Askofu Dallu: Marufuku shule za kanisa katoliki wanafunzi kuendelea na masomo baada ya kupata mimba

Ukisema wataruhusiwa waliobakwa hapo ujue kila mmoja atakayepata mimba atasema amebakwa na hamjui aliyembaka. Unatakiwa uangalie baadae itakuwaje. Nikuulize kidogo kwa uelewa wako nijibu kama watoto wa kike waliopata mimba wakiruhisiwa je, na kifungo cha miaka 30 jela kwa aliyeshirikiana na huyo msichana ifutwe?
.
Kwa hiyo ni kanisa linawafunga hao unaosema wameshirikiana na msichana?
 
Hivi seminarini kuna kuaga na msamaha kwa mwanafunzi anaekosea ?
Maana nijuavyo hawa jamaa ukilizua tu out bila huruma.
Hawajawahi samehe mwanafunzi hawa
Nashangas huyu nae kilichomleta huku ni nini
Kabla rais ajatoa mtazamo wake hasi ambao pia unaweza uita finyu hawa jamaa ndio maisha ya kibedui na ubabe
 
Kwanza punguzeni chuki

Mbili Kanisa halisapoti uzinzi, huruhusiwi kushiriki tendo la ndoa kama hujafunga ndoa Kanisani

So hata kama ukiwa above 18 kwa mafundisho ya Kikristo hauluhusiwi kujamiana

Serikari ndiyo inayotoa relief watu mjamiane angalau mkiwa wote above 18 na si wanafunzi (hii ni kama ka advantage ka nchi yetu Tanzania kuwa secular state)

Mimi ni mkatoliki tena mseminari, hakuna wazinzi kama mapadre wetu, ni bora Dr Slaa hakutaka kuwa mnafki katika hili akaomba kuacha upadre.

Ifike wakati sasa mapadre na maaskofu wakatoliki waruhusiwe kuowa kuliko kuendelea na uzinifu na ufiraji.

Hakuna mwanaume rijali mwenye mbegu zake anayeweza kukaa bila kuchuja.

Kina Pengo wanawatafuna masista hilo tunalijuwa tuache unafkiunafki.

Kanisa kwa msimamo wa kuwazuia watawa wake kuowa au kuolewa moja kwa moja linasapoti uzinzi tu.

Tena ni afadhali masista kwa nature ya mwanamke anaweza kukaa bila kugongwa lakini siyo mapadre na maaskofu hawa ni wazinzi tu.
 
ASKOFU Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki Songea Mhashamu Damian Dallu amesema kuwa anaunga mkono hatua ya Rais John Magufuli kutoruhusu wanafunzi wanaopata ujauzito kuendelea na masomo, na kusema kuwa shule zinazomilikiwa na Kanisa Katoliki hazitaruhusu wanafunzi wanaopata ujauzito kuendelea na masomo.

Amesema hayo katika Ibada ya Misa Takatifu ya Upadrisho wa Shemasi Jerome Mtatifikolo, iliyofanyika katika Parokia ya Bikira Maria Afya ya wagonjwa Ilole jimboni Iringa ambapo amebainisha kuwa wanaoshabikia wanaopata mimba kurudi shule wanaharibu utamaduni wa kiafrika na kuchafua heshima ya Taifa.

“Hayo mambo siyo sehemu ya utamaduni wetu wa Afrika, ni mambo ya kigeni yanayotaka kutuchafulia utamaduni wetu. Nawashangaa eti wanapigania haki ya tendo la ndoa, haki ya wapi hiyo?.

Tutakuwa na shule za namna gani zinazoruhusu mwanafunzi kwenda kulea mtoto kisha arudi tena na akipata mimba nyingine aende tena nyumbani?” Amehoji Askofu Dallu.

Katika hatua nyingine Askofu Dallu amewaasa waamini kufanya maandalizi ya kutosha hasa ya kiroho wanapojiandaa kuingia katika Sakramenti ya Ndoa ili ndoa zao ziwe na mwelekeo wa kiimani zaidi. Amesema kuwa kabla ya kupewa upadri, Shemasi Jerome alihudhuria mafungo ya kiroho ya siku 5 jambo ambalo linapaswa kuigwa na wale wanaojiandaa kupokea Sakramenti ya ndoa badala ya kujikita katika kufanya maandalizi ya kimwili.

“Watu wa familia mnatumia siku ngapi kufanya mafungo kabla ya kufunga ndoa? Au ndiyo ile kufanya maandalizi mengine ya kimwili marefu. Mkumbuke kuwa hata sisi mapadri tunatoka kwenu, matokeo ya kukosa maandalizi ya kutosha kabla ya ndoa ndiyo haya tunayoshuhudia sasa hivi ambapo wanaoishi ndoa kama Sakramenti ni wachache,” ameeleza.

Aidha amesema kuwa watu wanaoishi maisha ya pamoja kwa muda mrefu hadi kuwa na watoto hawastahili kuitwa wachumba kwa kuwa uchumba kielelezo chake ni Maria na Yosefu, na kuwataka kuacha kutumia jina hilo na badala yake wajiite wachumba sugu.

“Ulisikia wapi watu wanaishi uchumba mpaka wanakuwa na wajukuu? Tafuteni jina jingine kuanzia sasa labda mjiite wachumba sugu. Tutapata mapadri na masista wa namna gani? Kielelezo cha uchumba ni Yesu na Maria,” Ameeleza.

Pia amesema kuwa kazi ya karama ni kujenga umoja wa Kanisa na siyo kuligawa, na kumtaka kila mmoja kutumia wito wake kumtajirisha mwingine.
View attachment 547182

Chanzo:Gazeti la Kiongozi..
Sijasoma yote! Ila itoshe tu kumwambia hata Roman Catholic sii utamaduni wetu Waafrika! Zetu ni chini ya miti mikubwa na Mawe Makubwa na Mapango!

Kama tunataka Uafrika wetu tuondoe hadi hizo shule na makanisa na Serikali na chochote kisicho originate Africa!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Askofu kaharibu...yaani bora angeendelea kunyamaza tu...
Kuna majimbo na mashirika yanapokea watoto waliozaliwa nje ya ndoa kwa ajili ya daraja takatifu la upadre......sasa kama kwenye upadre watoto wa kiume wanakubaliwa sembuse wazazi wao ambao ndo walopata hizo mimba wakiwa bado shuleni wakataliwe kurudi shule?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
KUMBE!!!
Mimi ningemuelewa zaidi huyu mtumishi wa Mungu kama angesema, ni "marufuku mwanafunzi kujiingiza kwenye mambo ya ngono, pia ni marufuku kuvunja amri ya kuzini hata kwa wasio wanafunzi" sasa kauli yake imeacha mpenyo wa wanafunzi wafanye ngono ila OLE wao wakikamatwa hasa hawa wasichana, shule basi. Hapa naona anaikuza biashara ya kondom.
Hapo kwenye red, huoni kama kanisa limeshabikia matumizi ya kondom kupitia kauli yake. Fafanua kama sio kweli alimaanisha nini kwamba wasichana wakipata mimba hakuna kurudi shuleni! Maana yake ili usipate mimba tumia kondom#$!? Logic ya kawaida tu hii
Ni sawa lkn Hata kutofanya zinaa hatopata mimba kabisa husimamia haki,(kutofanya zinaa) kwenye logic ya kawaida husimamia batili(kondom)
 
Ni wapi ameruhusu hayo yote uliyoyasema. Sijawahi kusikia kiongozi yeyote akikubali uchafu unaoutaja wewe.
Kwa kuwekea mkazo mimba, basi naturally vijana watahakikisha hawapati mimba kwa kutumia moja wapo ya uchafu nilioutaja
 
.
Mila zetu afrika ni za kuhurumiana kusaidiana na kuthaminiana. Hivyo katika familia zetu mtoto akimyea mzazi, hatupwi wala kunyimwa haki zake za msingi kama mtoto
Taboo zetu zinasemaje kuhusu kujamiiana kabla ya ndoa...??

Je! Wajibu wa mwanafunzi nini..?
 
Askofu yuko sahihi. Je watoto wanaopata mimba kwani wako kwenye ndoa?kusema waendelee na masomo ni kusema waendelee na uzinzi japo kuna wazinzi sugu ambao hawapati mimba .
Ok kwanni ssa wasiseme asiye bikra pia atimuliwe shule??? Mimba na maadili vina uhusiano gani???
 
ASKOFU Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki Songea Mhashamu Damian Dallu amesema kuwa anaunga mkono hatua ya Rais John Magufuli kutoruhusu wanafunzi wanaopata ujauzito kuendelea na masomo, na kusema kuwa shule zinazomilikiwa na Kanisa Katoliki hazitaruhusu wanafunzi wanaopata ujauzito kuendelea na masomo.

Amesema hayo katika Ibada ya Misa Takatifu ya Upadrisho wa Shemasi Jerome Mtatifikolo, iliyofanyika katika Parokia ya Bikira Maria Afya ya wagonjwa Ilole jimboni Iringa ambapo amebainisha kuwa wanaoshabikia wanaopata mimba kurudi shule wanaharibu utamaduni wa kiafrika na kuchafua heshima ya Taifa.

“Hayo mambo siyo sehemu ya utamaduni wetu wa Afrika, ni mambo ya kigeni yanayotaka kutuchafulia utamaduni wetu. Nawashangaa eti wanapigania haki ya tendo la ndoa, haki ya wapi hiyo?.

Tutakuwa na shule za namna gani zinazoruhusu mwanafunzi kwenda kulea mtoto kisha arudi tena na akipata mimba nyingine aende tena nyumbani?” Amehoji Askofu Dallu.

Katika hatua nyingine Askofu Dallu amewaasa waamini kufanya maandalizi ya kutosha hasa ya kiroho wanapojiandaa kuingia katika Sakramenti ya Ndoa ili ndoa zao ziwe na mwelekeo wa kiimani zaidi. Amesema kuwa kabla ya kupewa upadri, Shemasi Jerome alihudhuria mafungo ya kiroho ya siku 5 jambo ambalo linapaswa kuigwa na wale wanaojiandaa kupokea Sakramenti ya ndoa badala ya kujikita katika kufanya maandalizi ya kimwili.

“Watu wa familia mnatumia siku ngapi kufanya mafungo kabla ya kufunga ndoa? Au ndiyo ile kufanya maandalizi mengine ya kimwili marefu. Mkumbuke kuwa hata sisi mapadri tunatoka kwenu, matokeo ya kukosa maandalizi ya kutosha kabla ya ndoa ndiyo haya tunayoshuhudia sasa hivi ambapo wanaoishi ndoa kama Sakramenti ni wachache,” ameeleza.

Aidha amesema kuwa watu wanaoishi maisha ya pamoja kwa muda mrefu hadi kuwa na watoto hawastahili kuitwa wachumba kwa kuwa uchumba kielelezo chake ni Maria na Yosefu, na kuwataka kuacha kutumia jina hilo na badala yake wajiite wachumba sugu.

“Ulisikia wapi watu wanaishi uchumba mpaka wanakuwa na wajukuu? Tafuteni jina jingine kuanzia sasa labda mjiite wachumba sugu. Tutapata mapadri na masista wa namna gani? Kielelezo cha uchumba ni Yesu na Maria,” Ameeleza.

Pia amesema kuwa kazi ya karama ni kujenga umoja wa Kanisa na siyo kuligawa, na kumtaka kila mmoja kutumia wito wake kumtajirisha mwingine.
View attachment 547182

Chanzo:Gazeti la Kiongozi..
 
Hili kanisa huwa siliamini kabisa,naona kama ni saccos tu.
Kuna mambo wao wakifanya hawawezi kuyakemea,kama Askofu Kilaini mpaka sasa ana hudumu uku akiwa na kashfa ya kuongwa pesa za Escrow. Kwenye jambo kama hilo hautowaona wakifungua mdomo kabisa.
 
Nimeipenda sana hii post. Mimi ni mromani mfu. Siku hizi siendi kanisani kutokana na unafiki ninaouna wazi kwa viongozi wetu. Kwenda huko ni kwenda kukwazana tu. Safari hii ni kuhakikisha tunasimamia ukweli na sio kuwategemea viongozi wa dini kwani hao ni baadhi ya watu wanafiki wa kutupwa.
Unakwenda Kanisani ili kusikia kile unachokitaka..??
 
Maaskofu wamesahau maandiko ya kuhukumu???
Ndo maana nilibaki kuisoma Biblia tu na sio kwenda kanisani kwa unafki na ujinga wa hawa maaskofu uchwara

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwaiyo wewe unapenda upate msamaha bila kuomba msamaha. Mbona yesu alipokuta watu wamegeuza hekalu kuwa mpango la wanyangani hakuwasamehe bali aliwafukuza wote . tusitumie biblia vibaya kwa kisingizio cha yesu kusema msamehe mtu saba Mara sabini. Hiyo mpya ya kutoa msamaha kabla ya kosa. Na sijawahi kuona kwenye biblia sehemu ambapo wamesamehe kosa kabla haijafanyika
 
Hawa Maaskofu hopeless, mbona wao wanalaumiwa kwa kufira watoto wa altar, wanazini tena na wake za watu, wamewapa wasichana wa kwaya mimba, wanasamehewe. Wanaona ugumu gani kuwasamehe hawa watoto. Hovyo kabisa eti maaskofu , uozo mtupu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
18 Reactions
Reply
Back
Top Bottom