Erythrocyte
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 117,571
- 217,926
Dkt. Frederick Onael Shoo ametangazwa mshindi usiku huu dhidi ya wagombea wengine na ataongoza Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) kwa kipindi cha miaka minne.
Alikuwa akichuana na Maaskofu wenzake akiwemo Dr. Steven Munga, Dr. Abednego Keshomshahara, Blaston Gavile na Dr. Alex Malasusa (ambaye amewahi kuongoza KKKT katika cheo hicho kwa miaka 8).
Dkt. Shoo amepata kura 144 huku mshindani wake wa karibu, Dkt. Keshomshahara akipata kura 74 kati ya kura 218 zilizopigwa (katika mzunguko wa mwisho baada ya kubaki wawili).
Dkt. Shoo alichaguliwa kwa mara ya kwanza kuongoza Kanisa hilo Agosti mwaka 2015 baada ya kupata kura 153, dhidi ya Dkt. Munga aliyepata kura 67 wakati huo
=====
Arusha. Dk Frederick Shoo amechaguliwa tena kuwa mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) baada ya kupata kura 144 dhidi ya 74 za mpinzani wake.
Kwa ushindi huo, Dk Shoo anaendelea kuliongoza kanisa hilo kwa miaka mingine minne na kufuata nyayo za wakuu wa kanisa hilo waliomtangulia walioliongoza kwa vipindi viwili vya miaka minne.
Ametangazwa kuwa mshindi usiku wa kuamkia leo Jumamosi Agosti 24, 2019 baada ya kumalizika kwa uchaguzi uliofanyika mjini Arusha na kutawaliwa na kila aina ya upinzani.
Alipata kura 144 kati ya 218 huku mpinzani wake Askofu Abednego Keshamshahara wa Dayosisi ya Kaskazini Magharibi akipata kura 74.
Chanzo: Mwananchi