Askofu Bagonza: Kuna watu wanasali Novena kumlilia Mungu leo siku ya tano

Anaandika Askofu Bagonza

Chanjo Mbowe ,Katiba mpya, Tozo za miamala na Rais Samia.

Mambo haya 5 yameshikilia mustakabali wa nchi kwa sasa. Amani, haki, Maendeleo na ustawi vinatikiswa. Jiulize...
Mungu wetu atajibu kwa uaminifu na tutaona matendo makuu ya Mungu!
 
Usinichokoze.

Mie nasema kwamba hiyo tuhuma ni ndogo. Kuna kubwa zaidi. Kwa mfano, Mbowe alifadhili matukio ya ughaidi wa mabomu ya Olasiti Arusha.

Watu kadhaa walikufa. Msimamizi Mkuu wa ughaidi huo alikuwa mwanachadema aitwaye Mohammed Mtoi. ..
Huu ushahidi uliwahi kuuripoti polisi? hilo tukio la bomu na ajali uliyounganisha havina uhusiano wa moja kwa moja, umetengeneza picha yako kichwani ukatuwekea hapa tuisome, ushahidi zaidi unahitajika.

Sasa ngoja nikupe tukio moja lenye uhusiano wa moja kwa moja; lile bomu la Soweto ni nani alielipua? na ni nani aliewaambia wafuasi wa Chadema siku ile ya mkutano kuna bomu litalipuka hivyo kwa usalama wao wasiende kwenye ule mkutano? jibu unalijua, kama hulijui ni Madelu.
 
kumeibuka watu wqanaojiita maaskofu kumbe niwachumia tumbotu kama huyu aliyeharisha hapa na yule mwenzie mwanaharakati uchwara mwamakula wanaingilia mambo yasiyowahusu na ndiyo maana hawatafaulu katikaharakati zao....
Niliposoma hoja yako ya pili nikagundua wewe kwa Elimu yako ya ngumbalo huwezi mjibu baba askofu. Yaani wewe kwa uelewa wako Wana ccm Ni viongozi tu?

Sasa nikuambie mie wazazi wangu ni wafia dini wa ccm. Lakini hawataki kabisa kusikia hiyo kitu inaitwa chanjo. Huo ni mfano tu lakini Kuna kundi kubwa Sana la Wana ccm hawataki chanjo. Shida yako upo maporini huko unalima ulezi huwezi jua yanayoendelea duniani
 
kumeibuka watu wqanaojiita maaskofu kumbe niwachumia tumbotu kama huyu aliyeharisha hapa na yule mwenzie mwanaharakati uchwara mwamakula wanaingilia mambo yasiyowahusu na ndiyo maana hawatafaulu katikaharakati zao.

1. hakuna sehemu serikali imetumia nguvu kuwataka watu wakachanjwe maana ni hiari na siyo lazima kwahiyo huyu jamaa ni muongo.

2. hakuna mwana ccm aliyepinga chanjo umeona ni kiongozi gani wa ccm ameibuka na kuipinga chanjo? huo ni uongo na uzandiki.

3.suala la mbowe wanaolivalia njuga kulipinga ni wana chadema pekeyao ulishaona mwana ccm analizungumzia suala ambalo liko mahakamani? usimhusishe kila mtu hao nchadema pekeyao.

4.suala la tozo mmeshaambiwa linashughurikiwa kwanini mnalifanya kama ajenda tena?

5.suala la katiba liko chadema lini umelisiukia kwa ccm huo ni uongo na askofu muongo huyo siaskofu bali ni mchumia tumbo mmekula hela za mabeberu zitapikeni tu hamna jinsi

Mengine yote hayana umuhimu askofu acha uchnganishi kama umekula hela za watu rudisha ulinde heshima yako najidharirisha
Hivi wewe una akili kweli??unajua 99%ya umasikini wetu unaletwa na katiba mbovu...raisi sio Mungu anafanya makosa awamu zote sita wangekuwa jela Sasa hivi..
 
Anaandika Askofu Bagonza


Chanjo Mbowe ,Katiba mpya, Tozo za miamala na Rais Samia.

Mambo haya 5 yameshikilia mustakabali wa nchi kwa sasa. Amani, haki, Maendeleo na ustawi vinatikiswa. Jiulize:

1. Kwa nini itumike nguvu na jitihada za ziada kuwaaminisha watu wakachanje wakati afya ni mali yao?

2. Kwa nini wana CCM wapinge chanjo wakati afya ni sera ya ilani yao ya Uchaguzi?

3. Kwa nini suala la Mbowe kufunguliwa mashtaka ya ugaidi linapigiwa kelele na watu bila kujali itikadi zao?

4. Kwa nini tozo za mihamala zimeligawa bunge na serikali na kuusambaratisha uwajibikaji wa pamoja?

5. Kwa nini madai ya Katiba Mpya sasa yanaanza kusikika ndani ya CCM kuliko ilivyokuwa katika awamu ya 5?

6. Kwa nini watu wengi wakiwamo Wana CCM wanamlaumu Rais SSH kwa yote 4 (Mbowe, Tozo, Katiba Mpya na Chanjo)?

Ukweli usiotamkwa
a). Awamu ya 5 ilimwaga sumu kali kupinga chanjo na uwepo wa Corona. Waliopinga chanjo na corona hawawezi kuvinadi leo ikakubalika. Watafutwe wengine kutoka makundi yote.

b). Serikali na Chama tawala vimegawanyika juu ya chanjo. Kila mtu anatamani katiba mpya inayoruhusu Rais kuhojiwa bila ya anayehoji kupata madhara. Kuna wengi waliomuunga mkono lakini sasa wanafikiri vinginevyo.

c). Tuhuma za ugaidi dhidi ya Mbowe zimeligawa Taifa. Zimefuta mazuri yote ya awamu ya 6. Zimechochea madai ya Katiba Mpya. Waliomshauri Rais hawalitakii mema Taifa. Hata chama tawala wanataka haki za Binadamu. Urais uko mnadani.

c). Mpaka sasa mawaziri (wa fedha na Waziri wa Miamala ya simu) hawajatoa hoja zenye nguvu kuhalalisha tozo za juu kwa watumiaji. Wengi wanaona mawaziri wanamhujumu Rais au Rais ameruhusu kuhujumiwa.

d). Rais Samia ni "Rais wa Katiba" kwa mujibu wa Katiba. Kuna "wapotoshaji" pande zote (CCM na Upinzani) wanaosema Rais hapendi katiba mpya kwa sababu hii anaiona nzuri kwa kumleta madarakani. Muungano huu wa "wapotoshaji" si salama kwa Rais. Rais ana fursa nzuri ya kuweka historia. Anaelekea kuipoteza.

Muhimu
Kumshikilia Mbowe kwa tuhuma zinazoonekana "bambikizi", kunaua uwezekano wa maridhiano na mazungumzo ya kuliunganisha Taifa.

Taifa lililogawanyika
-Haliwezi kujibu ushirikina wa
kisomi (conspiracy)

-Haliwezi kuchanja chanjo kikamilifu

-Haliwezi kuingia vita dhidi ya corona

-Haliwezi kuwa na bajeti endelevu

-Linaongozwa na nguvu kuliko akili

-Haliwajibiki kwa pamoja mbele ya
umma

-Huwaona raia kuwa maadui wa Taifa.

Damu isiyo na hatia isipokomboa huangamiza na mateso ya mwenye haki ni hukumu kwa matawala asiyeona dhuluma.

Kuna watu wanaomba Novena leo siku ya 5.
Tunaendelea kumlilia Mungu wa Yakobo
 
Wanaouliza kwa nini Mbowe amekamatwa sasa na si vinginevyo wanasahau kuwa Mbowe, Lema, Meya wa zamani Ubungo Boniface walikamatwa mara baada ya matokeo ya uchaguzi mkuu kutangazwa na kabla Rais hajaapishwa kwa kuchochea maandamano yasiyo na kikomo kupinga matokeo. Mambosasa alihojiwa na vituo vya ITV na TBC na kutoa madai hayo hayo ya ugaidi.
 
62 Reactions
Reply
Back
Top Bottom