Askofu Bagonza(KKKT): Hivi viongozi wa dini wana mipaka kusema juu ya mienendo ya nchi? Hiyo mipaka imeanza lini?

Kuna sehemu Yesu alifanya hayo kiongozi...?
Naomba unioneshe katika maandika matakatifu yanayoruhusu hayo.?
Yesu alikemea rushwa, aliwakosoa wakusanya kodi na askari, akisisitiza watu watende haki. Mbona hayo hamyasemi kwamba aliingilia siasa?
 
Mkuu concept ni simple tu.Hakuna viongoz wa dini Bali wafuasi wa vyama vya siasa wenye makoti ya dini.Pengo anaeleweka ni mfuasi wa CCM, gwajima ni Chadema na kakobe ni Chadema. Sasa hawa watu wote wanatumia makoti ya dini kutimiza malengo yao kisiasa. Huwezi mkuta pengo anakemea ccm au kakobe anawakemea chadema. Na hata huku mtaani maneno ya hawa watu tunayatafsiri kulingana na misimamo yetu kisiasa.

Kuna uzi umeanzushwa humu ukimponda kakobe na bila shaka ni wafuasi wa ccm Na kuna Uzi upo humu unamponda Pengo na bila shaka ni Chadema wanaoponda.Kwa mazingira haya huwezi sema hawa wanahubiri neno la Mungu labda kwa kutumia itikadi za kisiasa ndo utasema hivo.Chadema wanasema kakobe anahubir neno la Mungu Na CCM pia wanasema pengo anahubiri neno la Mungu lkn kwa uhalisia hawa wote Wanahubiri Siasa kwa koti la dini.

Chadema huibuka na kuwaona mashujaa viongoz wa dini pale wanapoiponda serikal na hapa utaona sifa kedekede na CCM huibuka kuwashambulia viongoz wa dini pale wanapoinda serikal au CCM na hapa utaona matusi na kejeli za kila aina.Kwa mantiki hii ni wazi viongoz wa dini hawatimizi wajibu wao zaid ya kuleta mipasuko na chuki ktk dini.NENO LA BWANA haliongezi chuki ktk jamii au kuibua makundi,neno la bwana LINAWAUNGANISHA WATU PAMOJA kwa mantiki hiyo hakuna anayetoa neno la Mungu zaid ya majungu,fitna na unafki kwa koti la dini.
Hopeless kabisa !! Mi nilidhani utasema wanachoongea ni uzushi na uwongo, kumbe nawe unatuletea mitizamo yako ya magengeni. So sad
 
Hopeless kabisa !! Mi nilidhani utasema wanachoongea ni uzushi na uwongo, kumbe nawe unatuletea mitizamo yako ya magengeni. So sad
Huyo jamaa unayemjibu alitakiwa tu aseme fact juu ya siasa na mambo au taaluma zingine. Siasa ina waalimu, kuna mainjinia, kuna matapeli, maprofesa, etc.

Tatizo siyo kuingia ktk siasa. Tatizo ni kuendesha siasa ktk maeneo yako ya kazi tofauti na wenzako. Askofu wetu kama akisimama jukwaani, safi kabisa na atashindana na wengine. Hii ya kuvizia wanaokuja kusali halafu unaanza kupiga siasa ndani ya jengo lako, NO!
Lemmy Ongalla (dr Lemmy) aliwahi imba wimbo kwamba kosa ni letu. Akawataja washona viatu, waimbaji, nk. kuingia ktk siasa. Ukiwa kiongozi wa Dini ukatamani kusema mambo ya siasa, njoo jukwaani ili ukutane na wenzako. Ukibaki kanisani, msikitini ukasema siasa wakati ukielewa wenzako hawaingii kwako kufanya siasa, hapo kuna tatizo. Hii ni sawa na Profesa atakayeamua kuendesha siasa darasani wakati akijua wanasiasa hwaingii huko aliko.
 
Raisi yeye akisimama jukwaani akaongea la moyoni inakuwa hapaswi kusema hivyo ila viongozi wa dini mnasema waachwe.
Kiongozi wa dini anapokuwa kwenye kusanyiko rasmi atachosema ni kauli ya mimbari. Ndo maana wanatakiwa watenganishe mahali pa kusemea mawazo yao na mahali pa kutolea ujumbe wa nyumba ya ibada. Akiwa na mkewe.wanawe.rafiki zake ruksa !! ILA ANAPOVAA VAZI RASMI NA KUSIMAMA MAHALI RASMI PA IBADA KAULI ANAYOTOA SIO YAKE ILA YA CHEO CHAKE. SASA JE !! NAFASI YAKE HIYO NDIO KAZI YAKE?
 
Hueleweki!!
 
Back
Top Bottom