Askofu Gamanywa amwalika waziri Pinda kwenye matembezi jumamosi ijayo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Askofu Gamanywa amwalika waziri Pinda kwenye matembezi jumamosi ijayo

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by ASKOFU MSAIDIZI, Nov 6, 2011.

 1. A

  ASKOFU MSAIDIZI JF-Expert Member

  #1
  Nov 6, 2011
  Joined: Jan 11, 2011
  Messages: 209
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  [h=1]Taifa la Vikombe vya Mwaisapile na Gamanywa, Makinda na India[/h]


  Askofu gamanywa wa wapo Mission ameanzisha huduma inayoitwa Mamaritaliana katika vituo viwili vya mwanzo (wapo mission na mbezi jogoo) ammbapo ameingia ubia na masanja mkandamizaji kwenye sekta ya matangazo.

  Mapema januari mwaka huu askofu gamanywa alieka bayana kuwa anaunga mkono tiba ya babu loliondo na kwamba yupo katika utafiti wa ndani ili kuboresha na kuendeleza maono ya babu loliondo.
  Kabla ya babu loliondo kupata misukosuko , askofu gamanywa hajatangaza matokeo ya utafiti wa tiba ya babu lakini amekuja na tiba kama hiyo inayoitwa tba lishe.
  Taarifa kutoka kwa atu waliokwenda wanasema gharama za tiba hiyo ni kubwa mno kwani kumuona daktari ni tshs 20,000/=, kutoa sumu ni shs 50,000/= ambapo dosi ni mara tatu ambapo unatakiwa kulipia tshs 150,ooo/=.
  Mashart ya tiba hiyo ni kwamba kila mtu anasumu mwilini kutokana na kunywa soda ,bia, na vyakula, kuvuta hewa hivyo mtu yoyote anapokwenda hapo ni sharti atoe sumu kwanza ndipo aendelee na uchunguzi mwingine!!!
  Ukisikiliza matangazo yanayotolewa kila baada ya dakika 10 na meneja wa matangazo wapo radio utamsikia vizuri , masanja mkandazaji anasisitiza utoaji wa sumu ili kuingiza tshs 150,000/=
  baada ya kutoa sumu mgonjwa anapewa dose ya dawa kutoka china shirika la dynapharm ambapo inagharimu kuanzia tshs 200,000/=,500,000/=, 1000,000/= kutokana na daktari atakavyo ona uwezo wako.
  Mtu aliyekwenda anasema watu wamekuwa wanapanga msululu mkubwa huku wakiwa wameweka miguu yao kwenge makalai au ndoo na kutolewa sumu ambayo inabadili kabisa maji yanakuwa meusi tiii na daktari anakutisha ‘unaona!!!’ ‘sasa unamatatizo makubwa unatakiwa dose kubwa kuokoa maisha yako”
  huduma hiyo imepanuka na sasa imepelekwa mbezi kwa jogoo ambako askofu gamanywa alikuwa anendesha kanisa lake ili kupata umati mkubwa na sehemu kubwa kwani amepewa maono kuwa umati mkubwa wa mataifa unakuja na sasa huduma ya maombi imesimamishwa mpaka watu watolewe sumu kwanza!!!
  Mmoja wa mhudumu katika huduma hiyo alisikika akisema hata kama mwakyembe ana sumu mwilini inaweza kutolewa.
  Kutokana na kupanuka huduma hiyo , rais kikwete ambaye alifungua kituo hicho amemtuma waziri mkuu mizengo pinda kwenda kufanya matembezi siku ya jumamosi ijayo ilikupata fedha za kuendesha mradi huo.
  Umetokea mgogoro kati askofu gamanywa na daktari wake kutokana na ushauli wa kitaalamu. Daktari huyo ambaye aliwahi kufanya kazi mhimbili amekuwa akipinga kitendo cha kutoa sumu mara kwa mara kwasababu kinadhofisha uwezo wa mwili kutoa sumu wenyewe kupitia jasho na inn. Daktari huyo amekuwa akipinga matumizi ya dawa kwa watu ambao matatizo yao hayajafika kiasi cha kutumia dawa hizo. Hatua hiyo inapingwa na askofu gamanywa ambaye anataka mapato kupitia huduma hizo ili kuwavuta wachina wa dynapharm kuwekeza zaidi!!!
  Uhusiano wa rais kikwete na askofu gammanywa ulianza wakati wa kampeni za mwaka 2010 ambpo askofu gammanywa aliitwa na bernadi membe na kuandaa mikakati ya kuimaliza chadema kupitia agenda ya udini.
  Askofu gammanywa alipewa fungu la kushambulia cdm na akawaita waumini wake na kuitisha mkutano wa waandishi wa habari kilimanjaro hotel dsm na kuwambia watanzania kuwa uchaguzi umetawaliwa na udini!!! Katika mkukutano huo a;iwambia waandishi kuwa yapo makanisa ambayo yanaendesha kampeni za udini .kauli hii ya gamamnywa iliwakera watu wengi . Kampeni kama hiyo ilifanywa na bernadi membe aliyepelekwa mwanza kuishambulia cdm.
  Baada ya kauli hiyo gammanywa na kikwete wamekuwa marafiki wakubwa na sasa wanalipana fadhira!!!
  Kikwete amefungua kituo cha maadili cha askofu gammanywa kinachofanya kazi sambamba na tiba ya samaritalian
  na sasa kikwete amemtuma pinda kuendesaha harambee kuendeleza tiba lishe!!!
  Kabla ya hapo mwaka 2007 kikwete alikataa kumuchangia pesa gamanywa fedha za kununua uwanja wa mbez kwa jogoo mpaka uwanja huo umemegwa na kuuzwa kwa mtu mwingine.
  Hapa ndipo tunaona urafiki wa kikwete na gamanywa umetokana na kampeni za udini!!!
  Mtazamo wangu juu ya suala la tiba na afya , ni bora wananchi tukawa makini na dawa za kichina ambazo ni gharama sana kuliko za kwetu na kwamba kwa kufanywa hivyo tunaua uchumi wa nchi na kukumbatia fedha.
  Pia wachina wametengeneza vitu feki vingi kiasi cha kutengeneza dawa za kuongeza makalio wakati wao wenyewe hawana makalio makubwa na wala hawataki kuongeza!!!
  Serikali ijifunze kutoka kwa tukio la babu loliondo ambalo sasa limekuwa doa kubwa kwa watanzania na limeongeza ushirikina unaochochea mauaji ya maalubino.
  Serikali iboreshe huduma za afya nchini ili kuepuka kupeleka watu india na kuwaacha walalahoi wakiangamia na dawa za kichina mpaka makanisa ya na tumika kupotosha ukweli.
  Kumekuwepo na uzembe mkubwa katika uanzishaji wa kampuni ya kitapeli ya deci ambapo mdau mkubwa katika kanisa alikuwa askofu gammanywa ambaye alitangaza deci kupitia radio wapo lakini ilipokaribia kufa akaenda kuondoa fedha zote na kuwaacha yatima wakitapeliwa. Askofu gamanywa akiwa mwenyekiti wa pct ndiye aliyeunganisha usajili wa kanisa la delivelence church la jackson mtares lilimiliki share kubwa deci na kuyavuta makanisa mengi kuingia
  wakristo na waislamu wengi wanamiminika kwenye tiba ya askofu gamanywa kama walivyomimika kwenda kupanda mbegu deci
  tahadhari iliyopo ni kwamaba matangazo yote ya wapo radio yamekuwa ni tiba ya askof gamanywa tu!!
  Kinacho itenganisha jamii ya walala hoi na matajiri walio jikita kiungozi serikali ni ni kuwa wao wakiugua kamasi tu basi panado wanazifuata India kwa vocha ya Mama Makinda huku sie tukikimbiziwa Loliondo kwa punda.
   
 2. Albedo

  Albedo JF-Expert Member

  #2
  Nov 6, 2011
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Askofu Mbona unaonekana Mtu wa Fitna, Majungu na kila aina ya Uzandiki kwa Huduma za Wenzako?
   
 3. N

  Ntambaswala JF-Expert Member

  #3
  Nov 6, 2011
  Joined: Dec 7, 2008
  Messages: 255
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Hivi kwanini watu saba kati ya kumi, wanaojinufaisha kiujanja hapa nchini wanakuwa kwa asili sio Watanzania
   
 4. g

  gambagumu JF-Expert Member

  #4
  Nov 6, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 697
  Likes Received: 296
  Trophy Points: 80
  pumba hueleweki
   
 5. yutong

  yutong JF-Expert Member

  #5
  Nov 6, 2011
  Joined: Apr 15, 2011
  Messages: 1,604
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  kazi tunayo
   
 6. A

  ASKOFU MSAIDIZI JF-Expert Member

  #6
  Nov 6, 2011
  Joined: Jan 11, 2011
  Messages: 209
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  sikiliza Radio Wapo Ujue ukweli sasa hivi Usiwe mvivu Kufuatilia!!
  Utajua Mbivu Na Mbichi
   
 7. A

  ASKOFU MSAIDIZI JF-Expert Member

  #7
  Nov 6, 2011
  Joined: Jan 11, 2011
  Messages: 209
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kama Kuna Mtu ni Mgonjwa ni Bora akatoe Sumu Kwani hata Loliondo Mawaziri Walikwenda lakini sasa hivi wamegeuka wanakwenda India.


   
 8. A

  ASKOFU MSAIDIZI JF-Expert Member

  #8
  Nov 6, 2011
  Joined: Jan 11, 2011
  Messages: 209
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  [h=3]Rostam aponda tiba ya Mchungaji Loliondo[/h] WAKATI Watanzania wengi wakimiminika kwenda wilayani Loliondo, mkoani Arusha kupata dawa inayodaiwa kutibu magonjwa sugu, Mbunge wa Igunga (CCM), Rostam Aziz ameibuka na kusema tiba hiyo haina lolote akidai kwamba ndugu zake watano wameitumia lakini hawajapona.

  Akihutubia wananchi katika mkutano wa hadhara wa kuwashukuru wapigakura uliofanyika kwenye Viwanja vya CCM wilayani Igunga, Tabora mbunge huyo alisema haiamini dawa hiyo kwa kuwa ana ushahidi kwa ndugu zake hao ambao anadai kwamba wanaendelea kuugua kisukari licha ya kutumia dawa hiyo siku saba zilizopita.

  Aliwataka wale watakaokwenda Loliondo ambao wanatumia dawa za hospitalini kuendelea kuzitumia badala ya kuzipuuza na kuzitupa... "Ndugu zangu wananchi wa Igunga, mimi mjomba wangu Hassan mnamfahamu karibu wote hapa mjini ni mgonjwa wa siku nyingi wa kisukari. Ameshakunywa dawa hiyo lakini mpaka sasa ni mgonjwa kama mnavyomuona sasa hiyo dawa inaponyesha nani?"

  Hata hivyo, aliwataka wananchi wote wenye imani juu ya dawa hiyo waende huku akiwasisitizia kutopuuza ushauri wa madaktari kwani.

  Wakati Rostam akipinga dawa hiyo, wilayani Kahama, mamia ya wafanyabiashara wamefunga shughuli zao na kukimbilia Loliondo kwa Mchungaji Mwasapile kunywa dawa hiyo huku baadhi ya waliorejea baada ya kuinywa wakidai kuwa hali zao sasa ni nzuri.

  Wafanyabiashara hao wengi wao wanaondoka kwa siri wakidai wanakwenda Dar es Salaam katika shughuli zao, lakini siri imefichuka baada ya baadhi yao kuoneka katika runinga wakiwa katika foleni wakisubiri kupatiwa huduma hiyo.

  Mbali ya kuzungumzia suala hilo la tiba ambalo limegusa hisia za wananchi wengi wa Afrika Mashariki, mbunge huyo aliwapa pole wananchi wa Igunga ambao nyumba zao zimeezuliwa na upepo uliosababishwa na mvua kubwa zilizonyesha wiki iliyopita ambazo ziliathiri kaya 19. Aitoa msaada wa Sh500,000 kwa kila kaya iliyokumbwa na maafa hayo.


  Source:mwananchi.co.tz
   
 9. A

  ASKOFU MSAIDIZI JF-Expert Member

  #9
  Nov 6, 2011
  Joined: Jan 11, 2011
  Messages: 209
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mambo sasa yameiva baada ya kiongozi wa Wapo mission Askofu Silvester Gamanywa kuandaa mdahalo rasmi wa wanatheolojia kuchambua iwapo kuna uhalali wa tiba ya babu wa Loliondo kibiblia au hapana, utafiti wa kina uliofanywa na blog hii umebaini kuwa wadau wengi wengependa mdahalo huo uwalete pamoja Askofu Zachary Kakobe, Mzee wa Upako Lusekelo, Askofu Malasusa, Askofu Mokiwa, Mwingila,Mufti Simba na Askofu Methodius Kilaini. Mjadala huu unafatia kile kinachoonekana kuwa ni minyukano na misigano inayoendelea baina ya viongozi wa dini hapa nchini kuhusu tiba ya babu Mwasapile huko Loliondo ambapo kuna baadhi wanaunga mkono tiba hiyo huku wengine wakipinga vikali.
   
 10. mpayukaji

  mpayukaji JF-Expert Member

  #10
  Nov 6, 2011
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 943
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Jamani mbona cheo cha uaskofu siki hizi hakina hata maana? Tangu lini tapeli kama Silvester Gamanywa akawa askofu zaidi ya aspofu? Gamanywa hana roho mtakatifu bali roho mtakakitu. Hii ni mbegu chafu inayojumuisha matapeli kama Kakobe Rwakatare, Mzee wa Upako, Mwakasege na matapeli wengine waliotamalaki nchini kwetu wakiwaibia wajinga wachache kwa madai ya kuwaba huduma wakati wanachowapa ni hujuma. Gamanya alianzia Keko utapeli wake kabla ya kumuingiza mjini aliyekuwa waziri mkuu Fredrick Sumaye na kuweza kupata mshiko kiasi cha kununua uwanja Mbezi Jogoo. Dereva wake aliyekuwa na rasta aitwaye Emmanuel Masala aliishia kuwa mtu wa kukata tamaa baada ya kutapeliwa na tapeli Gamanywa. Ni vizuri wajinga wanaowaamini hawa matapeli kuelevuka na kuondokana na kunyonywa na hawa mbwa mwitu waliovaa mavazi ya uchungaji na uaskofu.
   
 11. j

  jani Member

  #11
  Nov 6, 2011
  Joined: Aug 8, 2011
  Messages: 87
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 15
  hiyo stori ya kuhusu gamanywa na loliondo sio ukweli....hakukubaliana na babu wa loliondo alisema anaifanyia uchunguzi...sema hakushauri mtu aende huko....af hlo swala la kununua kiwanja mbezi baada ya kumtapeli sumae ni saundi....mpaka kesho wana bomba la deni wanalipunguza taratib taratib hawakukinunua chote kama kreti la bia
   
 12. Muke Ya Muzungu

  Muke Ya Muzungu JF-Expert Member

  #12
  Nov 7, 2011
  Joined: Jun 17, 2009
  Messages: 3,451
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 0
  jamani hacheni wivu. mimi ni muumini kwa gamanywa. huyu mzee ni bomba kweli tena ndo askofu wa ukweli hapa nchini. hachana na wakina kakobe, wengine wivu tu. kama ana uwezo wa mungu kutoa sumu mwilini, mwacheni atoe, kwani kawalazimisha kwend akwake? majitu mengine bwana
   
 13. M

  Mwamakula JF-Expert Member

  #13
  Nov 7, 2011
  Joined: Nov 7, 2010
  Messages: 1,893
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  Kama Askofu Gamanywa anaamua Kutoa Sumu hakuna anaye mkataza ila kazi hiyo inafanywa na Dctk ISAAC NDODI na SAMSONI KIBONA. Anapaswa kujua hilo ili ajue maadui zake!!!
   
 14. M

  Mwamakula JF-Expert Member

  #14
  Nov 7, 2011
  Joined: Nov 7, 2010
  Messages: 1,893
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  Pesa inayotegemewa kwa ajili ya Hatua za mwanzo za Mradi wa TIBA LISHE a.k.a Samaritaliani ni 500,000,000/=.

  PINDA ANAKAZI KUBWA YA KUCHANGISHA PESA HIYO!!!!
   
 15. M

  Mwamakula JF-Expert Member

  #15
  Nov 7, 2011
  Joined: Nov 7, 2010
  Messages: 1,893
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  changia mradi wa tiba ya askofu gamanywa sambamba na wachina kwa bsnk crdb a/c 01j1013657901 ukitaka piga simu 0787 582845.

   
 16. S

  SIKUOGOPI Member

  #16
  Nov 7, 2011
  Joined: Oct 3, 2011
  Messages: 27
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Gamanywa huwezi kumtofautisha na Mama Rwakatare! Maana wote ni Matapeli tu! Tena ni wataalamu sana na Siasa za Makanisa juu ya Miradi Ndani ya Makanisa!

  Gamanywa haki ya kimsingi anayo juu ya kutafuta pesa kwa ajili ya Maisha ya familia yake but si Kulazimisha masuala ya Binafsi na
  maendeleo yake binafsi kulilazimisha Kanisa kushiriki.

  Mradi wa Tiba mbadala anaondesha kiibinadamu ni sawa! Ila yeye ni Mtumishi kwa nafasi yake anafundisha nini Waumini kama si Kulazimisha kununua Dawa badala ya Maombi.

  Tukubaliana bila unafiki wowote Gamanywa kwa hili ni Tapeli tu na Fedhuli wa Kiimani kama Mama Rwakatare anavyofundisha waumini Kutegemea Vitambaa! Badala ya Kumtegemea Mungu!

  Haki ya Muhimbili ni Kumpa Mgonjwa Tiba ya Kitaalamu maana ni Muhimbili si Kanisa!

  Haki ya Isack Ndodi ni Tiba Mbadala tena Baada ya Kutibiwa na Muhimbili nawe kwa kutokuamini vipimo vya Muhimbili ndipo unaenda kwa Miti Shamba ya Ndodi na maana wao wamejipambanua mapema sana! Tiba mbadala!

  Sasa kote huku ukishindwa ndo unakimbilia Kanisani kupona kwa Imani yako! Tena Baada ya Maombi!.

  Je nini maana yake Gamanywa kufanya Tiba badala ya Maombi ?

  Kanisa Katoliki na Lutherani pia Anglican wao wanazo Hospitali za kawaida kabisa ambazo zitatoa tiba kama za Muhimbili na Si Tiba Mbadala kama anavyofanya Gamanywa!

  Gamanywa atueleze wazi tu kwamba hili dili ni langu ni Kanisa analoliongoza yeye linalotoa Huduma Hii.

  Narudia tena Gamanywa kwa Hili wewe ni Tapeli na Fedhuli wa Kiimani.
   
 17. k

  kazuramimba Senior Member

  #17
  Nov 7, 2011
  Joined: Jun 14, 2011
  Messages: 107
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Askofu gamanywa anakosea sana nashindwa kuelewa kwa nini hajifunzi lile swala la DECI yeye ndie alie lianzisha na lili muaibisha sana but still hajajifunza.Kiukwel amepotoka sana na huu ni uhuni hamna kitu kabisa.Binafsi nina mfahamu mama mmoja alie tolea sumu na mimba ikatoka mwingine alitolewa mara mbili sasa hivi ukimwona utazani ana ukimwi kakonda kupindukia.
   
 18. M

  Mwamakula JF-Expert Member

  #18
  Nov 8, 2011
  Joined: Nov 7, 2010
  Messages: 1,893
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  Tiba ya Gammanywa inapaswa Kuchunguzwa na serikali!!!!
   
 19. Muke Ya Muzungu

  Muke Ya Muzungu JF-Expert Member

  #19
  Nov 8, 2011
  Joined: Jun 17, 2009
  Messages: 3,451
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 0
  Askofu inaonekana unayomengi sana moyoni. tunaomba habari zaidi ili tujue kama ni kuchunguzwa waanzie wapi. Naona siyo tiba tu. Juzi nimeona hadi mama Happy Gamanywa kwenye thredi hii na wachaga kibao waliopewa nafasi Wapo redio na gazetini, tujuze sisi hatujui mengi
   
 20. Kiby

  Kiby JF-Expert Member

  #20
  Nov 8, 2011
  Joined: Nov 16, 2009
  Messages: 5,205
  Likes Received: 1,007
  Trophy Points: 280
  Gamanywa alikuwa mhubiri wa kipentekoste mzuri tu, ila kilichomharibu ni pale Ben Mkapa alipomlambisha pesa ya walipa kodi kwa kumpa ukurugenzi wa taasisi ya ukimwi nchini. Kuanzia hapo roho ya gamanywa iligeuka na amekuwa akitafuta fursa ya kuwa karibu na mafisadi kibiashara. Alijaribu komsogelea Jk mwanzoni mwa serikali yake akatolewa nje. Sasa hivi amefanikiwa kusogezwa baada ya kukubali kutumiwa katika uchaguzi uliopita kwa kuwaaminisha watanzania kuwa chadema ni wadini. Narudia tena kusema mtu ambaye amekwisha kulifanya kanisa kuwa pango la wanyang'anyi kwa biashara zake hawezi kamwe kusahihika na kumrudia Mungu katika utakatifu wake. Hivyo kupigizana kelele na gamwanya kuzitofautisha deal zake na kanisa, ni sawa na kutwanga maji kwenye kinu ama kuloweka jiwe majini ukitarajia litalainika.
  .
   
Loading...