Askofu Gamanywa amuomba Waziri Simbachawene serikali iunde Tume ya Maadili ya Viongozi wa Dini na mwenyekiti ateuliwe na Rais!

Kuhani mussa mwacha anakuja juu. Mutu ya kongo hiyo inahubiri injili ya miujiza. Baba yake aliyemlea Mulilege mukombo alias Mzee wa yesu yuko wapi.
 
Yaani anataka wanasiasa waanze kuwapangia kwenye dini zao? Anaamini sana wanasiasa? Anawaona wanasiasa ni malaika?
 
Askofu Gamanywa amemuomba waziri wa mambo ya ndani mh Simbachawene aishauri serikali iunde chombo cha kusimamia maadili ya viongozi wa dini kama ilivyo Tume ya Maadili ya Watumishi wa Umma.

Gwajima ameomba chombo hicho kiitwe Tume ya Maadili ya viongozi wa dini na mwenyekiti wake awe anateuliwa na Rais wa JMT.

Waziri Simbachawene ni mgeni rasmi katika kongamano la Wapentecoste.

Source: Wapo Radio/ Shallom tv
Mmmh! Unaomba serikali iamue mambo ya imani, sidhani kama hilo limekaa sawa. Labda ndani ya mikusanyiko ya kimadhebu kwa mfano pentecostal waunde chombo hicho na wakisimamie wao kwa umoja wao na kanuni zao na imani yao.

Wakamjibu, “Ni vya Kaisari.” Basi Yesu akawaambia, “Mpeni Kaisari kilicho cha Kaisari, naye Mungu mpeni kilicho cha Mungu.”
Mathayo 22:21 NEN
 
Umenikumbusha meme ya "Govern me harder" ....wakati watu wanajioelewa wakitaka kupunguzia madaraka serikali zao,,hawa wapumbavu wanataka tuongezee hawa viongozi nguvu...hivi wana akili kwli?
 
Maadili wanavunja serikali wenyewe. Mke Kigoma Mme Dodoma. Hao watoto watakaozaliwa wanalelewa na nani? Huyo Mama au baba anaebaki pekeeyake atawezaje kujiepusha na majaribu kulinda maadili.
 
Amesema Bakwata, TEC, CCT na Pentecoste watakuwa na uwakilishi kwenye Tume kwa kutoa wajumbe!
Serikali inashindwa kusimamia mashirika yake na bila kujali manufaa yake kwa wananchi wanaamua kuyaua kwa makusudi bila sababu yoyte ya msingi.
Mfano waziri wa fedha Mwingulu anatangaza kufilisi shirikalaa PRIDE africa ambalo bado ni tishio kwenye soko pamoja na kuwa nje ya ulingo kwa miaka kadhaa. Badala ya kufanya taratibu za kitaalmu wanaamua kwa mihemuko na kujihani eti linamadeni mengi. Wamezembea wenyewe na sasa wanataka kudhurumu haki za hao kina mama maskini. Bila aibu kwamb amwaka huu mwezi wa tatu mapka wa tano wizara yake imekwiba kwa kughushi mabilioni ya fedha kama alivyotangaza waziri mkuu. Baada ya hapo kimya!. Wanaua PRIDE, hawa ni watu wa kuwaongezea majukumu mengine zaidi?

Majukumu ya serikali inashindwa kuyafanya, watu wanapata stress na wengine wakuwa katika hali tete. Wakipigwa huko, hukimbilia kwa Mungu ili wakapate tiba, halatu leo tena unataka wakikimbilia kwenye Imani nako wakute ccm ile ilie isiyowajali!.

Ndugu yangu acha. Unataka kusababisha watanzania wengi wapoteze maisha. Waache watu waabudu na kuomba Mungu wao kwa uhuru kwa imani zao na kwa kuwa ndiyo sehemu pekee inayowasaidia waendelee kuishi.
 
Kama kweli hivi ndivyo alivyosema Gamanywa, taifa letu litakuwa limefika pabaya Sana tena Sana na katika hili hadhi ya uaskofu wa Gamanywa utakuwa na mashaka Sana hali inayoweza kutafsiriwa kama dhana ya ushindani wa kimaslahi makanisani

Tokaa enzi na enzi hadi sasa duniani kote taifa hutegemea wakuu wa dini kama nyenzo muhimu Sana ya awali na endelevu katika kujenga maadili ya watu wake wakiwemo wanasiasa wote, ni kituko kikubwa kumsikia askofu akiomba msaada wa nguvu ya kidola kulinda maadili ndani ya himaya zao.

Kwa namna hii, hapa anatafuta waandae mtu ndani ya Baraza lao atakaye pewa nguvu ya dola kuwamaliza washindani wenzake katika kuponda fedha za wanaomtafuta Mungu au pia kumshughulikia aliye na mawazo mbadala yasiyoifurahisha serikali.
 
Askofu Gamanywa amemuomba waziri wa mambo ya ndani mh Simbachawene aishauri serikali iunde chombo cha kusimamia maadili ya viongozi wa dini kama ilivyo Tume ya Maadili ya Watumishi wa Umma.

Gwajima ameomba chombo hicho kiitwe Tume ya Maadili ya viongozi wa dini na mwenyekiti wake awe anateuliwa na Rais wa JMT.

Waziri Simbachawene ni mgeni rasmi katika kongamano la Wapentecoste.

Source: Wapo Radio/ Shallom tv
Tatizo ni nini bwashe hadi Ngamanywa kufikia hatua ya kuomba hiyo tume? Viongozi wa Dini wanamisbehave?
 
Nadhani hujafamu vizuri uwezo alionao Mch. Gamanywa kwa uhalisia hata Kakobe aliyekutwa na bil 6 bank hampati. Huyo analingana na hadhi ya Mwingira wa efatha.

Ana pesa ya kutosha tuu. Ana uwezo wa kununua kiwanja mil 400. Yuko vizuri mpakwa mafuta wa bwana. Nadhani hata gwajima hampati kwa pesa huyo mtumishi.
Mbona kama vile hujatueleza vitega uchumi vyake tukaelewa vizuri sheikh,
 
Kuhani mussa mwacha anakuja juu. Mutu ya kongo hiyo inahubiri injili ya miujiza. Baba yake aliyemlea Mulilege mukombo alias Mzee wa yesu yuko wapi.
Wakati anasimuliaga huduma aliyolelewa ndio walimsumbua sana alipoanza ya kwake, mpaka kumfanyia figisu kwa rushws ili azuiwe kuhudumu,
 
Askofu Gamanywa amemuomba waziri wa mambo ya ndani mh Simbachawene aishauri serikali iunde chombo cha kusimamia maadili ya viongozi wa dini kama ilivyo Tume ya Maadili ya Watumishi wa Umma.

Gwajima ameomba chombo hicho kiitwe Tume ya Maadili ya viongozi wa dini na mwenyekiti wake awe anateuliwa na Rais wa JMT.

Waziri Simbachawene ni mgeni rasmi katika kongamano la Wapentecoste.

Source: Wapo Radio/ Shallom tv
Inaonesha wazi hii ilimlenga Gwajima hadi ukashindwa ficha hisia zako na kumwandika katika habari.
 
Back
Top Bottom