Askofu Dk Shoo: Naipongeza hatua ya kufufua njia ya reli ya Dar es Salaam hadi Moshi mkoani Kilimanjaro

alipata elimu ya kuondoa ujinga bila ya kuongeza maarifa.(Bagonza)
Kinachoshangaza zaidi mwenye elimu ya kuongeza maarifa anajibu hoja za mwenye elimu ya kuondoa ujinga! Sijui ni nani ataonekana ''kituko'' kwa watu wenye fikra pana!
 
Enea>>>>Tanzania ina square kilometer 945.000. Kwa hiyo katika ukubwa huo, utekaji umeenea katika ukubwa/maeneo gani?

Kupata kasi>>>Kwa kasi ya kiwango gani huu utekaji unaenda hasa ikichukuliwa kuwa Tanzania ina watu zaidi ya milioni 55?
Siku yakikufika ndipo utakapojua kuwa yamefikia kiwango gani. yalipoanza kwa wanasiasa, wanahabari walikuwa kimya wakidhani hayatawafika, yalipofika wa wanahabari wafanyabiasha nao wakaona hayatawafika, yakahamia kwa wanamuziki, wakaharakati hatujui nani anafuatia.
 
Hayachagui kama unavunja sheria! Tii sheria bila shuruti!

Kumbuka Tanzania ina wananchi milioni 55 lakini walioko magerezani ni 17,000!
 
Mbona huja sema na aliyo yaongea. Kuhusu uchaguzi wa serikali za mitaa??
View attachment 1302025

Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) limeipongeza Serikali ya Awamu ya Tano, kwa kuboresha miundombinu ya barabara na hatua ya kufufua njia ya reli ya Dar es Salaam hadi Moshi mkoani Kilimanjaro.

Kanisa hilo limesema siri ya kwanza ya maendeleo katika nchi ni uwepo wa miundombinu bora na miongoni mwake miundombinu ya kwanza ni ya njia ya reli.

Mkuu wa KKKT, Askofu Dk Fredrick Shoo alitoa pongezi hizo kwa Serikali ya Awamu ya Tano Rais Dk John Magufuli juzi kwenye mahubiri ya Ibada ya Misa ya Jumapili, iliyofanyika katika Kanisa Kuu la Bungo KKKT Dayosisi ya Morogoro.

Ibada hiyo maalumu ya Jubilee ya miaka 25 ya Ndoa na Utumishi wa Kichungaji wa Baba Askofu Jacob Mameo Ole Paulo na mkewe Rose Suleiman Kim’hanga, ilihudhuriwa pia na Waziri Mkuu mstaafu Edward Lowassa, mkewe Regina, na wakuu wa mikoa ya Njombe, Christopher Ole Sendeka, wa Kigoma, Emmanuel Maganga na mwenyeji wao wa Morogoro, Loata Ole Sanare.

Askofu Shoo amesema siri ya kwanza ya maendeleo katika nchi ni uwepo wa miundombinu bora na miongoni mwake miundombinu ya kwanza ni ya njia ya reli.

Dk Shoo alisema kama Taifa linataka maendeleo, siri ya kwanza ni kuwa na miundombinu bora na zaidi ni ya reli, hivyo alimshukuru Rais John Magufuli kwa kuanzisha tena treni kutoka Dar es Salaam hadi Moshi. “Miundombinu bora ni jambo la msingi sana kwa maendeleo ya nchi, sisi hapa sote tumesafiri kutoka mbali kuja Morogoro kwenye sherehe hii.

“Na watu wa Kaskazini wakati huu ni kurudi nyumbani, nasikia wanatumia usafiri wa treni na imejaa kweli kweli kutoka Dar es Salaam kwenda mikoa ya Kaskazini mbali na usafiri wa mabasi,” alisema Askofu Mkuu huyo wa KKKT.

Alisema treni hiyo ilikuwa imefungwa muda mrefu, ambayo wakati huo ilikuwa ikitoka Dar es Salaam, Kilimanjaro kwenda hadi Taveta nchini Kenya. Hata hivyo, baada ya usafiri huo kusimama kwa miaka mingi, baadhi ya watu walidiriki kung’oa vyuma vya reli na kwenda kuviuza kama chuma chakavu kwani jambo hilo lilimchukiza kuona hakuna reli.

“Jambo la kung’oa miundombinu ya reli lilinisikitisha kweli na kama vitu vilivyonichukiza ni kuona hatuna reli kweli nilijuliza tuna kwenda wapi kama nchi? Kwa hali ya sasa namshukuru Rais Magufuli, treni iliyoanza kusafiri siku chache zilizopitia kwenda Moshi na mikoa ya Kaskazini mabehewa yote yanajaa licha ya uwepo wa mabasi,” alisema Askofu Mkuu Shoo.

Kutokana na mahitaji makubwa ya usafiri huo, aliambiwa kuwa hata baadhi ya mabehewa ya treni ya Deluxe ya kwenda Kigoma, yamehamishiwa njia ya Moshi kutokana na mahitaji makubwa ya usafiri huo.

“Kwa sasa nilikuwa natamani nisafiri na treni, lakini kwa vile upo ujenzi wa reli ya mwendokasi (SGR) kutoka Dar es Salaam hadi hapa Morogoro itakuwa ni kiunganishi cha usafiri wa haraka kwa treni,” aliongeza.

Treni ya abiria inayofanya safari zake Dar es Salaam kupitia mikoa ya Pwani, Tanga na Kilimanjaro ilianza rasmi Desemba 6, mwaka huu baada ya huduma hiyo kusimama kwa takribani miaka 25 iliyopita. Pia safari za treni ya mizigo kutoka Tanga hadi Moshi zilishaanza.

Chanzo: Habari Leo

VIDEO: MAONI YA WANANCHI WAKIWA NDANI YA TRENI

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hapo hutawasikia wale wenye kauli za kuchanganya siasa na dini. Ila ingekuwa kakemea sasa kusingetosha huku jukwaani
Kina nani hao wa kauli za kuchanganya siasa na dini?

Na wale wa kauli za kutochanganya siasa na dini ni kina nani?
 
Tulisema wengi tutamuelewa Magufuli. Tunachotofautiana na spidi ya kumuelewa.
Kwa taarifa ni kuwa sio treni tu imejaa hata ndege zimejaa.
Kuna baadhi ya wenzetu huwa wanasema maendeleo ni watu sio vitu. Sasa hapo baba askofu inabidi awaite akao nao chini awaelimishe.

Sent using Jamii Forums mobile app
Akiwakosoa pia mkubali, msiseme anachaganya siasa na dini.
 
Wanaposema maendeleo ya watu hawakatai maendeleo ya vitu, tatizo ni pale vitu vinapokuwa muhimu kuliko watu. Hata kwenye bible imeandikwa juu ya watu wanaopenda pesa, tatizo siyo pesa, problem is preoccupation with money.
Unapotaka kuleta maendeleo ya watu ni lazima uanze na vitu. Kabla ya Nyerere Tanzania ilikuwa na watu. Nyerere aliposhika hatamu alijenga shule, viwanda, miundo mbinu na hospital kwa fujo japo vilijuwa vichache. Lengo ilikuwa kuendeleza watu.
Tukikupa kiwanja sehemu isiyokuwa na umeme, maji wala barabara inaweza kukuchukua miaka 50 ili kuliendeleza hilo eneo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
View attachment 1302025

Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) limeipongeza Serikali ya Awamu ya Tano, kwa kuboresha miundombinu ya barabara na hatua ya kufufua njia ya reli ya Dar es Salaam hadi Moshi mkoani Kilimanjaro.

Kanisa hilo limesema siri ya kwanza ya maendeleo katika nchi ni uwepo wa miundombinu bora na miongoni mwake miundombinu ya kwanza ni ya njia ya reli.

Mkuu wa KKKT, Askofu Dk Fredrick Shoo alitoa pongezi hizo kwa Serikali ya Awamu ya Tano Rais Dk John Magufuli juzi kwenye mahubiri ya Ibada ya Misa ya Jumapili, iliyofanyika katika Kanisa Kuu la Bungo KKKT Dayosisi ya Morogoro.

Ibada hiyo maalumu ya Jubilee ya miaka 25 ya Ndoa na Utumishi wa Kichungaji wa Baba Askofu Jacob Mameo Ole Paulo na mkewe Rose Suleiman Kim’hanga, ilihudhuriwa pia na Waziri Mkuu mstaafu Edward Lowassa, mkewe Regina, na wakuu wa mikoa ya Njombe, Christopher Ole Sendeka, wa Kigoma, Emmanuel Maganga na mwenyeji wao wa Morogoro, Loata Ole Sanare.

Askofu Shoo amesema siri ya kwanza ya maendeleo katika nchi ni uwepo wa miundombinu bora na miongoni mwake miundombinu ya kwanza ni ya njia ya reli.

Dk Shoo alisema kama Taifa linataka maendeleo, siri ya kwanza ni kuwa na miundombinu bora na zaidi ni ya reli, hivyo alimshukuru Rais John Magufuli kwa kuanzisha tena treni kutoka Dar es Salaam hadi Moshi. “Miundombinu bora ni jambo la msingi sana kwa maendeleo ya nchi, sisi hapa sote tumesafiri kutoka mbali kuja Morogoro kwenye sherehe hii.

“Na watu wa Kaskazini wakati huu ni kurudi nyumbani, nasikia wanatumia usafiri wa treni na imejaa kweli kweli kutoka Dar es Salaam kwenda mikoa ya Kaskazini mbali na usafiri wa mabasi,” alisema Askofu Mkuu huyo wa KKKT.

Alisema treni hiyo ilikuwa imefungwa muda mrefu, ambayo wakati huo ilikuwa ikitoka Dar es Salaam, Kilimanjaro kwenda hadi Taveta nchini Kenya. Hata hivyo, baada ya usafiri huo kusimama kwa miaka mingi, baadhi ya watu walidiriki kung’oa vyuma vya reli na kwenda kuviuza kama chuma chakavu kwani jambo hilo lilimchukiza kuona hakuna reli.

“Jambo la kung’oa miundombinu ya reli lilinisikitisha kweli na kama vitu vilivyonichukiza ni kuona hatuna reli kweli nilijuliza tuna kwenda wapi kama nchi? Kwa hali ya sasa namshukuru Rais Magufuli, treni iliyoanza kusafiri siku chache zilizopitia kwenda Moshi na mikoa ya Kaskazini mabehewa yote yanajaa licha ya uwepo wa mabasi,” alisema Askofu Mkuu Shoo.

Kutokana na mahitaji makubwa ya usafiri huo, aliambiwa kuwa hata baadhi ya mabehewa ya treni ya Deluxe ya kwenda Kigoma, yamehamishiwa njia ya Moshi kutokana na mahitaji makubwa ya usafiri huo.

“Kwa sasa nilikuwa natamani nisafiri na treni, lakini kwa vile upo ujenzi wa reli ya mwendokasi (SGR) kutoka Dar es Salaam hadi hapa Morogoro itakuwa ni kiunganishi cha usafiri wa haraka kwa treni,” aliongeza.

Treni ya abiria inayofanya safari zake Dar es Salaam kupitia mikoa ya Pwani, Tanga na Kilimanjaro ilianza rasmi Desemba 6, mwaka huu baada ya huduma hiyo kusimama kwa takribani miaka 25 iliyopita. Pia safari za treni ya mizigo kutoka Tanga hadi Moshi zilishaanza.

Chanzo: Habari Leo

VIDEO: MAONI YA WANANCHI WAKIWA NDANI YA TRENI
Hakuna nchi yeyote Duniani narudia tena hakuna nchi yeyote Duniani inayotaka maendeleo ya dhati na uimarishaji wa viwanda bila Treni ni mwendawazimu tu atakaekataa hili Bravo Rais Magufuli japo wazungu wanatubania na vimsaada vyao lakini ukiwa na nia na uthubutu tumeweza natutaweza tena kwani wao waliweza wana nini na sisi tushindwe tuna nini kwa pamoja tutafika nchi ya maendeleo lipa kodi mtanzania mwenzangu kazi ndio kwanzaa tunaanza na matokeo mazuri twayaona kwa macho ya nyama Kongole Magufuli kwa uthubutu Umoja ni Nguvu Merry christmas and Happy New Year

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Naungana na askofu wa kkkt-moshi kwa pongezi hili na alichokisema. Reli hii ikiboreshwa itasaidia sana kuwadhibiti TABOA wanaopenda kujipandishia nauli kila mwisho wa mwaka

Ila pongezi hii isitumike vibaya kuhalalisha yale yote yasiyo halali na yaliyojaa dhurma yanayoihusu serikali yetu.

Asikofu huyu watanzania wengi wamejenga imani naye na wanampenda kwa kupenda kusimamia ukweli na haki. Mwenyezi Mungu ampe maisha mema yenye fanaka mja wake

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom