Askofu Frederick Shoo: Viongozi wa dini wanapaswa kutoegemea upande mmoja wa siasa kwa kuwa watu wa vyama vyote ni waumini wao

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,498
9,279
MKUU wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Askofu Dkt. Frederick Shoo, amekemea vitendo vya kupigwa na kudhalilishwa kwa baadhi ya wagombea hasa wanawake katika kampeni za uchaguzi na kutahadharisha kuwa iwapo vitendo hivyo, vikiaachiwa viendelee vitahatarisha amani.

shoo.jpg
MKUU wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Askofu Dk. Frederick Shoo, picha mtandao

Sambamba na hilo, amesema suala la viongozi wa dini kuegemea chama kimoja cha siasa linapaswa kukemewa kwa kuwa linawagawa wananchi.

Askofu Dkt. Shoo aliyasema hayo jana jijini hapa alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari baada ya kufungua mdahalo wa viongozi wa dini kuhusu kuhamasisha ushiriki wa wanawake kwenye uongozi na ngazi za uamuzi.

Mdahalo huo umeandaliwa na Shirika la Wanawake katika Sheria na Maendeleo Barani Afrika (WiLDAF) kwa ufadhili wa Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na masuala ya wanawake (UN-Women).

Alisema viongozi wa dini wanapaswa kutoegemea upande mmoja kwa kuwa watu wa vyama vyote ni waumini wao.

“Unapoegemea waziwazi chama kimoja, tukijua hawa ni wanasiasa na siasa ni mchezo wa aina yake, kama viongozi wa dini, maandiko yanaelekeza vizuri kabisa namna ya kusimama na namna ya kuhitaji wote kuwashauri na kuwaombea. Kama kuna mahali pa kukemea kutokana na ukiukwaji wote kwa pamoja, fanya bila ubaguzi na kuficha,” alisema.

Kuhusu vitendo vya udhalilishaji, Dk. Shoo alisema lugha za kudhalilisha zinamkwamisha mwanamke kushiriki kwenye uongozi hivyo zinapaswa kukemewa.

“Tumekemea na kutahadharisha kwamba uvunjifu wa amani unaanza na jambo dogo kwa hiyo si tu wanawake, kuwadhalilisha, kuwapiga wagombea wa aina yoyote hususan wanawake. Linapotokea jambo la namna hiyo, linagusa hisia za watu. Nasema mambo hayo ni ya kukemewa na kuachwa mara moja na jamii yetu,” alisema.

“Tumeshuhudia lugha za udhalilishaji hasa kipindi hiki cha kampeni. Ni vyema mdahalo ukatoka na tamko la kukemea wale wote wenye lugha za udhalilishaji wanawake,” alisisitiza.

Alisema pia suala la rushwa linamkwamisha mwanamke licha ya kuwa na uwezo.
“Hii imesababisha wanawake kushindwa kuthubutu kujitokeza kushiriki kwenye ngazi za maamuzi, sisi viongozi wa dini tunapaswa kulaani na kukemea vitendo hivi viovu, wanawake wanayo haki ya kushika nafasi,”alisema.

Hata hivyo, alisema wanawake wanaojitambua hawapaswi kuwa na hofu zinapozungumziwa haki za wanawake.

“Kwenye sensa ya watu na makazi ya mwaka 2002, inaonyesha wanawake ni asilimia 51, ili nchi yetu iwe na maendeleo ya uchumi wa viwanda kundi hili lazima lishiriki kwenye ngazi za maamuzi ya maendeleo ya kiuchumi,” alisema.

Dk. Shoo alisema kuna ushiriki duni wa wanawake kwenye ngazi za maamuzi, ambapo ngazi ya ubunge wanawake ni asilimia 36.9, ambao wanatokana na majimbo na viti maalum.

Alitaja mambo manne, ambayo viongozi wa dini wanapaswa kusimamia ni kuhamasisha ushirikishwaji wa wanawake katika ngazi za uongozi na uamuzi, kuzuia migogoro isiyo ya lazima, kejeli, lugha za kashfa na udhalilishaji hususan kipindi hiki cha kampeni za uchaguzi.

“Wale tunaofahamu nafasi ya mama sawasawa hakuna kinachoudhi unaposikia mtu anakutukania mama yako au anamdhalilisha mama. Ni kitu kinagusa hisia, tuchunge ndimi ni muhimu sana,” alisema.

Naye Shehe wa Mkoa wa Morogoro, Twaha Kilango, alisema kipindi kilichopo sasa kinapaswa kila mmoja kulinda ndimi yake, ili kutoleta madhara kwa jamii.

Mkurugenzi Mtendaji wa WILDAF, Wakili Anna Kulaya, alisema vitendo vya udhalilishaji vinavyoondoa utu wa mwanamke ni miongoni mwa vikwazo vinavyochangia ushiriki mdogo wa wanawake kwenye uongozi.
 
MKUU wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Askofu Dkt. Frederick Shoo, amekemea vitendo vya kupigwa na kudhalilishwa kwa baadhi ya wagombea hasa wanawake katika kampeni za uchaguzi na kutahadharisha kuwa iwapo vitendo hivyo, vikiaachiwa viendelee vitahatarisha amani...
Ukisema haki ,usawa na Uhuru kwa nchi hii unaitwa Chadema. Huu Uzi maccm yatakuja mpinga baba askofu maana wamezoea Yale ya masheikh ubwabwa wa BAKWATA
 
MKUU wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Askofu Dkt. Frederick Shoo, amekemea vitendo vya kupigwa na kudhalilishwa kwa baadhi ya wagombea hasa wanawake katika kampeni za uchaguzi na kutahadharisha kuwa iwapo vitendo hivyo, vikiaachiwa viendelee vitahatarisha amani...
Viongozi wa dini ni binadamu sio miungu. Wanapaswa kuegemea upande wa HAKI na kutetea wanyonge. Vinginevyo ni UNAFIKI.
 
Nampongeza Sana Askofu Shoo Mkuu wa Kanisa la KKKT ! Maaskofu wote hapa Nchini , nawasihi Sana wasiegemee upande wowote wa Chama chochote cha Siasa hapa Nchini kwa sasa ! Tuwaache Watanzania Waamue tarehe 28 October . Tusiwagawe Waumini ! Narudia tena kulizungumza hili , Kiongozi wa kiroho ( Shekhe , Padri , MCHUNGAJI , Maaskofu hawapaswi kuonyesha ushabiki kwa Chama chochote
 
Back
Top Bottom