Mwanahabari Huru
JF-Expert Member
- Mar 9, 2015
- 14,243
- 34,899
Kumjua adui ni nusu ya ushindi. Tanzania ya viwanda kwa sasa ina maadui wakubwa wawili: wa kwanza ni neno "kufuta" na wa pili ni neno "kutaifisha". Tukiwajua maadui zetu hawa wawili, ndoto ya viwanda itawezekana.
Maneno haya mawili yakikaa midomoni mwa watawala, yanafukuza uwekezaji, yanatishia usalama wa mitaji na kuyeyusha uthubutu katika kukopa na kudhoofisha kujiamini katika kutumia (consumer confidence).
Uchumi wa soko huria hutawaliwa na usalama wa mitaji na kuheshimu sekta binafsi na mali zake. Soko huria hushamiri mahali palipo na uhuru wa kujumuika, kuungana, kutengana na kushiriki. Maneno "kufuta" na "kutaifisha" ni sumu ya uhuru huo.
Maendeleo katika uchumi wa utandawazi ni UHURU, siyo vitu wala fedha. Tanzania ya viwanda inawezekana bila matumizi ya "kufuta" na "kutaifisha".