Askofu Dr Stephen Munga amuonya Kadinali Pengo: Kunyamaza wakati mwingine ni hekima

Askofu Dr Stephen Munga amuonya Kadinali Pengo

KUNYAMAZA WAKATI MWINGINE NI HEKIMA

Waungwana taifa la Mungu, someni hii kwa furaha na uvumilivu.

"Ikawa, Sauli aliporudi baada ya kuwafuatia Wafilisti, aliambiwa ya kwamba, Daudi yuko katika nyika ya Engedi. Ndipo Sauli akatwaa watu elfu waliochaguliwa katika Israeli wote, akaenda kumtafuta Daudi na watu wake juu ya majabali ya mbuzi-mwitu.

Akafika penye mazizi ya kondoo kando ya njia, na huko kulikuwa na pango; Sauli akaingia ndani ili kwenda haja. Na Daudi na watu wake walikuwa wakikaa mle pangoni ndani sana. Nao watu wa Daudi wakamwambia, Tazama, hii ndiyo siku ile aliyokuambia BWANA, Angalia, nitamtia adui yako mikononi mwako, nawe utamtenda yoyote utakayoona kuwa mema. Basi Daudi akainuka, akaukata upindo wa vazi lake Sauli kwa siri. Lakini baadaye, moyo wake Daudi ukamchoma, kwa sababu amekata upindo wa vazi lake Sauli.

Akawaambia watu wake, Hasha! Nisimtendee bwana wangu, masihi wa BWANA, neno hili, kuunyosha mkono wangu juu yake, kwa maana yeye ni masihi wa BWANA. Basi Daudi akawazuia watu wake kwa maneno hayo, asiwaruhusu kumshambulia Sauli. Kisha Sauli akatoka pangoni, akaenda zake.

Daudi naye akainuka baadaye, akatoka pangoni, akamwita Sauli, akisema, Bwana wangu, mfalme. Na Sauli alipotazama nyuma, Daudi akainama uso wake hadi chini, akamsujudia."
(1 Samweli 24:1-8).

Nimeleta maneno haya kutoka biblia ili niseme jambo muhimu kwa wakati wetu. Natumia maneno haya baada ya kusikiliza mazungumzo ya baadhi ya viongozi wa kiimani katika mkutano wao na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam. Ni baada ya kupokeo vipande vya video ( video clips) na kuvisikiliza pia mitandaoni.

Kama kawaida nilishikika na majukumu kwa hiyo sikuweza kufuatilia mkutano huo kwa karibu na hivyo nisemalo hapa si juu ya mkutano mzima bali ni juu ya "clips" nilizosikiliza. Nimemsikiliza kwa makini na kwa maoni yangu wenzetu walizungumza kupitiliza (they overstated matters). Ni mitazamo yao na kamwe sio mitazamo ya viongozi wote wa kiimani. Hata hivyo, niliyosikia yanasaliti ukweli wa mambo kama nitakavyoeleza.

Awali ya yote niweke wazi kwamba mashaka katika mazungumzo niliyoyasikiliza sio ya ama Mhe. Magufuli, Rais wetu au Comrade Makonda, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam. Shida ni waliozungumza kwa kujipendekeza na kupendezesha kwa maslahi binafsi. Najaribu kuwa mwaminifu katika hoja hii.

Nijieleze kidogo hapa. Niseme wazi kwamba kisera mimi nilikuwa mfuasi wa CCM. Uchungaji na Uaskofu ndivyo vimeninyang'anya haki hiyo. Nimemwita Mhe. Makonda Comrade kwa sababu mimi nilikuwa CCM mpaka nilipowekwa wakfu kuwa Mchungaji. Mimi nilikuwa ile CCM ya Mwalimu. Hata hivyo, baada ya hapo na hata kuwekwa wakfu kuwa Askofu nilishirikiana na makomredi Marais na Makatibu Wakuu na Makatibu wa CCM mkoani na wilayani kwangu.

Nilifanya hivyo kwa sababu katiba na sera za CCM zilisimama katika misingi ya haki na kuheshimu utu wa mtu. Zaidi ya yote ni CCM iliyoongoza mchakato wa utawala wa kidemokrasia na hivyo kufungua milango ya siasa za ushindani kwa kuruhusu kuanzishwa kwa vyama vingine vya siasa. Nakiri wazi kwamba nimekuwa karibu na viongozi wa juu wa CCM kwa muda mrefu na Comrade Makamba na Kinana ( schoolmate) ni mashahidi.

CCM imefanya mazuri mengi na makosa mengi katika nyakati tofauti lakini mtazamo wake wa nia ya kujisahihisha iliyorithi tangu Baba wa Taifa ndiyo uhai wake ulioleta matumaini. Kwa hiyo CCM ndiyo iliyozaa demokrasia ya vyama vingi.

Tena tukumbuke kwamba wakati ule kura za kukubali demokrasia ya vyama vingi hazikutosha lakini CCM ikachukua maamuzi magumu ya kuruhusu demokrasia ya vyama vingi vya siasa. Inakuwaje leo CCM inakula mtoto iliyomzaa kwa kukandamiza demokrasia?!

Someni vizuri "postings" zangu. Sijawahi kumsema neno lolote Mhe. Magufuli. Mimi ni nani hata nimseme mpakwa mafuta wa Bwana?! Mhe. Magufuli ni mtawala wa nchi ya Tanzania. Kwangu mimi yeye ni mpakwa mafuta wa Bwana.

Anafanya mazuri na anafanya makosa lakini hukumu yake imo mikononi mwa Mungu. Watanzania fahamuni kwamba alipoapishwa Mhe JPM mlimuweka mkononi mwa Mungu na kwamba Mungu ahukumu juu ya mambo yake. Nimejizuia sana kutosema neno juu ya Mhe. JPM hadharani kwa sababu ni mpakwa mafuta wa Bwana.

LAKINI LIKIWEPO NENO LA MOJA KWA MOJA LA KUMWAMBIA TOKA KWA BWANA NITAFANYA HIVYO NA KAMWE HAKUNA WA KUNIZUIA. Ila hapa namhoji Muadhama Pengo katika mkutano ulioitishwa na komredi Makonda, je, uliyoyasema na kuyatukuza yametoka kwa BWANA?!

Sasa nirudi kwenye somo. Wenzangu viongozi wa kiimani mliohudhuria mkutano ulioitishwa na Komredi Makonda na kupewa nafasi ya kuongea, kwa kweli mlijipendezesha. Sijui huko kwenu kiapo cha kichungaji kikoje. Huku kwetu kiapo hicho kinamdai Mchungaji aseme kweli hata kama amekaa mezani, akila chakula na Kaisari, kilichoandaliwa na Kaisari, lakini amwambie Kaisari mambo yake kwa kweli yote.

Huu ni mfano wa Yohana Mbatizaji aliyekaa chakulani na Herode, akila chakula cha Herode, lakini akimwambia Herode maovu yake. Yohana alimwambia Herode kwamba Herodia mke wake, si mke wake kihalali bali alitumia mamlaka yake kumnyang'anya Filipo (ndugu yake) mke wake. Kwa maneno mengine Herode alitumia vibaya mamlaka aliyopewa na Mungu kuwadhalimu mpaka ndugu zake. Ilimgharimu Yohana maisha yake lakini alitimiza utume wake.

Ndugu zangu viongozi wa kiimani, akiwemo mtumishi niliyemheshimu sana, Muadhama Pengo, mmesema kwa kusifu kulikopitiliza mipaka (you overstated the matters you stated). Tanzania ilikuwepo kabla ya Mhe. Magufuli na itakuwepo baada yake. Tanzania sio mali ya mtu awaye yeyote bali ni mali ya Mungu mwumbaji wa mbingu na nchi. Muadhama Pengo umetoa kauli tata zinazoweka utukufu kwa wanadamu na si kwa Mungu.

Wengine waliozungumza naweza kuwapuuzia mbali lakini wewe kutamka maneno yale sikutegemea! Mkumbuke Yesu Kristo aliyeungama maungamo mazuri mbele ya Pilato pasipo kuyumba. Huyu Kristo hakumpendezesha Pilato ili ahurumiwe na kupendelewa. Mtasimamaje mbele zake Kristo siku ya hukumu?! Kwa machozi baada ya kukusikiliza namwachia Bwana Yesu ahukumu juu yako.

Mimi kamwe sitasema neno lolote la hukumu. Wewe ni mtumishi na wakili wa siri za Mungu sina neno la kusema juu yako bali namwachia Kristo aliyekuita wewe na mimi katika utume huu. Wakati mwingine ni heri kunyamaza kuliko kusema na kupitiliza hata kukufuru.

Muadhama Pengo nitaendelea kukuheshimu kwa namna ile Daudi alivyomheshimu Sauli. Daudi alikuwa na nafasi ya kumuua Sauli lakini alitambua mipaka ya uwezo wake. Mimi sitakuhukumu na wala sitakujakaa nimhukumu Mheshiwa sana JPM kwa sababu najua dhahiri kwamba ni Mungu atakayemhukumu kwa mambo yote yanayotokea katika taifa hili la Mungu.

Nafanya hivyo kwa kukumbushwa na Daudi akiwa katika hali ngumu ya kuwindwa na Sauli aliyetaka kumuua Daudi. Lakini Daudi akawaonya watu wake akisema:

"Hasha! Nisimtendee bwana wangu, masihi wa BWANA, neno hili, kuunyosha mkono wangu juu yake, kwa maana yeye ni masihi wa BWANA. Basi Daudi akawazuia watu wake kwa maneno hayo, asiwaruhusu kumshambulia Sauli."

Nitaendelea kumheshime Rais wangu JPM na sina kibali cha kumhukumu lakini CCM inakandamiza vyama vya upinzani na yeye kama Mwenyekiti wa CCM arejee maamuzi ya CCM kuruhusu demokrasia ya vyama vingi vya siasa. Akisha kufanya hivyo aangalie faulu zilizofanyika katika mchakato wa uchaguzi wa serikali za mitaa.

Anapoyafanya hayo, yeye kama muumini wa kanisa katoliki aongee na Mungu aliyempa kibali kutawala nchi hii na kuona kama ametenda haki. Mungu ndiye atakayehukumu lakini kwa haya niliyoyasema damu yake haitadaiwa mikononi mwangu. Hapa nasimama, Mungu nisaidie.

+Askofu Stephen Munga
KKKT
Pengo ni mzigo kwa kanisa katoliki amezeeka apumzike kwa heshima analiaibisha kanisa na kulishushia heshima kiukweli sitashangaa kuona kanisa katoliki Tanzania linaanguka unless kanisa limdhibiti pengo kwa namna njema iwayo kwa maslahi ya jumuia ya kristo na heshima ya kanisa pengo awe muted for ever!!
 
Askofu Pengo ameshapoteza dira na mwelekeo, mi nikisia leo askofu Pengo atasoma misa pale UDSM mi nakula kona kwenda kanisa la Msewe!
 
Kwa hyo na yy hana hekima? Maana huwa anasema sema kila siku... Au yy akitoa maoni ni sawa ,wenzie ndio hukosea???
 
Kuakaa kimya wakati mwengine ni hrkima
HUYU MUNGA ANATABIA MBAYA
WENZAO WATUWAZIMA WA HESHIMA WANAANDIKIANA BARUA AU HT KUALIKANA VYAKULA WANAAMBIANA UKWELI YANAISHA
MAASKOFU WANAKOSOANA MITANDAONI
MUNGA anatuketea mambo ya juma lokole huyu
Huwezi kumuheshimu mtu afu unamkosoa mtandaoni
Mfate offsini kwake km unayosema ni kweli
 
Mwenzenu katumwa asafishe njia kwa waumini, 3/4 ya wakristo wote Tanzania ni RC. kila mkoa/wilaya wapo
 
Askofu Munga amepoteza mwelekeo

sasa Hajui ashike lipi kati ya dini na siasa
Nakuona kama mtu aliyekalilishwa maneno juu ya watumishi wa Jehovah na mambo ya kisiasa.
Soma maandiko na Roho mtakatifu akusaidie kuelewa. KWA UFUPI MTUMISHI NA UTUMISHI WA JEHOVA NI ZAIDI YA SIASA. SIASA NI SEHEMU YA MAMBO YA HUDUMA YAKE ANAYOPASWA KUSHUGHURIKIA ILI KUSUDI LA JEHOVA JUU YA WANADAMU LITIMILIKE. HIVYO HAIWEZEKANI KUTENGANISHWA ISIPOKUWA KWA YULE ASIYEELEWA KWA NINI JEHOVA ALIMUITA.
Mfano Nabii Eliya alimkabiri batabara Mfalme Ahabu 1wafalme 18:17-46,
NABII MIKAYA PEKEE KATI YA MANABII ZAIDI YA MIA NNE WAKATI WOTE ALIMWAMBIA MFALME AHABU UKWELI HATAKAMA ULIMUUMIZA MFALME, MFALME HAKUMPENDA, MANABII WENGINE WOTE MIA NNE WALIKUWA WAKIMSIFU MFALME NA KUKUBALIANA NA KILA ALILOLIAMUA NA KULIFANYA ISIPOKUWA NABII MIKAYA PEKEE soma 2mambo ya Nyakati 18:1- 34, 1Falm 18, maamzi na matendo ya Mfalme yalilitesa taifa ingawa manabii mia nne waliumga mkono mambo hayo.
Yohana mbatizaji hakukubaliana na upotovu wa Mfalme Herode.

Tanzania Leo tunao watumishi (wanaojiita) zaidi ya mia NNE NI wangapi wanaosimama kama NABII MIKAYA, Eliya na Yohana nawaona Askofu Bagonza na Askifu Muga, wengine wakowapi?????? Je, hawapo katka kundi la manabii mia NNE kama wale wa kipindi cha Mfalme Ahabu , ??? Je sio hao tunawaona wakila na kunywa na Mfalme kisha kutoka nje na kupongeza uovu wa Mfalme wetu Leo????

YUKO WAPI NABII ELYA AU NABII MIKAYA WA LEO WA KUMKABILI MFALME AHABU WA LEO ????
Askifu Bagonza , Askifu Muga mmebakia ninyi tu kwa sasa, TUKO WENGI TUNAWAOMBEA AZIDISHE UJASIRI NDANI YENU KUISEMA KWELI YAKE KWA AJILI YA TAIFA LETU TANZANIA.

Wanaofanana nanyi wamechagua upande wa manabii mia NNE , msihofu, NABII ELIYA NA HATA NABII MIKAYA kwa nyakati zao kila mmoja aliachwa peke yake ila Jehovah alikuwa upande wao nao waliliponya Taifa lao nanyi mtaliponya Taifa letu kwani JEHOVA yule yule yu upande wenu.
 
Hujasoma hata post yenyewe umeshacomment, huu ni umbumbumbu wa hali ya juu sana. Hata hivyo sina mashaka kuwa msimu wako utapita kama wengine pia walivyopita
 
Askofu Dr Stephen Munga amuonya Kadinali Pengo

KUNYAMAZA WAKATI MWINGINE NI HEKIMA

Waungwana taifa la Mungu, someni hii kwa furaha na uvumilivu.

"Ikawa, Sauli aliporudi baada ya kuwafuatia Wafilisti, aliambiwa ya kwamba, Daudi yuko katika nyika ya Engedi. Ndipo Sauli akatwaa watu elfu waliochaguliwa katika Israeli wote, akaenda kumtafuta Daudi na watu wake juu ya majabali ya mbuzi-mwitu.

Akafika penye mazizi ya kondoo kando ya njia, na huko kulikuwa na pango; Sauli akaingia ndani ili kwenda haja. Na Daudi na watu wake walikuwa wakikaa mle pangoni ndani sana. Nao watu wa Daudi wakamwambia, Tazama, hii ndiyo siku ile aliyokuambia BWANA, Angalia, nitamtia adui yako mikononi mwako, nawe utamtenda yoyote utakayoona kuwa mema. Basi Daudi akainuka, akaukata upindo wa vazi lake Sauli kwa siri. Lakini baadaye, moyo wake Daudi ukamchoma, kwa sababu amekata upindo wa vazi lake Sauli.

Akawaambia watu wake, Hasha! Nisimtendee bwana wangu, masihi wa BWANA, neno hili, kuunyosha mkono wangu juu yake, kwa maana yeye ni masihi wa BWANA. Basi Daudi akawazuia watu wake kwa maneno hayo, asiwaruhusu kumshambulia Sauli. Kisha Sauli akatoka pangoni, akaenda zake.

Daudi naye akainuka baadaye, akatoka pangoni, akamwita Sauli, akisema, Bwana wangu, mfalme. Na Sauli alipotazama nyuma, Daudi akainama uso wake hadi chini, akamsujudia."
(1 Samweli 24:1-8).

Nimeleta maneno haya kutoka biblia ili niseme jambo muhimu kwa wakati wetu. Natumia maneno haya baada ya kusikiliza mazungumzo ya baadhi ya viongozi wa kiimani katika mkutano wao na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam. Ni baada ya kupokeo vipande vya video ( video clips) na kuvisikiliza pia mitandaoni.

Kama kawaida nilishikika na majukumu kwa hiyo sikuweza kufuatilia mkutano huo kwa karibu na hivyo nisemalo hapa si juu ya mkutano mzima bali ni juu ya "clips" nilizosikiliza. Nimemsikiliza kwa makini na kwa maoni yangu wenzetu walizungumza kupitiliza (they overstated matters). Ni mitazamo yao na kamwe sio mitazamo ya viongozi wote wa kiimani. Hata hivyo, niliyosikia yanasaliti ukweli wa mambo kama nitakavyoeleza.

Awali ya yote niweke wazi kwamba mashaka katika mazungumzo niliyoyasikiliza sio ya ama Mhe. Magufuli, Rais wetu au Comrade Makonda, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam. Shida ni waliozungumza kwa kujipendekeza na kupendezesha kwa maslahi binafsi. Najaribu kuwa mwaminifu katika hoja hii.

Nijieleze kidogo hapa. Niseme wazi kwamba kisera mimi nilikuwa mfuasi wa CCM. Uchungaji na Uaskofu ndivyo vimeninyang'anya haki hiyo. Nimemwita Mhe. Makonda Comrade kwa sababu mimi nilikuwa CCM mpaka nilipowekwa wakfu kuwa Mchungaji. Mimi nilikuwa ile CCM ya Mwalimu. Hata hivyo, baada ya hapo na hata kuwekwa wakfu kuwa Askofu nilishirikiana na makomredi Marais na Makatibu Wakuu na Makatibu wa CCM mkoani na wilayani kwangu.

Nilifanya hivyo kwa sababu katiba na sera za CCM zilisimama katika misingi ya haki na kuheshimu utu wa mtu. Zaidi ya yote ni CCM iliyoongoza mchakato wa utawala wa kidemokrasia na hivyo kufungua milango ya siasa za ushindani kwa kuruhusu kuanzishwa kwa vyama vingine vya siasa. Nakiri wazi kwamba nimekuwa karibu na viongozi wa juu wa CCM kwa muda mrefu na Comrade Makamba na Kinana ( schoolmate) ni mashahidi.

CCM imefanya mazuri mengi na makosa mengi katika nyakati tofauti lakini mtazamo wake wa nia ya kujisahihisha iliyorithi tangu Baba wa Taifa ndiyo uhai wake ulioleta matumaini. Kwa hiyo CCM ndiyo iliyozaa demokrasia ya vyama vingi.

Tena tukumbuke kwamba wakati ule kura za kukubali demokrasia ya vyama vingi hazikutosha lakini CCM ikachukua maamuzi magumu ya kuruhusu demokrasia ya vyama vingi vya siasa. Inakuwaje leo CCM inakula mtoto iliyomzaa kwa kukandamiza demokrasia?!

Someni vizuri "postings" zangu. Sijawahi kumsema neno lolote Mhe. Magufuli. Mimi ni nani hata nimseme mpakwa mafuta wa Bwana?! Mhe. Magufuli ni mtawala wa nchi ya Tanzania. Kwangu mimi yeye ni mpakwa mafuta wa Bwana.

Anafanya mazuri na anafanya makosa lakini hukumu yake imo mikononi mwa Mungu. Watanzania fahamuni kwamba alipoapishwa Mhe JPM mlimuweka mkononi mwa Mungu na kwamba Mungu ahukumu juu ya mambo yake. Nimejizuia sana kutosema neno juu ya Mhe. JPM hadharani kwa sababu ni mpakwa mafuta wa Bwana.

LAKINI LIKIWEPO NENO LA MOJA KWA MOJA LA KUMWAMBIA TOKA KWA BWANA NITAFANYA HIVYO NA KAMWE HAKUNA WA KUNIZUIA. Ila hapa namhoji Muadhama Pengo katika mkutano ulioitishwa na komredi Makonda, je, uliyoyasema na kuyatukuza yametoka kwa BWANA?!

Sasa nirudi kwenye somo. Wenzangu viongozi wa kiimani mliohudhuria mkutano ulioitishwa na Komredi Makonda na kupewa nafasi ya kuongea, kwa kweli mlijipendezesha. Sijui huko kwenu kiapo cha kichungaji kikoje. Huku kwetu kiapo hicho kinamdai Mchungaji aseme kweli hata kama amekaa mezani, akila chakula na Kaisari, kilichoandaliwa na Kaisari, lakini amwambie Kaisari mambo yake kwa kweli yote.

Huu ni mfano wa Yohana Mbatizaji aliyekaa chakulani na Herode, akila chakula cha Herode, lakini akimwambia Herode maovu yake. Yohana alimwambia Herode kwamba Herodia mke wake, si mke wake kihalali bali alitumia mamlaka yake kumnyang'anya Filipo (ndugu yake) mke wake. Kwa maneno mengine Herode alitumia vibaya mamlaka aliyopewa na Mungu kuwadhalimu mpaka ndugu zake. Ilimgharimu Yohana maisha yake lakini alitimiza utume wake.

Ndugu zangu viongozi wa kiimani, akiwemo mtumishi niliyemheshimu sana, Muadhama Pengo, mmesema kwa kusifu kulikopitiliza mipaka (you overstated the matters you stated). Tanzania ilikuwepo kabla ya Mhe. Magufuli na itakuwepo baada yake. Tanzania sio mali ya mtu awaye yeyote bali ni mali ya Mungu mwumbaji wa mbingu na nchi. Muadhama Pengo umetoa kauli tata zinazoweka utukufu kwa wanadamu na si kwa Mungu.

Wengine waliozungumza naweza kuwapuuzia mbali lakini wewe kutamka maneno yale sikutegemea! Mkumbuke Yesu Kristo aliyeungama maungamo mazuri mbele ya Pilato pasipo kuyumba. Huyu Kristo hakumpendezesha Pilato ili ahurumiwe na kupendelewa. Mtasimamaje mbele zake Kristo siku ya hukumu?! Kwa machozi baada ya kukusikiliza namwachia Bwana Yesu ahukumu juu yako.

Mimi kamwe sitasema neno lolote la hukumu. Wewe ni mtumishi na wakili wa siri za Mungu sina neno la kusema juu yako bali namwachia Kristo aliyekuita wewe na mimi katika utume huu. Wakati mwingine ni heri kunyamaza kuliko kusema na kupitiliza hata kukufuru.

Muadhama Pengo nitaendelea kukuheshimu kwa namna ile Daudi alivyomheshimu Sauli. Daudi alikuwa na nafasi ya kumuua Sauli lakini alitambua mipaka ya uwezo wake. Mimi sitakuhukumu na wala sitakujakaa nimhukumu Mheshiwa sana JPM kwa sababu najua dhahiri kwamba ni Mungu atakayemhukumu kwa mambo yote yanayotokea katika taifa hili la Mungu.

Nafanya hivyo kwa kukumbushwa na Daudi akiwa katika hali ngumu ya kuwindwa na Sauli aliyetaka kumuua Daudi. Lakini Daudi akawaonya watu wake akisema:

"Hasha! Nisimtendee bwana wangu, masihi wa BWANA, neno hili, kuunyosha mkono wangu juu yake, kwa maana yeye ni masihi wa BWANA. Basi Daudi akawazuia watu wake kwa maneno hayo, asiwaruhusu kumshambulia Sauli."

Nitaendelea kumheshime Rais wangu JPM na sina kibali cha kumhukumu lakini CCM inakandamiza vyama vya upinzani na yeye kama Mwenyekiti wa CCM arejee maamuzi ya CCM kuruhusu demokrasia ya vyama vingi vya siasa. Akisha kufanya hivyo aangalie faulu zilizofanyika katika mchakato wa uchaguzi wa serikali za mitaa.

Anapoyafanya hayo, yeye kama muumini wa kanisa katoliki aongee na Mungu aliyempa kibali kutawala nchi hii na kuona kama ametenda haki. Mungu ndiye atakayehukumu lakini kwa haya niliyoyasema damu yake haitadaiwa mikononi mwangu. Hapa nasimama, Mungu nisaidie.

+Askofu Stephen Munga
KKKT
Clip fupi tu hiyo ndio maelezo yote haya! Duh, ipo kazi! Nimeishia njiani sijayamaliza kwa kweli maana kujitetea kwingi na kujijaradia kumezidi sana!
 
Mimi ni Mkatoliki damu, lakini kwa hili la uropokaji wa pengo Mr. Munga nimekuelewa. Huyo pengo anatia aibu, labda ni uzee unamsumbua!!
 
Ufupi wa clip siyo hoja, issue ni content au ujumbe uliobebwa na clip, hata kama lingekuwa neno moja au mawili tu yametamkwa yanatosha kuandikiwa stori ya urefu wowote. Kutokumaliza kusoma inaweza kuwa imetokana na uzembe wako.
 
Mimi ni Mkatoliki damu, lakini kwa hili la uropokaji wa pengo Mr. Munga nimekuelewa. Huyo pengo anatia aibu, labda ni uzee unamsumbua!!

Wewe sio mkatoliki wewe Ni CHadema. Hakuna baya lolote alilosema mwadhama, Tena Kasema kwa maneno niliyoyasikia hapa. He was very klar and precise. Shida yenu sio Mwadhama. Shida yenu Ni Makonda. Ndo mana Shao na huyo Munga kwenu Ni mashujaa. You know why. Because nyie mnaojihita wanademokrasia, hamjawahi kuishi hiyo Demokrasia na sijui hata kama mnailewa maana yake. Hamjawahi kuheshimu mawazo Huru ya wengine . Kama kuna Madikteta Basi ndo nyinyi. Originale.
 
Wewe kichaa kwelikweli, chadema siyo dini! Naweza kuwa chadema na Mkatoliki vilevile japo sina kadi ya chama chochote cha siasa. Hivyo classification yako kuwa mimi ni chadema ni baseless na ni ya kipuuzi kwelikweli.

Hivi uoni tatizo lolote pengo kuacha wito wake wa kuhubiri neno la Mungu na kuanza kuhubiri uchama wake wa ccm. Sidhani kama yeye pengo ni mbumbumbu kama wewe, hivyo anajua ya kwamba dini kubwa ya Katoliki ambayo yeye ni mmoja wa viongozi wake, ina wahumini kutoka vyama mbalimbali. Hivyo hata kama yeye kama binadamu anaipenda ccm siyo vyema kukaa anasifia sifia uccm wake na kuwasifia wanasiasa wa mlengo wa chama chake. Siyo sawa hata kidogo labda watu wajingawajinga kama wewe msioelewa ndiyo mnaona yuko sawa.
 
Mwenzenu katumwa asafishe njia kwa waumini, 3/4 ya wakristo wote Tanzania ni RC. kila mkoa/wilaya wapo
Njia ipi? Wakatoliki awafuati au kupelekwa kinyumbunyumbu, wengi wetu tunajua mbichi na mbivu ndiyo maana tumedumu kwenye ukatoliki kwa sababu ni dhehebu imara na kweli lisilohubiri hubiri vimiujiza feki. Manyumbu wengi walishashidwa ukatoliki, walishaondoka na kuamia kwenye vikanisa vidogo vinavyohubiri uongo uongo kupitia mgongo wa tumiujiza ujiza. Hivyo hata akitokea huyo unayesema anasafisha njia wakatoliki siyo wajinga kufuata mlengo wake wa siasa eti labda kwa sababu yeye ni askofu, watampuuza tu na kufuata yale tu anayofundisha yanayohusiana na imani yetu ya Catholic basi.
 
Pengo akimtukuza Kaisari na vibaraka wake anakuwa anatimiza wajibu wa kidini, Muga na wenzake wakitahadharisha na kukemea mambo yanayofanywa na Kaisari wanakuwa wanafanya siasa, hii nchi ina vilaza wengi sana!!!
 
Back
Top Bottom