Askofu Dk Shoo: Naipongeza hatua ya kufufua njia ya reli ya Dar es Salaam hadi Moshi mkoani Kilimanjaro

MsemajiUkweli

JF-Expert Member
Joined
Jul 5, 2012
Messages
11,750
Points
2,000

MsemajiUkweli

JF-Expert Member
Joined Jul 5, 2012
11,750 2,000
1577168641643.jpeg

Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) limeipongeza Serikali ya Awamu ya Tano, kwa kuboresha miundombinu ya barabara na hatua ya kufufua njia ya reli ya Dar es Salaam hadi Moshi mkoani Kilimanjaro.

Kanisa hilo limesema siri ya kwanza ya maendeleo katika nchi ni uwepo wa miundombinu bora na miongoni mwake miundombinu ya kwanza ni ya njia ya reli.

Mkuu wa KKKT, Askofu Dk Fredrick Shoo alitoa pongezi hizo kwa Serikali ya Awamu ya Tano Rais Dk John Magufuli juzi kwenye mahubiri ya Ibada ya Misa ya Jumapili, iliyofanyika katika Kanisa Kuu la Bungo KKKT Dayosisi ya Morogoro.

Ibada hiyo maalumu ya Jubilee ya miaka 25 ya Ndoa na Utumishi wa Kichungaji wa Baba Askofu Jacob Mameo Ole Paulo na mkewe Rose Suleiman Kim’hanga, ilihudhuriwa pia na Waziri Mkuu mstaafu Edward Lowassa, mkewe Regina, na wakuu wa mikoa ya Njombe, Christopher Ole Sendeka, wa Kigoma, Emmanuel Maganga na mwenyeji wao wa Morogoro, Loata Ole Sanare.

Askofu Shoo amesema siri ya kwanza ya maendeleo katika nchi ni uwepo wa miundombinu bora na miongoni mwake miundombinu ya kwanza ni ya njia ya reli.

Dk Shoo alisema kama Taifa linataka maendeleo, siri ya kwanza ni kuwa na miundombinu bora na zaidi ni ya reli, hivyo alimshukuru Rais John Magufuli kwa kuanzisha tena treni kutoka Dar es Salaam hadi Moshi. “Miundombinu bora ni jambo la msingi sana kwa maendeleo ya nchi, sisi hapa sote tumesafiri kutoka mbali kuja Morogoro kwenye sherehe hii.

“Na watu wa Kaskazini wakati huu ni kurudi nyumbani, nasikia wanatumia usafiri wa treni na imejaa kweli kweli kutoka Dar es Salaam kwenda mikoa ya Kaskazini mbali na usafiri wa mabasi,” alisema Askofu Mkuu huyo wa KKKT.

Alisema treni hiyo ilikuwa imefungwa muda mrefu, ambayo wakati huo ilikuwa ikitoka Dar es Salaam, Kilimanjaro kwenda hadi Taveta nchini Kenya. Hata hivyo, baada ya usafiri huo kusimama kwa miaka mingi, baadhi ya watu walidiriki kung’oa vyuma vya reli na kwenda kuviuza kama chuma chakavu kwani jambo hilo lilimchukiza kuona hakuna reli.

“Jambo la kung’oa miundombinu ya reli lilinisikitisha kweli na kama vitu vilivyonichukiza ni kuona hatuna reli kweli nilijuliza tuna kwenda wapi kama nchi? Kwa hali ya sasa namshukuru Rais Magufuli, treni iliyoanza kusafiri siku chache zilizopitia kwenda Moshi na mikoa ya Kaskazini mabehewa yote yanajaa licha ya uwepo wa mabasi,” alisema Askofu Mkuu Shoo.

Kutokana na mahitaji makubwa ya usafiri huo, aliambiwa kuwa hata baadhi ya mabehewa ya treni ya Deluxe ya kwenda Kigoma, yamehamishiwa njia ya Moshi kutokana na mahitaji makubwa ya usafiri huo.

“Kwa sasa nilikuwa natamani nisafiri na treni, lakini kwa vile upo ujenzi wa reli ya mwendokasi (SGR) kutoka Dar es Salaam hadi hapa Morogoro itakuwa ni kiunganishi cha usafiri wa haraka kwa treni,” aliongeza.

Treni ya abiria inayofanya safari zake Dar es Salaam kupitia mikoa ya Pwani, Tanga na Kilimanjaro ilianza rasmi Desemba 6, mwaka huu baada ya huduma hiyo kusimama kwa takribani miaka 25 iliyopita. Pia safari za treni ya mizigo kutoka Tanga hadi Moshi zilishaanza.

Chanzo: Habari Leo

VIDEO: MAONI YA WANANCHI WAKIWA NDANI YA TRENI
 
Johnny Sack

JF-Expert Member
Joined
Jan 21, 2017
Messages
1,313
Points
2,000

Johnny Sack

JF-Expert Member
Joined Jan 21, 2017
1,313 2,000
Penye kustahili pongezi tupongeze, lakini haya mazuri yote yanafutwa na utekaji ulioshamiri. Laiti huyu jamaa angefuata sheria za nchi kidogo tu he would have left the legacy of being the best president.
Wala hata isingemgharimu chochote
 
sheiza

JF-Expert Member
Joined
Sep 29, 2010
Messages
4,473
Points
2,000

sheiza

JF-Expert Member
Joined Sep 29, 2010
4,473 2,000
Tulisema wengi tutamuelewa Magufuli. Tunachotofautiana ni spidi ya kumuelewa.
Kwa taarifa ni kuwa sio treni tu imejaa hata ndege zimejaa.
Kuna baadhi ya wenzetu huwa wanasema maendeleo ni watu sio vitu. Sasa hapo baba askofu inabidi awaite akao nao chini awaelimishe.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
MsemajiUkweli

JF-Expert Member
Joined
Jul 5, 2012
Messages
11,750
Points
2,000

MsemajiUkweli

JF-Expert Member
Joined Jul 5, 2012
11,750 2,000
Penye kustahili pongezi tupongeze, lakini haya mazuri yote yanafutwa na utekaji ulioshamiri. Laiti huyu jamaa angefuata sheria za nchi kidogo tu he would have left the legacy of being the best president.
Inawezekana maneno, ''utekaji ulioshamiri'' lina maana nyingine tofauti na maana ya kiswahili sanifu!
 
emalau

JF-Expert Member
Joined
Apr 25, 2009
Messages
2,613
Points
2,000

emalau

JF-Expert Member
Joined Apr 25, 2009
2,613 2,000
Tulisema wengi tutamuelewa Magufuli. Tunachotofautiana na spidi ya kumuelewa.
Kwa taarifa ni kuwa sio treni tu imejaa hata ndege zimejaa.
Kuna baadhi ya wenzetu huwa wanasema maendeleo ni watu sio vitu. Sasa hapo baba askofu inabidi awaite akao nao chini awaelimishe.

Sent using Jamii Forums mobile app
Wanaposema maendeleo ya watu hawakatai maendeleo ya vitu, tatizo ni pale vitu vinapokuwa muhimu kuliko watu. Hata kwenye bible imeandikwa juu ya watu wanaopenda pesa, tatizo siyo pesa, problem is preoccupation with money.
 
MsemajiUkweli

JF-Expert Member
Joined
Jul 5, 2012
Messages
11,750
Points
2,000

MsemajiUkweli

JF-Expert Member
Joined Jul 5, 2012
11,750 2,000
Wanaposema maendeleo ya watu hawakatai maendeleo ya vitu, tatizo ni pale vitu vinapokuwa muhimu kuliko watu. Hata kwenye bible imeandikwa juu ya watu wanaopenda pesa, tatizo siyo pesa, problem is preoccupation with money.
Yes, vitu lazima vitangulie kabla ya watu. Hata Mwenyezi Mungu alianza kwanza kuumba vitu kabla ya binadamu kama tunavyoelezwa kwenye Biblia. Hii haikuwa na maana kuwa vitu vilikuwa muhimu zaidi ya binadamu.
 
MsemajiUkweli

JF-Expert Member
Joined
Jul 5, 2012
Messages
11,750
Points
2,000

MsemajiUkweli

JF-Expert Member
Joined Jul 5, 2012
11,750 2,000
Naona unataka twende somo la kiswahili, kwa mujibu wa kamusi shamiri maana yake - enea na kupata kasi, sasa ninaposema utekaji ulioshamiri maana yake ni utekaji ulioenea kwa kasi. Hapo nadhani tupo pamoja mwalimu wa kiswahili.
Enea>>>>Tanzania ina square kilometer 945.000. Kwa hiyo katika ukubwa huo, utekaji umeenea katika ukubwa/maeneo gani?

Kupata kasi>>>Kwa kasi ya kiwango gani huu utekaji unaenda hasa ikichukuliwa kuwa Tanzania ina watu zaidi ya milioni 55?
 
MsemajiUkweli

JF-Expert Member
Joined
Jul 5, 2012
Messages
11,750
Points
2,000

MsemajiUkweli

JF-Expert Member
Joined Jul 5, 2012
11,750 2,000

mitigator

JF-Expert Member
Joined
Dec 28, 2014
Messages
4,116
Points
2,000

mitigator

JF-Expert Member
Joined Dec 28, 2014
4,116 2,000
KKKT yakubali kishindo cha Rais Magufuli

View attachment 1302025

Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) limeipongeza Serikali ya Awamu ya Tano, kwa kuboresha miundombinu ya barabara na hatua ya kufufua njia ya reli ya Dar es Salaam hadi Moshi mkoani Kilimanjaro.

Kanisa hilo limesema siri ya kwanza ya maendeleo katika nchi ni uwepo wa miundombinu bora na miongoni mwake miundombinu ya kwanza ni ya njia ya reli.

Mkuu wa KKKT, Askofu Dk Fredrick Shoo alitoa pongezi hizo kwa Serikali ya Awamu ya Tano Rais Dk John Magufuli juzi kwenye mahubiri ya Ibada ya Misa ya Jumapili, iliyofanyika katika Kanisa Kuu la Bungo KKKT Dayosisi ya Morogoro.

Ibada hiyo maalumu ya Jubilee ya miaka 25 ya Ndoa na Utumishi wa Kichungaji wa Baba Askofu Jacob Mameo Ole Paulo na mkewe Rose Suleiman Kim’hanga, ilihudhuriwa pia na Waziri Mkuu mstaafu Edward Lowassa, mkewe Regina, na wakuu wa mikoa ya Njombe, Christopher Ole Sendeka, wa Kigoma, Emmanuel Maganga na mwenyeji wao wa Morogoro, Loata Ole Sanare.

Askofu Shoo amesema siri ya kwanza ya maendeleo katika nchi ni uwepo wa miundombinu bora na miongoni mwake miundombinu ya kwanza ni ya njia ya reli.

Dk Shoo alisema kama Taifa linataka maendeleo, siri ya kwanza ni kuwa na miundombinu bora na zaidi ni ya reli, hivyo alimshukuru Rais John Magufuli kwa kuanzisha tena treni kutoka Dar es Salaam hadi Moshi. “Miundombinu bora ni jambo la msingi sana kwa maendeleo ya nchi, sisi hapa sote tumesafiri kutoka mbali kuja Morogoro kwenye sherehe hii.

“Na watu wa Kaskazini wakati huu ni kurudi nyumbani, nasikia wanatumia usafiri wa treni na imejaa kweli kweli kutoka Dar es Salaam kwenda mikoa ya Kaskazini mbali na usafiri wa mabasi,” alisema Askofu Mkuu huyo wa KKKT.

Alisema treni hiyo ilikuwa imefungwa muda mrefu, ambayo wakati huo ilikuwa ikitoka Dar es Salaam, Kilimanjaro kwenda hadi Taveta nchini Kenya. Hata hivyo, baada ya usafiri huo kusimama kwa miaka mingi, baadhi ya watu walidiriki kung’oa vyuma vya reli na kwenda kuviuza kama chuma chakavu kwani jambo hilo lilimchukiza kuona hakuna reli.

“Jambo la kung’oa miundombinu ya reli lilinisikitisha kweli na kama vitu vilivyonichukiza ni kuona hatuna reli kweli nilijuliza tuna kwenda wapi kama nchi? Kwa hali ya sasa namshukuru Rais Magufuli, treni iliyoanza kusafiri siku chache zilizopitia kwenda Moshi na mikoa ya Kaskazini mabehewa yote yanajaa licha ya uwepo wa mabasi,” alisema Askofu Mkuu Shoo.

Kutokana na mahitaji makubwa ya usafiri huo, aliambiwa kuwa hata baadhi ya mabehewa ya treni ya Deluxe ya kwenda Kigoma, yamehamishiwa njia ya Moshi kutokana na mahitaji makubwa ya usafiri huo.

“Kwa sasa nilikuwa natamani nisafiri na treni, lakini kwa vile upo ujenzi wa reli ya mwendokasi (SGR) kutoka Dar es Salaam hadi hapa Morogoro itakuwa ni kiunganishi cha usafiri wa haraka kwa treni,” aliongeza.

Treni ya abiria inayofanya safari zake Dar es Salaam kupitia mikoa ya Pwani, Tanga na Kilimanjaro ilianza rasmi Desemba 6, mwaka huu baada ya huduma hiyo kusimama kwa takribani miaka 25 iliyopita. Pia safari za treni ya mizigo kutoka Tanga hadi Moshi zilishaanza.

Chanzo: Habari Leo
Yaan hii imekua habar kubwa kwenu kwamba wote tumewapata na wamejiunga na praise team but mlivyoyaajabu mkiparuliwa kidogo tu mnashika mtutu wa bunduki,hii ni abnormality kwenu.KKKT yakubali kishindo cha JPM "huu ni uhariri wa sintofaham kwamba hapo mwanzo kkkt walikua hawamkubali wakati kila mnalofanya Ask Malasusa yupo.Hoja hapa ni misimamo thabiti ya askofu Shoo hvy baada ya pongez mmeona habar kubwa so far,maovu ya serkali ya jpm hayawez kuhqlqlishwa na mazuri,Lait JPM angekubali kutibiwA ugonjwa wa kiburi na kutojishusha angekua kiongozi mzuri.
 
jd41

JF-Expert Member
Joined
Aug 23, 2015
Messages
3,365
Points
2,000

jd41

JF-Expert Member
Joined Aug 23, 2015
3,365 2,000
Enea>>>>Tanzania ina square kilometer 945.000. Kwa hiyo katika ukubwa huo, utekaji umeenea katika ukubwa/maeneo gani?

Kupata kasi>>>Kwa kasi ya kiwango gani huu utekaji unaenda hasa ikichukuliwa kuwa Tanzania ina watu zaidi ya milioni 55?
Punguza mahaba yaliyopitiliza, matukio ya utekwaji yameongezeka sana kwa wakati huu, haiwezekani ndani ya siku 4 watu wawili waripotiwe kutekwa, halafu wewe una simplify eti lazima huo utekwaji uripotiwe maeneo mengi ya nchi ndio tuanze kupiga kelele!, kwasababu hauna ndugu au rafiki alietekwa sio? una kiwango kikubwa sana cha ubinafsi, fikiria na wenzio wacha kutetea kwa kila jambo wanaokulisha ugali hata kama wanaokosea.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Forum statistics

Threads 1,389,758
Members 528,022
Posts 34,033,839
Top