TataMadiba
JF-Expert Member
- Feb 7, 2014
- 9,866
- 5,742
Jana 31/01/2016 ilikuwa ni siku ya kumuingiza kazini Askofu Mkuu wa Kanisa la KKKT, Fredrick Shoo. Shughuli iliyofanyika katika Kanisa Kuu la KKKT, mjini moshi. Mgeni rasmi katika ibada hiyo muhimu alikuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Majaliwa Kassim Majaliwa.
Ibada hiyo pia ilihudhuriwa na Waziri Mkuu aliyeshinikizwa kujiuzulu kutokana na kashfa ya mkataba tata wa Kampuni ya kufua umeme wa dharura ya RICHMOND.
Leo takribani magazeti yote yameandika kauli ya Askofu Fredrick Shoo kuhusiana na Serikali ya Magufuli, Vyombo vya dola na mihimili ya yake.
Kwenye kurasa za mbele kabisa za magazeti zimepambwa na vichwa vya habari kama: "ASKOFU AMPASULIA JIPU MAJALIWA LA POLISI KUINGIA BUNGENI", "ASKOFU MPYA KKKT AONYA UTUMBUAJI MAJIPU", "ASKOFU MPYA KKKT AWASHUKIA POLISI", "MAGUFULI AONYWA".
Kazi ya utumbuaji majipu inafanywa na viongozi wenye akili timamu na makini tena kwa mujibu wa sheria na taratibu za nchi. Aidha Bunge ni muhimili ambao watu wenye taaluma mbalimbali wakiwemo wanasheria. Ni muhimili unaofanya kazi kwa kufuata kanuni, sheria na Katiba ya nchi.
Iweje leo Kiongozi wa kanisa aone kama yote hayo ni kinyume na kanuni, utaratibu, sheria na Katiba ya nchi?