Askofu Dkt. Mtokambali: " Wito wa maombi maalum ya kitaifa ya siku 21 dhidi ya wimbi la pili la maambukizi ya virusi vya Corona (COVID-19)”.

Kinyungu

JF-Expert Member
Apr 6, 2008
12,277
2,000
Wana jamvi amani kwenu !

Leo nachukua nafasi hii kumpongeza askofu mkuu Dkt. Barnabas W. Mtokamhali wa kanisa la TAG; kwa barua ya kumbukumbu TAG/MNM/GEN/45 ya tarehe 05 Machi 2021; kwenda Maaskofu wote wa Majimbo,Wakurugenzi wote wa Idara na Vitengo, Waangalizi wote wa Sehemu, Wachungaji wote, na Washirika wote wa Tanzania Assemblies of God (TAG) kuhusu “WITO WA MAOMBI MAALUM YA KITAIFA YA SIKU ISHIRINI NA MOJA (21) DHIDI YA WIMBI LA PILI LA MAAMBUKIZI YA VIRUSI VYA CORONA (COVID-19)”. Hivyo, maombi kwa kanisa la TAG kuanza Jumatatu tarehe 8 Machi mpaka Jumapili tarehe 28 Machi-2021.

Mambo makuu ya kuombea ni kama ifuatavyo:

• Toba kwa ajili ya Kanisa na Taifa.

• Kuomba neema ya uponyaji wa COVID 19 kwa waliopata ugonjwa huu.

• Kuomba maambukizi ya COVID 19 yasienee nchini.

• Kuomba dhidi ya magonjwa mengine kama vile Kisukari, Presha, Moyo, Tezi Dume, Figo, Saratani n.k.

• Kuomba dhidi ya hofu inayowakamata watu wakati huu wa wimbi la COVID 19.

• Kuomba dhidi ya majanga mengine kama vile Nzige, Ukame, Mafuriko, Ajali n.k.

• Kuomba kwa ajili ya ustawi wa Taifa letu na uchumi wake

• Kuombea Viongozi wa Nchi (Rais na Wasaidizi wake, Bunge, Mahakama n.k).

• Kuombea umoja na mshikamano wa Taifa letu wakati huu wa janga na baada ya janga kupita.

• Shukrani.

Mwisho, Kanisa la Tanzania Assemblies of God (TAG) linatambua kuwa Mungu pekee ndiye kimbilio na nguvu, msaada utakaoonekana tele wakati huu wa janga hili la Corona. Hivyo basi, hatutaogopa ijapobadilika nchi, ijapotetemeka milima moyoni mwa bahari (Zahuri 46:1-2a). Lakini pia, tunaamini juu ya umuhimu wa kujikinga kwa kufuata tahadhari zote na maelekezo yote ya kitaalam yanayotolewa na serikali kupitia Wizara ya Afya (Waefeso 5:15-17).

Tukumbuke kwamba katika lile wimbi la kwanza la janga hili, tulimwomba Mungu akaturehemu na kutupa uponyaji wake. Basi nawaomba kwa nia moja tumwombe Mungu tena katika wimbi hili la pili, kwa bidii yote na kwa kujidhabihu kwa ajili ya taifa letu na Bwana aliye mwaminifu atatusikia.

Askofu mkuu Dkt. Barnabas W. Mtokamhali wa kanisa la TAG; alimalizia waraka maalum kwa kuwatakia baraka za Bwana wanapoendelea kumwamini Mungu asiyeshindwa na kitu juu ya wimbi hili la pili la virusi vya ugonjwa wa korona .
Pole mwenyewe amechanjwa sembuse wao walioletewa dini na meli za mapazia
 
Dumas the terrible

JF-Expert Member
Jan 20, 2021
1,674
2,000
Acheni usanii nyie makanjanja,huyo Mungu mnamlisha memes sana yani,aponye yeye mkampa tuzo ya kushinda corona jiwe haahaahaa nyie ndo mnasababisha janga lirudi kwa kasi kwa unafiki wenu,
Hakuna cha maombi wala miujiza ya harusi ya kana Yesu kugeuza maji divai,
Kuhusu corona msipochukua tahadhari mtakufa kama kuku wa mdondo halafu mkaanza kumwekea huyo Mungu memes zenu et ni mipango yake na kazi yake haina
makosa

Shubhamit!

Ndanganya wadau?
 
Good Father

JF-Expert Member
Feb 28, 2014
9,227
2,000
Wana jamvi amani kwenu !

Leo nachukua nafasi hii kumpongeza askofu mkuu Dkt. Barnabas W. Mtokamhali wa kanisa la TAG; kwa barua ya kumbukumbu TAG/MNM/GEN/45 ya tarehe 05 Machi 2021; kwenda Maaskofu wote wa Majimbo,Wakurugenzi wote wa Idara na Vitengo, Waangalizi wote wa Sehemu, Wachungaji wote, na Washirika wote wa Tanzania Assemblies of God (TAG) kuhusu “WITO WA MAOMBI MAALUM YA KITAIFA YA SIKU ISHIRINI NA MOJA (21) DHIDI YA WIMBI LA PILI LA MAAMBUKIZI YA VIRUSI VYA CORONA (COVID-19)”. Hivyo, maombi kwa kanisa la TAG kuanza Jumatatu tarehe 8 Machi mpaka Jumapili tarehe 28 Machi-2021.

Mambo makuu ya kuombea ni kama ifuatavyo:

• Toba kwa ajili ya Kanisa na Taifa.

• Kuomba neema ya uponyaji wa COVID 19 kwa waliopata ugonjwa huu.

• Kuomba maambukizi ya COVID 19 yasienee nchini.

• Kuomba dhidi ya magonjwa mengine kama vile Kisukari, Presha, Moyo, Tezi Dume, Figo, Saratani n.k.

• Kuomba dhidi ya hofu inayowakamata watu wakati huu wa wimbi la COVID 19.

• Kuomba dhidi ya majanga mengine kama vile Nzige, Ukame, Mafuriko, Ajali n.k.

• Kuomba kwa ajili ya ustawi wa Taifa letu na uchumi wake

• Kuombea Viongozi wa Nchi (Rais na Wasaidizi wake, Bunge, Mahakama n.k).

• Kuombea umoja na mshikamano wa Taifa letu wakati huu wa janga na baada ya janga kupita.

• Shukrani.

Mwisho, Kanisa la Tanzania Assemblies of God (TAG) linatambua kuwa Mungu pekee ndiye kimbilio na nguvu, msaada utakaoonekana tele wakati huu wa janga hili la Corona. Hivyo basi, hatutaogopa ijapobadilika nchi, ijapotetemeka milima moyoni mwa bahari (Zahuri 46:1-2a). Lakini pia, tunaamini juu ya umuhimu wa kujikinga kwa kufuata tahadhari zote na maelekezo yote ya kitaalam yanayotolewa na serikali kupitia Wizara ya Afya (Waefeso 5:15-17).

Tukumbuke kwamba katika lile wimbi la kwanza la janga hili, tulimwomba Mungu akaturehemu na kutupa uponyaji wake. Basi nawaomba kwa nia moja tumwombe Mungu tena katika wimbi hili la pili, kwa bidii yote na kwa kujidhabihu kwa ajili ya taifa letu na Bwana aliye mwaminifu atatusikia.

Askofu mkuu Dkt. Barnabas W. Mtokamhali wa kanisa la TAG; alimalizia waraka maalum kwa kuwatakia baraka za Bwana wanapoendelea kumwamini Mungu asiyeshindwa na kitu juu ya wimbi hili la pili la virusi vya ugonjwa wa korona .

Wajasiriamali katika wakati wao.

Duniani kuna manyumbu na binadamu wa kawaida.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom