BAK
JF-Expert Member
- Feb 11, 2007
- 124,789
- 288,011
Ujumbe wa baba Askofu Dr.Benson Bagonza (PhD), mkuu wa KKKT Dayosisi ya Karagwe.
____________________
Mwaka 2015 hatukuchagua malaika kuwa serikali. Tulichagua watu wenye ubinadamu. Watu hao na udhaifu wao wakaunda serikali. Serikali iliyoundwa na binadamu dhaifu, haiwezi kuwa takatifu kama malaika.
Kwa hiyo serikali ni dhaifu, kwa sababu imeundwa na watu dhaifu, na ilichaguliwa na watu dhaifu. Udhaifu maana yake ni "si kamilifu", "si takatifu" na ina uwezekano wa kufanya makosa.
Madaraka hayaondoi udhaifu. Madaraka si chanjo ya kuzuia kufanya makosa.
Kwa hiyo, nafasi au madaraka hayakingi uchoyo, ubabe, ulafi, uwongo, fitna, ukatili, upendeleo, ukabila, udini, ujinga, maradhi, na hila. Kisingizio cha "kufanya siasa" si kinga ya kuzuia madhara ya udhaifu huo.
Hali kadhalika, kutambua udhaifu si tiketi ya kuendelea kufanya makosa.
Kukubali kuwa unaweza kufanya makosa, ni ibada inayokubalika mbele za Mungu kwa sababu ni ukiri (admission) kuwa wewe si Mungu bali mwanadamu.
Kukiri udhaifu ni kupata nguvu, si kupoteza nguvu. Kunyenyekea ni kuhifadhi nguvu si kuogopa. Hapa ndipo tunakutana na tofauti kati ya ukatili na ujasiri, uungwana na unyonge.
Kama ningechagua, ningemheshimu anayenipa chakula kuliko anayeninyima chakula ili nimjue ana madaraka juu yangu.
Haki huanzia pale tunapokubaliana kuwa sisi ni binadamu wenye udhaifu katika kufikiri, kunena, kutenda. Waliopewa mengi, wadaiwa mengi. Yatosha siku kwa uovu wake.
Hasira ya Mwanadamu haitendi haki ya Mungu. Kisasi ni kwa Bwana wa visasi vyote, anayependa rehema kuliko sadaka!
Baba Askofu Bagonza