Askofu Bagonza: Wanaodhani wana furaha hawana furaha. Wapinzani hawana furaha, wapinzani wa wapinzani hawana furaha

Elli

Platinum Member
Mar 17, 2008
55,499
86,037
FURAHA KAENDA WAPI?

Waliopiga kura hawana furaha, Waliosusa/suswa hawana furaha. Waliopita bila kupingwa hawana furaha, Waliosimamia kura hawana furaha. Walioshinda hawana furaha, Walioshindwa hawana furaha

Waliopanga yaliyotokea hawana furaha, Waliopangiwa yaliyotokea hawana furaha. Walioshauri hekima hawana furaha. Waliokaa kimya hawana furaha, Wanaounga mkono nilichoandika hapa, hawana furaha. Wanaopinga nilichoandika hapa, hawana furaha

Wanaodhani wana furaha hawana furaha, Wapinzani hawana furaha. Wapinzani wa wapinzani, hawana furaha. ILA wanaodhani hawana furaha, ni KWELI hawana furaha. Ni bora kujiuliza huyu furaha yuko wapi?
*****

Askofu wa Dayosisi ya Karagwe ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Benson Bagonza ametaja makundi 14 ya watu anaodai hawana furaha kutokana na uchaguzi wa viongozi wa serikali za mitaa nchini Tanzania uliofanyika jana Jumapili Novemba 24, 2019.

Askofu Bagonza ametoa andiko jipya leo Jumatatu Novemba 25, 2019, ikiwa ni siku moja baada ya kufanyika kwa uchaguzi huo ambao kwa sehemu kubwa wagombea wa chama tawala CCCM wamepita bila kupingwa maeneo mengi.

Katika andiko lake hilo ambalo linasambaa katika mitandao ya kijamii ikiwamo makundi ya WhatsApp, Askofu Bagonza anasema waliopiga kura hawana furaha na waliosusa au kususwa hawana furaha.

Anasema waliopita bila kupingwa nao hawana furaha, waliosimamia kura hawana furaha, walioshinda hawana furaha na hata walioshindwa hawana pia furaha na uchaguzi huo

Katika andiko hilo, Askofu Bagonza anasema waliopanga yaliyotokea hawana furaha, waliopangiwa yaliyotokea hawana furaha na walioshauri hekima hawana furaha.

Anasema kutokana na uchaguzi huo, waliokaa kimya hawana furaha, wanaounga mkono nilichoandika hapa hawana furaha na wanaopinga anachoandika hapa, hawana furaha.

“Wanaodhani wana furaha pia hawana furaha. wapinzani hawana furaha, wapinzani wa wapinzani, hawana furaha. Wanaodhani hawana furaha ni kweli hawana furaha na kuhoji furaha yuko wapi,” anasema

Uchaguzi wa serikali za mitaa umefanyika jana Jumapili huku vyama sita vya upinzani vikisusia uchagizi huo ambavyo ni Chadema, CUF, NCCR Mageuzi, UPDP, Chaumma na ACT- Wazalendo.

====
Michango ya wadau

Viva baba Askofu na viongozi wote wa KKKT na makanisa ya kipentekosti!!

Miaka ya nyuma maaskofu na mapadre wa kanisa katoliki walikuwa wanasifika kuwa ni wasomi na wenye elimu kumbwa ya Mungu na duniani pia. Hata waumini wao walitembea vifua mbele kujivunia na kuwategemea viongozi wao badala ya kumtegemea Mungu. Ulikuwa jambo la kawaida muumini wa kanisa katoliki kutojua bibilia kabisa na akajiona bado yuko kwenye njia sahihi kutokana na viongozi wao.

Miaka hii mambo yamebadilika, maaskofu na mapadre wa kanisa katoliki ndiyo vibaraka na kichaka cha shetani. Hapa kwenye kichaka cha shetani kimezidi kwani toka hapo nyumba walishakuwaga maswahiba na shetani.

NB: Mimi pia ni mkatoliki aliyechoshwa na unafiki wa viongozi wake wa dini.
 
Nilishawahi sema PHd ya Bagonza Ni feki .Huo utafiti wa wasio na furaha nchi nzima kaufanya wapi?

PhD kazi yake ni kushusha takwimu sio hisia au halucinations

Chuo gani kilimtunuku hiyo PhD? Anaongea Kama mlevi Hana takwimu hata moja veriafiable na reliable
 
Nilishawahi sema PHd ya Bagonza Ni feki .Huo utafiti wa wasio na furaha nchi nzima kaufanya wapi?

PhD kazi yake ni kushusha takwimu sio hisia au halucinations

Chuo gani kilimtunuku hiyo PhD? Anaongea Kama mlevi Hana takwimu hata moja veriafiable na reliable

Jiwe gizani.

Sisi PhD yake haituhusu tunaangalia kile anachokisema je kina ukweli?

Yule sio Pengo wala Nyaisonga.
 
Hiv nani mwenye furaha!?
Ule utafiti uliotolewa wa mwaka 2018 kuwa Tanzania ilikuwa inashika nafasi ya sita toka mwisho kwa kukosa furaha duniani nadhani takwimu za sasa baada ya uchaguzi huu wa SM tutashindania nambari moja sisi na Afganistani. Na pengine tukawashinda kwa kishindo na kuwa taifa namba moja kwa ukosefu wa furaha.
Hapo hatuna vita, hatuna njaa wala majanga makubwa kama vimbunga,tetemeko au mafuriko, bali time"bahatika" kuwa na CCM.
 
Back
Top Bottom