Askofu Emaus Mwamakula akamatwa na Polisi kwa kuhamasisha Maandamano ya kudai Katiba Mpya

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
82,123
2,000
FB_IMG_1613395626412.jpgInstagram media - CLUDuxYp2nG ( 640 X 640 ).jpg


====

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
KUKAMATWA KWA ASKOFU EMMAUS BANDEKILE MWAMAKULA
KWA KOSA LA KUHAMASISHA MAANDAMANO HARAMU

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Polisi Dar es Salaam leo tarehe 15.02.2021 limefanikiwa kumkamata anayejiita Askofu EMMAUS BANDEKILE MWAMAKULA wa kanisa la Uamsho la Moravian kwa kosa la kuhamasisha maandamano nchi nzima kwa njia ya ujumbe wa maneno katika mitandao ya kijamii. Taarifa ilikuwa ikihamasisha wananchi wajitokeze kwa wingi ili kuandamana wakishinikiza na kudai katiba mpya jambo ambalo ni kinyume na taratibu na sheria za nchi.

Aidha awali Jeshi la Polisi kupitia idara ya upelelezi kanda Maalum Dar es salaam walifanikiwa kupata taarifa hiyo na kumkamata Askofu huyo kwa ajili mahojiano kwa jambo hilo ambalo lilileta taharuki kwa umma katika mitandao ya kijamii.

Jeshi la Polisi linatoa onyo kwa yeyote ambaye ameshawishika na kupanga kuandamana kuahirisha mara moja nia hiyo ovu ambayo iko kinyume na sheria.

Pia ifahamike ni kosa kufanya maandamano bila kuwa na kibali cha Polisi ili kupewa ulinzi, na atakayejaribu kuandamana atashughulikiwa kwa mujibu wa sheria. Hivyo wananchi wote wa jiji la Dar es salaam waendelee na shughuli zao za kukuza uchumi na kujipatia vipato vyao vya kila siku.


LAZARO B. MAMBOSASA– SACP
KAMANDA WA POLISI KANDA MAALUM
DAR ES SALAM.
15.02.2021

Zaidi, soma:

 

Grahams

JF-Expert Member
Mar 19, 2016
1,673
2,000
Huyu Askofu ndiyo ali organize matembezi ya hiyari kudai Katiba mpya?

Nadhani angejikita kwenye kuchunga kondoo wa bwana tu, utawala uliopo huwa haupendi kufosiwa kufanya mambo. Mambo yanafanyika pale mwenye nyumba atakapoamua.

Hata kama aliwahaidi Katiba mpya -mpaka apende mwenyewe.

Milioni 50 kila Kijiji - mpaka apende

Nyongeza ya mishahara - mpaka apende

You mention...
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom