufuli na Mungu ili aikomboe kutoka mikononi mwa mabeberu.

Gamanywa amesema baada ya kufanya utafiti huko Ulaya amegundua mabeberu wametuibia sana na Rais Magufuli ameletwa na Mungu kuja kutuokoa watanzania.

Gamanywa alikuwa katika majadiliano yaliyorushwa mubashara na Shalom tv yakimuhusisha pia mwanasiasa machachari aliyekuwa Chadema na sasa yuko CCM Dr David Kafulila aka tumbili.

Chanzo: Shalom tv

Maendeleo hayana vyama!
 
Ulihoji juu ya Bagonza kuonekana na Lissu wakifurahi, ikakuuma sana na ukamsema hapa askofu huyo kwa kujihusisha moja kwa moja na siasa!

Leo umeshasahau,unaandika kwa kujimwaga kabisa bila haya wala soni!

Hizi double standard ni aibu kwenu!
 
Kipindi chote hicho tunaibiwa ni akina waliokuwa madarakani na ambo walikuwa wakisaini hiyo mikataba na kupitisha sheria zake kwa hati za dharura?

Ilitakiwa aseme kwanza tuanze kwa kuwaadabisha hao waliotuingiza kwenye kuibiwa. Mabeberu hawakuja na kuanza kuchukua Almasi zetu kama hawakupewa ulinzi na ushirikiano na watawala waliokuwepo. Hao ndio inatakiwa tuwawajibishe, kwa style gani? Sanduku la Kura litaamua!
 
Ni vyema kwenye utafiti wake aseme ameufanya kuanzia lini hadi lini, na sababu za kuufanya kwenye hicho kipindi
 
Kwahiyo huyo Mungu ndo alimieta Magufuli ili watu wateseke wanavyoteseka saivi!!
 
Ulihoji juu ya Bagonza kuonekana na Lissu wakifurahi,ikakuuma sana na ukamsema hapa askofu huyo kwa kujihusisha moja kwa moja na siasa!0
Leo umeshasahau,unaandika kwa kujimwaga kabisa bila haya wala soni!
Hizi double standard ni aibu kwenu!
Sasa unalinganisha KKKT na Gamanywa?!

Uwe unasoma na kuelewa mada bwashee kuna tofauti kati ya Kanisa na Huduma ya kiroho...... Ndio sababu sijasema mchungaji Msigwa wa Chadema anachanganya dini na siasa!
 
Hawa mbuzi waliona mbali
download.jpeg
 
Hao mabeberu waliletwa na nani kuja kutuibia? kama ni mikataba walisaini na nani? huyo Gamanywa nae kaanza kuwa na mawazo ya kilevi, anaanza kujipendekeza, very soon atapoteza heshima yake.
 
Sasa unalinganisha KKKT na Gamanywa?!

Uwe unasoma na kuelewa mada bwashee kuna tofauti kati ya Kanisa na Huduma ya kiroho...... Ndio sababu sijasema mchungaji Msigwa wa Chadema anachanganya dini na siasa!
au Kama Gwaji Boy anachanganya dini na siasa(CCM)
 
Askofu wewe ndani ya miaka 5 umeona Almasi tu ikiibiwa; wakati watu wanatekwa, wengine wanapotea hadi Leo hawajulikani ni wazima ama lah, yote haya we umeona swafi tu ila hili la wizi wa alamasi ndiyo limekugusa vibaya sana hadi ukiamua ulisemee!!

Haya baba askofu Mungu akulinde!! Sisi tunasonga mbele!!
 
Nani walisababisha tuibiwe?

That's means serikali ya awamu ya 4 na 3 zimehusika sana
 
Back
Top Bottom