Askofu Fredrick Onael Shoo ashinda kuwa Mkuu wa Kanisa la KKKT

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
117,217
217,186
Askofu Dr.Fredrick Shoo (PhD) AMESHINDA uchaguzi wa kumpata mkuu wa kanisa la KK.jpg


Dkt. Frederick Onael Shoo ametangazwa mshindi usiku huu dhidi ya wagombea wengine na ataongoza Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) kwa kipindi cha miaka minne.

Alikuwa akichuana na Maaskofu wenzake akiwemo Dr. Steven Munga, Dr. Abednego Keshomshahara, Blaston Gavile na Dr. Alex Malasusa (ambaye amewahi kuongoza KKKT katika cheo hicho kwa miaka 8).

Dkt. Shoo amepata kura 144 huku mshindani wake wa karibu, Dkt. Keshomshahara akipata kura 74 kati ya kura 218 zilizopigwa (katika mzunguko wa mwisho baada ya kubaki wawili).

Dkt. Shoo alichaguliwa kwa mara ya kwanza kuongoza Kanisa hilo Agosti mwaka 2015 baada ya kupata kura 153, dhidi ya Dkt. Munga aliyepata kura 67 wakati huo

=====

Arusha. Dk Frederick Shoo amechaguliwa tena kuwa mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) baada ya kupata kura 144 dhidi ya 74 za mpinzani wake.

Kwa ushindi huo, Dk Shoo anaendelea kuliongoza kanisa hilo kwa miaka mingine minne na kufuata nyayo za wakuu wa kanisa hilo waliomtangulia walioliongoza kwa vipindi viwili vya miaka minne.

Ametangazwa kuwa mshindi usiku wa kuamkia leo Jumamosi Agosti 24, 2019 baada ya kumalizika kwa uchaguzi uliofanyika mjini Arusha na kutawaliwa na kila aina ya upinzani.

Alipata kura 144 kati ya 218 huku mpinzani wake Askofu Abednego Keshamshahara wa Dayosisi ya Kaskazini Magharibi akipata kura 74.

Chanzo: Mwananchi
 
Mlifurahi na kupiga vigelegele trump aliposhinda uchaguzi mkiamini chadema itakuwa kama.

Mkafurahi na kupiga vigelegele kenyatta aliposhinda uchaguzi mkiamini mtakuwa kama.

Leo mmeamia kwa shoo, hebu jipeni space maana mwisho wa siku huwa mnabaki yatima
 
Taarifa za uhakika ni kwamba Dr Shoo ametangazwa mshindi usiku huu dhidi ya wagombea wengine na ataongoza kanisa hilo kwa kipindi cha miaka minne .

Alikuwa akichuana na Maaskofu wenzake akiwemo Dr Steven Munga , Dr Abednego Keshomshahara , Blaston Gavile na Dr Alex Malasusa ( ambaye amewahi kuongoza KKKT katika cheo hicho kwa miaka 8 )

Taarifa zaidi zitaendelea kumiminwa hapa hapa
Kanisa la huko, viongozi wa huko
 
Taarifa za uhakika ni kwamba Dr Shoo ametangazwa mshindi usiku huu dhidi ya wagombea wengine na ataongoza kanisa hilo kwa kipindi cha miaka minne .

Alikuwa akichuana na Maaskofu wenzake akiwemo Dr Steven Munga , Dr Abednego Keshomshahara , Blaston Gavile na Dr Alex Malasusa ( ambaye amewahi kuongoza KKKT katika cheo hicho kwa miaka 8 )

Taarifa zaidi zitaendelea kumiminwa hapa hapa
Uongo wagombea walikuwa watatu tu waliopigiwa kura huo mlolongo wako feki na matokeo yako feki
 
Bado uchaguzi haujafanyika wapo kwenye taratbu za kufanya uchaguz. Huu ni uzushi tu.
 
Mulifurahi na kupiga vigelegele trump aliposhinda uchaguzi mkiamini chadema itakuwa kama......
Mkafurah na kupiga vigelegele kenyatta aliposhinda uchaguzi mkiamini mtakuwa kama.....
Leo mmeamia kwa shoo, hebu jipeni space maana mwisho wa siku huwa mnabaki yatima
Mkuu acha jazba,ulikuwa na maslahi na mambo ya kanisa au
 
Taarifa za kweli zitatolewa usiku huu ila kwa wakati huu hii c ya kweli
 
Mkuu acha jazba,ulikuwa na maslahi na mambo ya kanisa au
Jazba wapi nyie ni wajinga, kazi kugeuzwageuzwa tu! Mlipiga vigelegele trump alivyoshinda sijui mlikuwa mnajua mtaenda marekani
Ghafla mkaanza kumshobokea kenyatta
 
Back
Top Bottom