M-mbabe
JF-Expert Member
- Oct 29, 2009
- 13,203
- 23,020
Asante Baba Askofu Bagonza.
Kama kawaida yako, umeendelea kutufundisha Watanzania njia sahihi ipasayo kuzingatiwa katika ucha Mungu wetu kila iitwapo leo.
Mungu akutunze baba yetu.
=======
Anaandika Bagonza ( PhD)
CORONA: TUOMBE, TUSIOMBEOMBE
Vita dhidi ya Corona haiepukiki. Napendekeza haya:
1. Mungu haongei nasi kutumia Corona. Tunaalikwa kuongea na Mungu kwa tishio la Corona.
2. Katika vita kuna kujilinda na kushambulia adui. Tumesikia mbinu nyingi za kujilinda na chache za kushambulia Corona.
3. Tutangaze tunapofunga goli na tunapofungwa. Hofu ya kufungwa inaongeza mbinu za kujilinda. Watu wakiona na kusikia habari za watu wanaowajua, wataelewa kirahisi hatari inayotukabili.
4. Tuwalinde wachezaji wetu kwa gharama. Watumishi wa afya nchini kote, wapewe vifaa vya kujilinda na watengewe maeneo ya kukaa. Wasirudi majumbani.
5. Vifaa vipatikane na vijulikane viko wapi. Wenye uwezo wajinunulie na wawanunulie wasio na uwezo.
6. Visivyopatikana nchini viagizwe. Msamaha wa kodi utangazwe na ukiritimba wa kuviingiza uondolewe haraka. Mashirika yahanasishwe kuagiza haraka.
7. Tusitishe vyombo vya usafiri kutoka mkoa kwenda mkoa. Hivi sasa kirusi chaweza kuwa Ubungo asubuhi na jioni kikawa Kahama. Barabara nzuri na Bombadier hazisafirishi bidhaa tu. Hata virusi vinapata lifti.
8. Mashine za kupima virusi zipelekwe kila mkoa.
9. Elimu isisitizwe kuliko adhabu. Usugu wa adhabu utaongeza kasi ya maambukizi. Polisi wapige virusi, wasipige watu.
10. Tufunge na kuomba lakini tukumbuke Corona ni tatizo la kisayansi zaidi kuliko kuwa tatizo la kiroho. Tuombe, tusiombeombe.