Askofu Fredrick Onael Shoo ashinda kuwa Mkuu wa Kanisa la KKKT

View attachment 1188638

Taarifa za uhakika ni kwamba Dr Shoo ametangazwa mshindi usiku huu dhidi ya wagombea wengine na ataongoza kanisa hilo kwa kipindi cha miaka minne .

Alikuwa akichuana na Maaskofu wenzake akiwemo Dr Steven Munga , Dr Abednego Keshomshahara , Blaston Gavile na Dr Alex Malasusa ( ambaye amewahi kuongoza KKKT katika cheo hicho kwa miaka 8 )

Taarifa zaidi zitaendelea kumiminwa hapa hapa
Kwahyo malasusa kumbe hajastaafu mbona anagombea tena?
 
Yule kahaba mkuu yezebeli na kijakazi wake alexelias wameanguka kwa aibu!!

Nasikia nyamitako alikua anagawa mahela ili Dr Shoo ashindwe sasa kashindwa yeye

Kugawa pesa kwenye taasisi za kidini ili kufanikisha mambo yao sio jambo geni, jaribu kufuatilia chaguzi na teuzi za nyuma ndani ya taasisi za dini utaona traces mbalimbali zinazoashiria kitu hiyo au jikumbushe jinsi gani Askofu Kilaini na Nzigirwa walivyorudisha pesa za Escrow baada ya magazeti kuandika
 
Sipendi kabisa watu kumuhusisha Askofu wetu na Siasa.Daktari Shoo anasimama kwenye haki akiona zinakanyagwa na si anaibuka tu.Hajaonyesha mapenzi yake waziwazi kwa upande wowote.Niishie kwa kusema Hongera Dr.Shoo kwa kupewa kibali tena na Mungu
 
Haya makanisa ya kupigiana kura hatari sana maaskofu wanalogana balaa hahaaaa siwezi sahau uchaguzi uliomuondoa mwakyolile jinsi hawa watumishi walivochezeana huko mbeya.
Mwakyolile yule wa Konde?? Tiririka mkuu!!

Ingawa wengine tulijua Dr. Shoo atarudi, ni nadra sana kwa askofu aliyepo madarakani kuondolewa.
 
Ndo maaana wanaingilia siasa za ndani, kwenye kura kuna kampeini hvo nawao hawana mungu n siasa tu kma ccm na act
 
View attachment 1188638

Taarifa za uhakika ni kwamba Dr Shoo ametangazwa mshindi usiku huu dhidi ya wagombea wengine na ataongoza kanisa hilo kwa kipindi cha miaka minne.

Alikuwa akichuana na Maaskofu wenzake akiwemo Dr. Steven Munga, Dr. Abednego Keshomshahara, Blaston Gavile na Dr. Alex Malasusa (ambaye amewahi kuongoza KKKT katika cheo hicho kwa miaka 8).

Dkt. Shoo amepata kura 144 huku mshindani wake wa karibu, Dkt. Keshomshahara aliyepata kura 74 kati ya kura 218 zilizopigwa.
Huu utaratibu wa kupigiana kura kwa kazi ya Mungu unayagawa sana makanisa. Hapo walioshindwa kufika mahali wakakubali na kutoa ushirikiano kwa mteule/mshindi itahitaji miaka mingine miwili.
 
View attachment 1188638

Taarifa za uhakika ni kwamba Dr Shoo ametangazwa mshindi usiku huu dhidi ya wagombea wengine na ataongoza kanisa hilo kwa kipindi cha miaka minne.

Alikuwa akichuana na Maaskofu wenzake akiwemo Dr. Steven Munga, Dr. Abednego Keshomshahara, Blaston Gavile na Dr. Alex Malasusa (ambaye amewahi kuongoza KKKT katika cheo hicho kwa miaka 8).

Dkt. Shoo amepata kura 144 huku mshindani wake wa karibu, Dkt. Keshomshahara aliyepata kura 74 kati ya kura 218 zilizopigwa.
Jamaa walitaka kuingiza mtu wao.. Walidhani Kanisa ni sawa na chama chao kwamba polisi ndio wana wasaidia kuiba kura halali.. Mungu kwetu sisi ni kimbilio ... Msaada uonekanao wakati wote.. Bravo Dr. Shoo..
 
View attachment 1188638

Dkt. Frederick Onael Shoo ametangazwa mshindi usiku huu dhidi ya wagombea wengine na ataongoza kanisa hilo kwa kipindi cha miaka minne.

Alikuwa akichuana na Maaskofu wenzake akiwemo Dr. Steven Munga, Dr. Abednego Keshomshahara, Blaston Gavile na Dr. Alex Malasusa (ambaye amewahi kuongoza KKKT katika cheo hicho kwa miaka 8).

Dkt. Shoo amepata kura 144 huku mshindani wake wa karibu, Dkt. Keshomshahara akipata kura 74 kati ya kura 218 zilizopigwa (katika mzunguko wa mwisho baada ya kubaki wawili).
Kuna kibwengu kinaitwa sexless kutoka Lumumba kilitaman show apiģwe chini sijui kimejificha wp na boss wake shetan
 
Sipendi kabisa watu kumuhusisha Askofu wetu na Siasa.Daktari Shoo anasimama kwenye haki akiona zinakanyagwa na si anaibuka tu.Hajaonyesha mapenzi yake waziwazi kwa upande wowote.Niishie kwa kusema Hongera Dr.Shoo kwa kupewa kibali tena na Mungu
Haki zinapokanyagwa na watu fulani ndo anaibuka. Lakini zikikanyagwa na wengine hatumsikii. Hana tofauti na kina Ole Ngurumo, full double standards.
 
Mmh...kashinda??

kanisani kuna mashindano?

Kweli zama za mwisho zmekaribia.
Demokrasia. KKKT ni mfano bora kabisa, kwakuwa Mungu hawezi kututumia barua kuwa Fulani awe Askofu mkuu basi wajumbe wa mkutano mkuu acha wamchague miongoni mwa wale wakiopendekezwa nafasi hiyo.
KKKT ina demokrasi kuliko hata chama cha siasa kama CCM ambao eti wanapeleka jina moja kulipitisha na kusema kapita kwa 100%. Uongo mtupu!
 
Mulifurahi na kupiga vigelegele trump aliposhinda uchaguzi mkiamini chadema itakuwa kama......
Mkafurah na kupiga vigelegele kenyatta aliposhinda uchaguzi mkiamini mtakuwa kama.....
Leo mmeamia kwa shoo, hebu jipeni space maana mwisho wa siku huwa mnabaki yatima
Bila kuitaja Chadema mak....o yako yanawashwawashwa.
 
Malasusa amesahau nini tena? Ameongoza miiaka 8, leo anataka kurudi tena? Aache kumchezea Mungu.
Ni mtumwa wa jiwe huyo! Hapo kaambiwa ajaribu zali tena, bahati mbaya KKKT sii wale kina Kakobe au Mzee wa upako ambao bila woga kabisa nasema ni wajasiriamali wa Injili. Na hapo ukifuatilia kwa kina Makonda katumika kwenye dili hilo ambalo lime dunda
 
Back
Top Bottom