Askofu Bagonza: Wakimaliza ya kwenye simu, watahamia Hospitali, Mikopo yetu. Toba zetu na vitubio havitakuwa siri tena

Ameandika Asikofu Dr Kalikawe Lwakalinda Bagonza PHD

TUAZIME TENA HEKIMA YA WANYAMBO

"Nyani asiyekomaa bado (mchanga), huangua kicheko aonapo msitu ukiteketea". Kwa uchanga wake huwa hajiulizi usiku atalala wapi?

"Mtoto mtundu aliyezoea kutukana watu wazima, huwa haishii kwa mmoja".

Tumesikia mengi ya sirini. Hatukupaswa kuyasikia. Nini kinafuata?

1. Wakimaliza ya kwenye simu, watahamia hospitali. Majipu yetu, damu zetu, mikojo yetu, mate yetu, na vinyesi vitaanikwa!

2. Mikopo yetu na bill za baa zisizolipwa zitajukikana. Usisahau mkopo wa nyama wa mwaka jana wakati sasa unakula kisamvu!

3. Toba zetu na vitubio havitakuwa siri tena maana vitaanikwa. Bajameni, acheni kuwasumbua kwa simu watubishaji wenu. Hawana uhakika tena wa kutunza mambo yenu.

4. Kama wana siri hizo, hata "password" za ATM hazina haja tena. Akiba zetu ni akiba zao. Kukwapua mikoba hakufai tena, watu wanachukua wanachopenda kwa kuwa wanamiliki siri zetu.

Bi Kidude hata kama hakuwa Mnyambo, aliwahi kusema "Kunambia siri kisha ukasema nisimwambie mtu, mie siwezi kwa sababu hata wewe umeshindwa kutunza ukaniambia mimi".

Tumejiruhusu kuona "uchi wa mama zetu", acha tupatwe na upofu!!
Gombea ubunge tujue kama ni mwanasiasa
 
Huyu jamaa hua namkubali sana!
 
Bi Kidude hata kama hakuwa Mnyambo, aliwahi kusema "Kunambia siri kisha ukasema nisimwambie mtu, mie siwezi kwa sababu hata wewe umeshindwa kutunza ukaniambia mimi".

Tumejiruhusu kuona "uchi wa mama zetu", acha tupatwe na upofu!!
kweli mkuu kama mama kaamua kuachia wazi macho hayana pazia...wacha tupate upofu - lah.

haya mambo ni makubwa sana!! hii ni fita fita muraaa!!
 
Vua joho ujiunge na siasa baba askofu!
Kama unaona ni sahihi kiongozi wa nchi kutukanwa, maandiko unayohubiri kanisani unatufundisha tutii mamlaka!
Wewe endelea na mahubri, acha serikali ifanye yake, kama huna makandokando hofu ya nini?
Hivi huku kutkanwa mkuu wa Nchi naona kunazungumzwa sana na hata viongozi wengine wale mihemko wameingia kwenye mtego huo huo! nimeusoma ule waraka wa kina Mzee Makamba na Kinana na kuurudia mara nyingi tu sijaona mahali popote walipotoa hata tusi moja si kwa huyo Musiba wala Kiongozi yeyote. Sioni sababu ya kumhusisha Mkuu wa Nchi na waraka wa hawa wazee wetu. Au kusema kwamba Musiba anajiamini pengine kwa sababu anaona kuna watu wakubwa na wenye nguvu nyuma yake? jamani hivi kusema kuna watu nyuma ya Musiba ni Matusi kwa Mkuu wa Nchi? Hao watu wenye nguvu walio nyuma ya Musiba mmeshathibitisha kwamba ni Mkuu wa nchi? na wengine ni akina nani mbona hamuwatetei ? au wao ndiyo hayo matusi mnayoyatunga ni stahiki yao? mbona issue ya kutukanwa kwa hawa wazee na Musiba hakuongelewi kabisa? tuwe wakweli sio kumwingiza mwingiza Rais kwenye mambo ya hovyo hovyo kama haya eti kwa kisingizio cha kumtetea ni kumvunjia heshima yake zaidi.
 
Pammbaffff na msiingie kwenye masinagogi huku mmijawa na unafikiuna
 
Hawa mazwazwa wa lumumba skuizi wamegeuza mijadala ya kumkosoa Jiwe ni matusi. Wamesahau kuwa inamuamsha kutoka usingizini
Screenshot_2019-07-26_234253.jpg
 
Hongera sana baba askofu kwa kutokuwa mnafiki kama viongozi wengine wa dini wanaonyamazia maovu ,utekaji ,uuaji ,na ukiukaji wa haki za binadamu ilhali wana macho ,mdomo na masikio Mungu akulinde na akupe maisha marefu .
 
Na wewe upo tu bendele fuata upepo. Anatukanwa Trump na wala haogopi, itakuwa huyu? Kwani mtu kuwa Rais ubinadamu unaondoka?

Back
Top Bottom