Askofu Dallu: Kanisa Katoliki halifungamani na siasa. Kutoza kodi miradi na vibali vya Wamisionari ni uonevu

barafu

JF-Expert Member
Apr 28, 2013
6,726
32,818
image.jpeg

ASKOFU Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki Songea Mhashamu Damian Dallu amesema kuwa wamisionari hawakuja nchini kama wawekezaji bali ujio wao ulilenga kumkomboa mwanadamu kiroho na kimwili, na ndiyo chanzo cha utoaji wa huduma za msingi za kijamii ikiwemo elimu, afya na maji.

Ameeleza hayo hivi karibuni katika Adhimisho la Misa Takatifu ya kutoa Daraja Takatifu ya Upadri kwa aliyekuwa Shemasi Jerome Mponzi, katika Parokia ya Nyakipambo Jimbo Katoliki Iringa.

Askofu Dallu amesema kuwa wamisionari hawakujikita katika utoaji wa huduma za kiroho pekee, bali walihakikisha mwanadamu anakombolewa mzima mwili na roho, ndiyo maana walipojenga Kanisa walijenga pia vituo vya afya, hospitali au zahanati, shule na miradi ya maji.

“Sisi ndiyo tulioanzisha utoaji wa huduma za jamii kwa wananchi wote bila kubagua. Baada ya Serikali kuamka ndipo Mwalimu Nyerere akataifisha shule na miundombinu ya afya ili kuimarisha umoja wa kitaifa. Wazee wetu watangulizi walilielewa hili na hawakupiga kelele kwani waliona ni jambo jema linalowanufaisha watu wote. Baada ya muda huduma hizi zilizorota ndipo katika awamu ya pili baadhi yake zikarudishwa mikononi mwa Kanisa, na kisha Serikali kuingia mkataba ili wamisionari waendelee kutoa huduma kwa ufanisi zaidi, kwa manufaa ya wengi, huku Serikali ikisaidia,” amesema.

Aidha Askofu Dallu ameongeza kuwa inashangaza kuona mtawa aliyekuja nchini mwaka 1950, akajitoa kuhudumia jamii bila faida, anafuatwa na kudaiwa kibali cha kufanya kazi nchini na kumtaka alipe kodi, na kusisitiza kuwa huku ni kumfanya mmisionari kuwa kama mfanyabiashara, jambo ambalo siyo sahihi.

“Sisi siyo dini ya mtu wala hatuna mwelekeo au msukumo wa kisiasa. Hatuhitaji upendeleo wa mtu bali tunafuata utaratibu uliowekwa. Tumesajiliwa chini ya Wizara inayohusika na Katiba na Sheria, hatujasajiliwa chini ya Wizara inayohusika na mambo ya ajira,” ameongeza.

Akikumbushia juu ya Waraka wa Baba Mtakatifu Leo XIII uitwao ‘Rerum Novarum’, Askofu Dallu ameeleza kuwa kuna haja ya kujikita katika mfumo wa elimu unaolenga kujenga dhamiri za wasomi, ili kuliepusha Taifa dhidi ya watumishi wasio waadilifu.

Marufuku kubinafsisha karama

Pia Askofu Dallu ametoa angalizo kwa Vyama vya Kitume na waamini nchini kutobinafsisha karama, na badala yake kumtambulisha Kristo kupitia yale yote wanayoyafanya. Ameonya tabia ya watu kutaka kuonekana wao katika mambo wanayoyafanya na kumuweka pembeni Kristo, jambo linalochochea dharau dhidi ya viongozi wa kiroho.

“Kupitia karama zenu hakikisheni mtu anamuona Kristo na siyo ninyi. Chochote mnachokifanya ni lazima aonekane Kristo kwanza. Msitumie karama kufanya biashara. Na isitokee watu wanasali kwa ajili ya kuponywa tu, matokeo yake tutakuwa na makanisa ya wagonjwa, kwani wote watakaohudhuria watakuwa wagonjwa isipokuwa yule anayeombea. Huu ni mwanzo wa wakristo kuwa watumwa wa mwombeaji, na ni kinyume na maagizo ya Kristo ambaye alipowaponya watu aliwaambia waende zao,” ameeleza.
 
Wakatoliki walianzia Congo Brazzaville ambako kulikuwa na himaya kubwa ya u-Katoliki chini ya mfalme Leopard, hatimae ulifika Uganda na kuenea Kagera laking Church of England waliamua kujenga chuo Unguja kitakachotoa mapadre, waalimu na wapishi

Chuo hiki kilianzia Kiungani Zanzibar na wanafunzi wake wa kwanza walikuwa ni watumwa waliokombolewa kabla ya kusafirishwa kwenda Arabuni
 
Wakatoliki walianzia Uganda na jubilant Kagera lakini Church of England waliamua kujenga chuo Unguja kitakachotoa mapadre, waliamua na wapishi

Chuo hiki kilianzia Kiungani Zanzibar na wanafunzi wake wa kwanza walikuwa ni watumwa waliokombolewa kabla ya kusafirishwa kwenda Arabuni
Very true!
Na pia waliweka barrier kule kusini (Masasi) na waliwanunua watumwa waliokua wanapelekwa Kilwa na Mikindani.
Wakajenga hospital (Mkomaindo) na camp yao iliitwa " rest camp" ambayo sasa hivi ni mtaa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wakatoliki walianzia Uganda na jubilant Kagera lakini Church of England waliamua kujenga chuo Unguja kitakachotoa mapadre, waliamua na wapishi

Chuo hiki kilianzia Kiungani Zanzibar na wanafunzi wake wa kwanza walikuwa ni watumwa waliokombolewa kabla ya kusafirishwa kwenda Arabuni
Very true!
Na pia waliweka barrier kule kusini (Masasi) na waliwanunua watumwa waliokua wanapelekwa Kilwa na Mikindani.
Wakajenga hospital (Mkomaindo) na camp yao iliitwa " rest camp" ambayo sasa hivi ni mtaa..RC walikuja badae sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Very true!
Na pia waliweka barrier kule kusini (Masasi) na waliwanunua watumwa waliokua wanapelekwa Kilwa na Mikindani.
Wakajenga hospital (Mkomaindo) na camp yao iliitwa " rest camp" ambayo sasa hivi ni mtaa..RC walikuja badae sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
Uko sahihi mkuu watumwa wengine hawakujua wanataka wapi lakini walipofikishwa Mtwara walisema panafanana na kwao na waliamua maisha pale
 
Tandika kodi hao..! Wakristo waslamu wote piga kodi..! Kwanza humo ndo wanakopitishia vigari vyao pale bandalini kwa mwanvuli wa mali ya taasisi ya kidini..!

Sent using Jamii Forums mobile app
Piga kodi mpaka sadaka.

Dini ni siasa na siasa ni uchumi.

Ama piga kodi mpaka sadaka, ama futa kodi katika kila kitu, mpaka pombe.

Sent from my Kimulimuli
 
Nimependa hii. Siku zote nilikuwa nikajiuliza kanisa katoliki liko wapi Kwa yanayoendelea nchini.
Zile nyaraka zilizokuwa zikitolewa mara Kwa mara wakati wa utawala wa jk, sasa ziko wap!?
Muda ni mwalimu mzuri Sana, na pia husemwa kuwa, Kwa kujifanya huoni na kushindwa kukemea udhalimu unaofanywa Kwa mwenzako Kwa kigezo kuwa wewe haya kuhusu,ni kakudanganya kwani mdhalimu akiwamaliza wato atakugeukia wewe uliyejidangaya kuwa hayakuhusu!
Kanisa limekaa kimya ilihali waumini wake wakiumizwa, likafikiri halitaguswa. Sasa mambo yamegeuka ndio tunaanza kusikia sauti kama hizi za askofu Dallu.
Ukisoma gazeti la mwananchi la leo utasikitika Kwa kuwa kuna matukio lukuki ya uonevu lakini hakuna wa kukemea. Kanisa limefunga ndoa na bado wako ktk fungate, huku uonevu ukifanyika.
Duh, kanisa hili halina tofauti na wale viongozi wa dini enzi za Yesu. Nasikitika kuwa muumini wa kanisa linalofumbia macho uonevu.
 
Wakatoliki walianzia Congo Brazzaville ambako kulikuwa na himaya kubwa ya u-Katoliki chini ya mfalme Leopard, hatimae ulifika Uganda na kuenea Kagera laking Church of England waliamua kujenga chuo Unguja kitakachotoa mapadre, waalimu na wapishi

Chuo hiki kilianzia Kiungani Zanzibar na wanafunzi wake wa kwanza walikuwa ni watumwa waliokombolewa kabla ya kusafirishwa kwenda Arabuni
whats ya point bibie?
 
Back
Top Bottom