Askofu Emmaus: Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam asiligawe Taifa katika kipindi hiki!

DAGAA WA MWANZA

Senior Member
Jan 27, 2019
169
464
Viongozi Wakuu wa Nchi wametoa matamko ya kusitisha mikutano na mikusanyiko isiyokuwa ya lazima ikiwemo mikutano ya kisiasa ili kujihami na maambukizi mapya ya corona. Waziri Mkuu amekwenda hatua zaidi mbele kwa kutaja viongozi watakaohusika kutoa taarifa kuhusiana na ugonjwa wa corona! Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam hayumo katika orodha iliyotolewa na Waziri Mkuu.

Leo kuna video inasambaa mitandaoni ikimuonyesha Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam akifanya mkutano wenye mkusanyiko mkubwa wa watu jijini Dar es Salaam. Mkuu wa Mkoa hajaishia hapo, ameendelea kuutangazia umma kuhusu ni nani mwingine anaumwa corona. Hakuishia hapo, anaendelea kufanya siasa kwa lengo la kukejeli maamuzi ya Mwenyekiti wa CHADEMA ya kusitisha mikutano ya kisiasa kwa chama hicho kwa ajili ya kujihami na maambukizi ya corona!

Huko nyuma niliwahi kutoa tahadhari kuwa janga la corona lisitumike kama fursa ya kukandamizana. Kwa nafasi yake, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam ni mtu mwenye madaraka makubwa sana katika nchi hii! Inawezekana nafasi yake inaweza kumfanya asitambue kuwa alichokifanya amewakosea wananchi. Inawezekana pia washauri wake wasione kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam amefanya jambo ambalo halikustahili kufanyika katika kipindi hiki. Inawezekana pia mamlaka yake ya uteuzi isione kuwa alichokifanya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam hakikupaswa! Kwa sababu hiyo, huenda yeye mwenyewe asione haja ya kuomba msamaha na wala asione haja ya kufikiria kutokurudia tena kufanya hayo anayofanya.

Lakini mimi kama Askofu, ninamshauri Mkuu wa Mkoa wa Dar as Salaam kuona haja ya kuwaomba msamaha Watanzania ili aendelee kuwa na amani katika moyo wake na nafsi yake. Pia, ninawaomba wale waliokwazika na yale aliyofanya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam wamsamehe ili waendelee kuelekeza nguvu zao katika kujihami na maambukizi mapya ya corona.

Hiki ni kipindi kinachohitaji mshikamano kama Taifa. Tusiruhusu migawanyiko katika mapambano dhidi ya corona kwa kuwa ufalme uliogawanyika hauwezi kusimama (Mathayo 12:25). Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam anaweza (kama ataamua) kuisitiri Serikali yetu (kama ina mapungufu) kwa kutokupinga hadharani kwa vitendo maamuzi ya kusitisha mikutano pamoja na taratibu za kutoa taarifa kuhusu ugonjwa wa corona.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam pamoja na washauri wake wanapaswa kujua kuwa katika vita au mpambano ya kimaadili (just war or moral struggles), wapiganaji au wapambanaji hawaruhusiwi kumshambulia mtu au adui aliyesalimu amri au aliyejisalimisha. Mwenyekiti wa CHADEMA na Chama chake wameunga mkono tamko la Serikali na wameamua kusitisha mikutano ya kisiasa kwa Chama chao katika nchi nzima. Hivyo, hakukuwa na haja kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam kuitisha mkutano kwa lengo la kumshambulia kiongozi aliyeamua kuunga mkono juhudi za Serikali katika kipindi ambacho Serikali inahitaji uungwaji mkono wa hali ya juu na kila raia.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam pamoja na washauri wake wanaweza wasiufurahie sana ujumbe huu, lakini ulikuwa hauna budi kutolewa na Askofu (Ezekieli 33:1-20). Ninawasihi wausome ujumbe katika hali ya unyenyekevu. Wakishaulewa waingie katika toba na tafakuri namna ya kusonga mbele badala ya kuanza kulaumiana.

Tunasisitiza tena! Hiki siyo kipindi cha viongozi kusimama katika mikutano ya hadhara kwa lengo la kuwashambulia viongozi wengine wanaounga mkono jitihada za Serikali katika kupambana na maambukizi ya corona. Hata kama watajitokeza wanaopinga, wanatakiwa washawishiwe kwa hoja na elimu badala ya kejeli na vitisho! Tusiibue vita isiyo na sababu!

Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfuate!

Askofu Mkuu Emmaus Bandekile Mwamakula - Mkuu wa Kanisa la Moravian la Uamsho Tanzania & Afrika Mashariki na Mwenyekiti Mwenza wa Umoja wa Makanisa ya Moravian ya Uamsho Duniani

Bandiko langu > Makonda ni mpuuzi kama wapuuzi wengine tu na hatupaswi kumpuuza kwa upuuzi wake hata kama anatumwa
 
Uwezo wake wa kufikiri upo chini sana. Nafikiri ameathirika na malezi/lishe duni aliyokulia alipokuwa mtoto.
Umasikini ni mbaya sana kizaizai. Napenda niwaase wana JF wenzangu,tuupige vita kwa nguvu zetu zote umasikini,ila vita iwe halali,ili vizazi vyetu vije kutoishi katika umasikini kwani athari zake ni kubwa na mbaya sana.
Mfano halisi wa athari mbaya za umasikini ni Albert Bashite.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Well said mtumishi wa Mungu. Asipokuelewa akakaza shingo itakatika tu kwa hakika!
Nikuombe tu kwa heshima, mh. Rais asilifumbie macho hili suala la mteule wake kwani linakwenda kumpunguzia kura mbeleni! Alifanyie kazi hata Kama atatoa kauli ya kukemea itatosha sana. Mungu akakubariki na kukujaza hekima na busara zaidi.
 
DAGAA WA MWANZA,
Hakuna Askofu wa uamsho Moravian Tanzania. Na Moravian hakuna kitu kinachoitwa uamsho labda kwenye Kanisa la Moravian la Baba ako.

Acheni Tabia ya kulitumia Kanisa letu la Moravian kwenye siasa zenu za kipuuzi. Na ushabiki wenu umejikita kutumia taasisi za Kidini au mnadhani sisi waumini hatutafakari mnachokiongea na kutafakari lengo lenu la kuongea.

Nilifundisha Kidogo Kwa Muda Chuo Kikuu cha Teofilo Kisanji-Mbeya, nilikutana na Vichwa vyenye uelewa wa Juu kwenye Malezi ya Kiroho. Hawana Tabia za Kipuuzi na ni Watiifu kwa Serikali na hawajawahi kuikosea wale kuhoji wazi utendaji wake.

Ila Wanautaratibu wa kushauri Serikali kwenye masuala muhimu ila Siyo kwenye Majukwaa ya kisiasa na kijamii.

Ukitaka ujue ugolo ulioandikwa nitafutie ushauri aliouandika ukielezea kuichallenge kauli ya Mbowe ikilazimisha kuanza mikutano ya hadhara nchi nzima wakati Duniani kote wanahaha juu Covid-19.

Jamani tuache siasa kwenye dini, hata Shetani yalimshinda huko Mbinguni na akatupwa Duniani na sasa yupo kuzimu.
 
Well said mtumishi wa Mungu. Asipokuelewa akakaza shingo itakatika tu kwa hakika!
Nikuombe tu kwa heshima, mh. Rais asilifumbie macho hili suala la mteule wake kwani linakwenda kumpunguzia kura mbeleni! Alifanyie kazi hata Kama atatoa kauli ya kukemea itatosha sana. Mungu akakubariki na kukujaza hekima na busara zaidi.
Hakuna mtumishi wa Mungu hapa, ni Mtumishi wa Mbowe
 
Usishangae Kesho anawaita baadhi ya watumishi njaa anawapa bahasha wanatoa tamko la kumkana alietoa tamko. Makonda anatumwa na anaemtuma anajulikana.
Yawezekana safari hii hajamtuma ila Makonda ni mtu mwenye kiherehere sana. Anapenda kujitafutia umaarufu mbele ya Mfalme.

Hapa sasa utapata picha ni nani aliyetoa maagizo kwa Jeshi la Magereza pamoja na Polisi kuwashambulia Viongozi wa Chadema. Ndiyo maana anaweweseka. Ila siku zake za kuwa na kiburi zinahesabika.

Taifa kama Marekani kumkataa haikuwa bahati mbaya bali wameshamjua ni wa namna gani.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa ujumla nchi imepoteza Utawala bora kwani Waziri Mkuu kesha toa maelekezo inakuwaje yanatokea haya?
 
Baba Askofu, hizo ni dalili za Laana maana huanza taratiibu........
 
Back
Top Bottom